Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Kama yapi?
Magufuli amepiga marufuku mwenge
Magufuli amepiga marufuku sherehe za muungano na pesa kapeleka visiwani zikapambane na corona
Magufuli amefuta mei mosi
Magufuli amefunga shule zote na vyuo
Magufuli amesimamisha michezo yote
Serikali ya magufuli ilitayarisha hosputali zake kwa ajili ya kupokea wagonjwa
Magufuli amesisitiza barakoa na kunawa mikono
Ulitaka Rais wetu afanye nini?mnyonge mnyongeni
Magufuli kasema hayo yoote uliyotaja hapo juu ni upuuzi tu
 
Na kuna watu laki kadhaa waliougua wakakaa tu nyumbani wakajifungia wakapona. Hahah zee jinga hili, mtu moja kupona haimaanishi ni dawa, ingekua hivyo watu milioni waliopona duniani kwa kukaa tu miili yao ikapambana na virusi tungesema hiyo ni dawa kwa hiyo tusifanye lolote.
PhD hivi aligawiwa bure? Au alifanyiwa research na mtu mwingine? Mbona jinga sana?
Mambo haya ni makubwa sana ubongo wako ni kama wa memde hauwezi kuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
magufuli sasa hivi akiongea hotuba zake zinasambaa mpaka ulaya na amerika inakuwa ni gumzo.dunia nzima inatamani kusikia hotuba zake nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
HOTUBA NZURI ZA MAGUFULI? KWELI WEWE UPO MBALI NA UKWELI...HUYO LAUGHING STOCK ANAYESEMWA DUNIANI KWA UJINGA? MBONA HAJAZUNGUMZIA ILE DAWA YAKE FEKI ALIYOICHUKUA HUKO MALAGASY? KWANZA DUNIANI WANASIKIA KISWAHILI??? HAKUNA HATA MMOJA ANAYEVUTIWA NA HUYO MAGUFULI WAKO.
 
Mhe. Rais Magufuli anatarajiwa kutuma salaam kwa Taifa leo Mei 17, 2020.

Hotuba yake inaaminika itajaa mambo mazito.

Kaa standby kwenye media zote na mitandao ya kijamii muda si mrefu ujao.

Inatarajiwa kuanzia mida ya saa sita na nusu mchana (12:30PM) ndipo atakuwa mubashara.

JF will cover it

======

View attachment 1452519

‪RAIS AMETOA SALAAM BAADA YA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KANISA LA KKKT USHARIKA WA CHATO‬

Raisi Magufuli akiwa katika kanisa la KKKT Chato amepata nafasi ya kuzungumza mbapo ameongea mambo mbalimbali,

Katika hotuba hiyo Raisi ameanza kwa kumshukuru Mungu na viongozi wa dini wote nchini. Raisi magufuli amesema “Waimbaji wameimba hapa kwamba bila mungu huwezi kuongoza, bila kumtanguliza mungu huwezi ukafanya chochote. Kwahiyo napenda niwashukuru Watanzania wote, Viongozi wa dini mbalimbali ambao wameshiriki kuliombea taifa hili"

"Na ndio maana siku za nyuma wakati ugonjwa huu umeingia niliwaomba ndugu zangu watanzania angalau tutumie siku tatu za kuomba kwelikweli. Ninawashukuru sana kwa sababu wote tuliomba tulifunga na Mungu amejibu na Mungu ametusikia”

“Ndugu zangu mifano mingi imetolewa, hata katika mahubili yako leo Baba Mchungaji katika injili na katika matendo ya mitume umeeleza ni namna gani watu walivyoweza kumtegemea Mungu walivyoweza kufanikiwa”

“Yule kipofu alimlilia yesu, Mwana wa Daudi nirehemu, Yesu ambaye ni mtoto wa Mungu ambaye naye pia ni Mungu alimponya. Wakati wa dhoruba kula baharini wanafunzi walivyokuwa wamelala wakaona mtumbwi unataka kuzama walipiga kelele” Katika maandiko pia sehemu zingine Yesu aliwakemea kwanza mitume kwa kuwa na Imani ndogo na baadaye akaikemea pepo na mambo yakawa shwari kwahiyo sisi katika kipindi chochote kigumu cha aina yoyote tukimtanguliza Mungu tutafanikiwa”

“Kwahiyo ninawashukuru sana ndugu zangu, ninawashukuru sana Wachungaji, Masheikh, Mapadri, Maaskofu kila mmoja katika eneo lake ambao tulimtanguliza Mungu na Mungu ametusaidia sana”.

