Kiukwel ofisi za NIDA huduma zinaonekana zipo chini Kuna shida ambazo zinapelekea kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa namba +vitambulisho venyewe
1)Watumishi ni wachache, idadi ya watumishi ni wachache ukilinganisha na huduma zinazotolewa lwa wananchi watumishi waliopp wanalemewa na mzigo wa watu, wakati uncle anaingia madarakani aliwaondoka wafanyakazi takribani 500 waliokuwa wanafanya kazi kwa mikataba, hii kidgo ilikuwa inasaidia kupunguza mzigo wa kazi, sasa hv, ofisi za nida ukienda wafanyakazi hawazidi watano waliowwekwa permanent tena hao watano bahati na kama sipo wrong ni mkoa wa kagera nenda Morogoro pale tubuyu, ofisi ya nida ghorofa za kutosha lakini ulizia watumishi wa kufldumu wapo wangapi utaambiwa hata watano hawafiki.
2) Sehemu ya uchakataji, sehemu ambapo wanazalisha vitambulisho IPO moja pale kibaha, just imagine (tengeneza picha kichwani kwako) Tanzania nzima uchakataji/utengenezaji wa vitambulisho unafanyikia sehemu moja, watanzania tupo wangapi ?
Hapa ningeonelea kama wangekuwa na kanda/zones za kutengeneza vitambulisho kwa mfano kanda ya kati wawepo Dodoma wanazalisha vitambulisho, kanda ya kasakzn wawepo Arusha wanazalisha vitambulisho na kadhalika kusini wawepo mbeya wanazalisha vitambulisho ili kupunguza overrides ya kazi ya kuzalisha hizo I'd.
Nawasilisha