Wakuu naomba kujua jambo moja, Rais magufuli ameruhusu wanafunzi wa Vyuo Vikuu kurejea vyuoni na kuendelea na masomo yao, je kwa wale wanafunzi wa vyuo vikuu walioko huko Nyumbani Tanzania lakini wanasoma huku ng'ambo ambako nchi nyingi hawajaruhusu wanafunzi kurejea vyuoni watafanyaje,
mfano wanafunzi wanaosoma nchini Kenya, Uganda, Rwanda ambako hawajaruhusu watu wao kuendelea na mambo na bado wamefungiwa, watafanyaje waendelee na masomo yao kama hao wa huko tz?