“Ndugu zangu katika mapambano ya aina yoyote ni vita. Ugonjwa huu wa Corona hauna tofauti na vita nyingine. Nilikwisha eleza na wataalamu pia wameahaeleza ni namna gani nzuri ya kuweza kupambana na ugonjwa huu hata Baba Mchungaji umezieleza mbinu zote”.

“Ni kweli sikutoa amri ya lockdown ya kuwafungia watu majumbani, ulikuwa ni utumwa wa ajabu. Imagine wewe Lyabange ufungiwe saa nyingine hata usionane na Mme wako Iseme au na watoto wako. Sisi hapa huwa tunaondoka asubuhi kwenda kuchukua chakula, ukachume viazi, maharage yako, uende ziwani ukavue hivyo vyote vingekuwa vimezuiliwa tungekuwa tuko wapi sisi Watanzania miliono 60?"

Huruhusiwi kwenda sokoni, na saa nyingine unaruhusiwa kutoka kidogo tu, halafu usiku usitoke kana kwamba Corona inatembea usiku tu. Hebu tujiulize sisi Watanzania tuna miradi mingi tumeweka katika nchi yetu, Hiyo miradi yote ingekuwa imesimama.

"Tunajenga reli kwa mabilioni ya fedha, Makandarasi kutoka Nje wale wote tungewazuia vijana wasipate kazi tungekuwa wapi?"

"Tunajenga Mradi wa umeme, thamani yake ni Zaidi ya Trilioni saba zimechukuliwa na Watanzania kwenda kuinvest pale kusudi tuwe na umeme, leo wale wote tungekuwa tumewasimamisha, vijana wale wote tungekuwa tumewasimamisha; tunajenga barabara zote zingekuwa zimesimama."

"Hapo tunajenga meli kwenye ziwa Viktoria na juzi mmeona Injini zimekuja kutoka Korea, zote zile zingekuwa tumesimamisha na injini zisingekuja."


.
Jamaa anasema maiti za corona ziachwe zizikwe na ndugu na jamaa kama wanavozika wafu wengine kama wa ukimwi na TB
 
Watalii kutoka nchi gani??? Ni nchi IPI iliyonaakili timamu itaruhusu rain wake waje/warisk maisha Yao Tanzania.....Hivu unadhani hawajui kuwa Tz watu wanakufa kwa Corona na Data zinafichwa?????


