Rais Magufuli: Huduma za NIDA ziwe kila Wilaya au NIDA watoe hela ya 'guest' kwa Wananchi. Ukiona bei ya mahindi iko juu, kalime yako

Okk
Sasa kwa uzoefu kidogo uliyonao kwanini vitambulisho vina kuwa shida kutolewa

Ova
Mkuu sababu zipo nyingi
Hatuwezi kuzitaja humu but naimani wahusika Ni wajuzi zaidi na tunachoomba Ni sisi kuongeza nguvu ktk Hilo zoezi
Mfano mwanzo zoezi lilikua Ni dar tu
Sasa mh Raisi anasema Ni nchi nzima
So nguvu kazi lazima iongezeke
 
Hivi serikali ilshawahi kupanga bei ya mahindi?
Sheria ya food security ndio mchawi wa bei ya mazao ya vyakula. Pia tukumbuke kuwa kinachofanya bei ipande ni kuruhusu kuuza nje ya nchi. Serikali ikifunga uuzaji nje lazima bei ishue. Je kwa muktadha huo utasema serikali imepanga bei?
 
Lakini kwa sasa wanaolalamikia bei kupanda sio wasiolima pekee,kuna hats wakulima waliouza mazao yao mapema ili kukidhi shida kadhaa.

Sasa kuna Neema,ingawa naona sio kwa mtindo mwafaka.
 
Mkuu tumshauri aongeze nguvu kazi
Maana ofisi za nida kila wilaya zinaupungufu wa rasilimali watu
 
Tanzania ndio serikali pekee duniani isiyojulikana inatumia mfumo gani wa kuendesha uchumi wake sio capitalist au socialism! lazma tutengeneze mfumo wetu wa uchumi tutakao utumia sio kuingilia soko mfano kwenye umeme, maji, mafuta!.
 
Sasa kwani Serikali inafunga Soko la nje la mazao ?
Hali ya kuwa wakulima sio tu wanashindwa kuuza mazao yao bali pia vijana wanaacha kulima na kukimbilia mjini.
Mimi ni Kati ya Vijana niliyeamua kuja kutafuta fulsa mjini baada ya Mazao yangu kukosa soko na kuoza na kupelekea kuzitelekeza shughuri za Kilimo.
 
Nida wawezeshwe idadi staff,fungu na vitendea kazi. Hata wakiweka ada ndogo 5000 itasaidia.
Kwa sasa huduma ni bure ila wananchi walipa garama kubwa wanatumia pesa nyingi nauli, muda, chakula, ndoa mtihani nk.
Jambo la kujiuliza: Hao viongozi wa juu waliwasilisha matatizo na mapendekezo yao kwa ngazi za juu? Rais anavyozungumza hapa inaonekana kama ngazi za juu hawana taarifa na changamoto zinazowakabili NIDA. Ndiyo maana siku zote huwa rais anasema tusifanye kazi kwa mazoea kama ilivyokuwa zamani. Kiongozi ukipewa eneo fulani kuongoza ukiona kuna changamoto jaribu kuziwasilisjha kwa ngazi husikan asiyo kukaa tu.
 
Kilichosababisha ukose soko ni nini? Na ulipokuwa unalima ulitarget soko gani?
 
Mkuu wala tatizo sio kuuza nje ya nchi kwa wananchi, hayo mahindi!! Msimu wa mwaka jana sehemu kubwa ya nchi haikupata mvua za kutosha, hivyo kupelekea mavuno kupungua, mfano kanda ya ziwa toka mwezi wa sita, katavi na rukwa ndio kimbilio lao kwenye mahindi na mchele!! Kingine ni NFRA, kuacha majukumu yake ya kununua na kuhifadhi mahindi, inapofikia kipindi kama hiki wanayauza kwa bei nafuu ku stabilize bei!!! Sasa wao wamenunua tani kidogo, hapo hapo tena wakaingia kwenye biashara WFP, na kuwauzia ZIMBABWE!! leo unasikia kauli za kibabe kibabe tu!! Na hata sasa anayefaidika sio mkulima, ni mfanya biashara, mkulima alishayauza wakati yako bei chini ili kukizi matatizo yake!!! Fuatilia awamu zilizopita kwenye maghara ya NFRA, yalikuwa yananunua tani ngapi uje ulinganishe na awamu hii!!!
 
Hivi kwa wanaoijua korosho vizuri mtujuze hili zao LA shamba au kiwandani.Mi nilidhani ni zao LA shambani nikataka kujiuliza Inamaana anajipinga operation yake ya korosho?
 
Suala la kutengeneza vitambulisho sehemu moja siyo tatizo kama wanafanya kazi inavyotakiwa. Tena ndiyo vizuri kwa sababu za kiusalama. Kinachotakiwa ni kuwa na mashine na wafanyakazi wa kutosha. Kazi inaweza kufanyika masaa 24 na kwa siku saba kwa kutumia shift. Kuwa na sehemu tofauti tofauti za kutengeneza ni very risky na gharama.
 
Umeeleza vema!
 
Mbona korosho anapanga bei?
 
Safi sana, ngoja tukalime mahindi kwa wingi.Tatizo la watu wa mjini hawataki sisi wakulima tunufaike kabisa mahindi yakipanda kidogo tu kelele nyingi.
 
Kilichosababisha ukose soko ni nini? Na ulipokuwa unalima ulitarget soko gani?

Unaonekana ww ni wale wasomi uchwara mnaokaa mjini, mkulima wa kawaida analima zao analolimudu kulingana na mazingira yake. Matarajio yake ni kuuza ziada ya mazao yake. Huo muda wa kutsget soko gani ni kwa mtaji gani alio nao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…