Endeleeni kujitekenya
 
Corona ipo atuja kataa ila tusiifanye kuwakubwa kuliko Mola wetu ,alieumba Mbingu na ardhi na vilivyomo, kwahiyo ni lazima tufaham alimfiki mja jambo bila ya Mola kuridhia , kama wew ni wakufa na corona hata uchukue tahadhari vip ,utaondoka tu , kuna vitu lazima tuviweke sana ,
Kuna Corona ,ila tujue kuna Mola ambae hata mda huu akisema corona iondoke inaondoka mda huu huu!
Tuchukueni tahadhari ila tusimsahau Mola amini katka Mola wako Fanya ibada zako chukua tahadhari na Mola atakuvusha! Katika hili ,ila tusijisahau kabsa nakuona taratibu za wazungu ndio zipo sahihi sio Kweli , na ndio maana hata wakat wa Ebola madaktari wa virus waliita jamii usika na kujadiliana ,kuhusu jinsi ya kukabiliana na huo ugonjwa na jamii ilitoa njia zilizokua zinatumika za jadi na walifanikiwa ,
Kitu tunapaswa kuelewa ni kwamba hata karne za nyuma magonjwa yamilipuko yalikuepo na walitumia njia zao kwa wakt huo na wakafanikiwa na hakukua na lockdown, sio kwamba naipinga lockdown hapana ,ni lazima tujaribu njia tofauti maana sio kote iyo lockdown ilipo kuwa implemented imeleta Matokeo mema hapa ,kwengine imetumika na ugonjwa bado warindima, tujiulize tu kama huu ugonjwa tutakua nao kwa miaka kumi ijayo ,je tutakaa lockdown for ten years !? Kwa uchumi upi!? Hata hiyo Marekani aitahimili huo mshindo wake !
Kitu kiliitajika kufanywa ni watalaam wa magonjwa ya maambukizi barani Africa walipaswa kukaa na kuandaa mukthadha mzuri wa kupamba na huu ugonjwa na sio kukopi kutoka nchi za magharibi, ambayo pengine sio rafiki na jamii zetu,
Hata wew hapo jiulize tu kwa hazina uliyo nayo unao uwezo wa kukaa katka total lockdown kwa mda gani !? Na je hapo hapo ukawa na uwezo wa kuwasaidia nduguzo vijijin bila ya weye kuyumba ,!? Kiukweli hili suala linaitaj busara ya hali ya juu sana!si kwa viongozi wala wananchi wenyew, naangalia sisi ambao lazima tutoke ndio tueke mkate mezan! Je serikali itakua na uwezo wakugawa chakula kipind cha lockdown hadi iishe!?
Cha msingi ni kuchukua na kufanya kazi amna jinsi, hakika mauti yapo na kama uliandika utakufa kwa hili janga lazima ahad itimie, ila kama ni wakuishi ,utaish tu hata kijiji kizima kipate maambukizi utapona na kuishi,
Mola atufanyie wepesi katka kila kwenye uzito
Amin.
Angalia anavyowazuga watu anawaambia nyie kwani mmevaa barakoa. , anasema tumuachie mungu mean hata hizo barakoa haziamini, so watu wajiachie

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kimepangwa sijui.. Au ni muendelezo wa maigizo.

Dr. Kaleman leo akiwa Ofisi za TANESCO-GEITA alivaa Barakoa lakini ameenda Kanisani kavua na kuonesha hali ni shwari wale wote waliokuwa Kanisani leo itakuwa wameambiwa wasivae Barakoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“Mimi Mtoto wangu wa kumzaa amepata corona akajifungia, akajifukiza akapiga malimao, sasa hivi ni mzima kabisa anapiga push-up, msije mkadhani mimi sijapata Mtu wa karibu mwenye corona, tuondoe hofu”-JPM

“Kuna mambo ya hovyo yanafanyika, kila Mtu akifariki wanakimbilia kumpima corona, Mtu amefariki unampima yanini?, nguvu za kumpima wanazo, za kumuhudumia akapona hawana, Mtu atakapofariki kwa ugonjwa wowote hata wa corona lazima azikwe kwa kawaida, corona sio Ebola” -JPM

“Kuna rafiki yangu mmoja Injinia alipata kiharusi akapelekwa Muhimbili, wakampima wakasema ana corona, amepelekwa Amana Watu wanamuogopa kisa ana corona, Ndugu zake wakamtoa wakampeleka Agha Khan, wamechukua vipimo wakakuta mzima hana corona, amepona yupo nyumbani” -JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo raisi hahusiki na utoaji wa huduma za uhakika, hao anaowatuhumu si ni waajiriwa wake??
Tukisema hudama za afya zitolewazo na HSP za serikali zimefubaa/ dhaifu tutakuwa sahihi
 
Nimemsikia Rais akisema kuwa mwanae ilipata Corona hii inaweza kuwa sababu aliamua ajitenge ili kuepuka maambukizi ya Corona, kwa maoni yangu Rais alifanya jambo jema kama Kiongozi wa kitaifa na kuamua kufanya kazi kutoka Kijijini kwake Chato

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama mtoto wa rais kapata corona na yule jamaa kigogo2014, hakujua basi kumbe ni
Mweupe sana .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom