Rais Magufuli huhitaji kujieleza unapomtoa Waziri. Kwa January Makamba jikalie kimya

January katolewa kwa uhaini brother. Kuna vitu siyo vya kuongea every where. Just know hata wewe uliposaliti Chadema walikutoa pamoja na mazuri yote. Kumbuka tu msaliti ni zaidi ya mchawi.

Januari ni msaliti
Rais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.

Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.

Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.

Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.

Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?

Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.

Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa

Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini
 
Sijamsikia popote Rais Magufuli akitaja sababu za kumtumbua January. Ni kama vile unamlisha maneno!
Mbona kasema waziwazi, kwamba Makamba alishindwa kusimamia swala la mifuko mpk yy rais alivyoingilia kati. Na kaenda mbele zaidi kwa kumtaka aliyempa hii nafasi asifanye kama January achape kazi.
 
January katolewa kwa uhaini brother. Kuna vitu siyo vya kuongea every where. Just know hata wewe uliposaliti Chadema walikutoa pamoja na mazuri yote. Kumbuka tu msaliti ni zaidi ya mchawi.

Januari ni msaliti
Uhaini!!!
Kijana taratibu,fafanua uhaini according na constitution yetu
 
January ametenguliwa ili kumkomoa mzee makamba baba yake, kwasababu ya voice iliyasambaa, wala sababu siyo mifuko, kama ilikuwa mifuko angemtengua toka zamani tunavyomfahamu magufuli huwa hacheleweshi.
 
Ulikuwa husikilizi au hukuelewa.

Kasema kwenye wizara yake kulikua na miradi hewa ya kupanda mikoko, matumizi mabaya ya fedha za wafadhili, na marufuku ya mifuko ya plastiki aliichelewesha kwa miaka 4 na hata lilipotekelezwa juzi ni yeye alimlazimisha.

Sijui kama ni kweli au ni kumpaka matope jamaa, Makamba nae katia ngumu, kagoma kwenda Ikulu leo kama watumbuliwa wengine wanavyohudhuria
Mkuu hao wamezoea "kuambiwa" hivyo hawawezi kuona wasichoambiwa!!!
 
we zitto mbona kimbelembele kama ni kipenzi chako si umchukue sasa hivi umekuwa mtu wa kulalamikia kila jambo linalofanywa na chama tawala badala ya wewe kuonyesha mawazo mbadala huo ni ufilisi wa akili
 
Magufuli anataka kusema ucheleweshwaji wa azimio la kupiga marufuku mifuko ya plastic kwa more than 4 years ni kosa la January Makamba peke yake? Hizi lawama za kindezi sana. Yeye kama Rais alifanyaje kusort out the mess?
Alikuwa anamcheki tu halafu anasema hiiiiii
 
siku moja weekend nilikua na wageni wakiwepo wazazi wangu na vijana wangu wawili nikajitusu kwenda kukodi CD nikaipenda ya VAN'DAMEZ nikiwa najiamini kabisa nikampa kijana mmoja akaiweke kwenye kwenye deki na huku nikimuagiza alete na remote ya deki hahaha ile imeanza tu hata remote haijanifikia alaula! dah! kumbe ni PORN aisee sikua na namna zaidi ya kuisukuma TV idondoke
Bangi za kuvuta bila malengo 😂 😵😵
 
Rais Magufuli kwenye sababu za kumuondoa January Makamba bora jikalie zako kimya.

Nimekusikia Rais leo ukijaribu kuelezea sababu za kumuondoa Uwaziri Bwana January Makamba. Kwa kweli hukuwa umejiandaa na maelezo ya kuridhisha.

Rais, kwenye suala la mifuko ya plastiki tunajua ukweli kwamba wewe ndiye ulizuia lisiendelee ulipoambiwa kwamba litaua viwanda. Tunajua kwamba January ndiye ametumia miaka mitatu kuwaandaa wenye viwanda vya mifuko ili wabadilishe teknolojia na wasipate hasara. Tunajua kwamba January alifanya vikao vya umma (public hearings) kuanzia Karimjee mwaka 2017 hadi Mwanza mwaka 2018 na kwingineko kushirikisha wananchi kwenye jambo hili. Tunajua kwamba hatukusikia kauli yako kwenye mifuko ya plastiki hadi baada ya suala hili kufanikiwa. Hii sio kawaida yako maana wewe ni very predictable.

Tunajua kwamba mlimtegea Makamba ili afeli halafu mumtimue. Hakufeli. Sasa mnamtimua kwa kukamilisha kazi kwa weledi mkubwa! Mhe Rais wewe ni mkali maelekezo yako yasipotekelezwa. Umemuachaje Waziri miaka minne kwa kutotii maelekezo halafu unamtoa baada ya utekelezaji? Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kukubali hoja yako hii dhaifu sana.

Bwana Rais ulikutana na wafanyabiashara kote nchini kutwa nzima. Walitaja kero zao zote, nami nikaziorodhesha. Sikusikia hata mmoja akilalamikia NEMC. Kwasababu gani? Kwasababu January ameibadilisha NEMC. Alitaka kuibadilisha huko nyuma na akavunja bodi na kuondoa menejimenti lakini kwakuwa inasemekana kulikuwa na ndugu zako walioguswa ukaagiza uamuzi ule ubatilishwe. Unadhani Watanzania wamesahau?

Bwana Rais fedha zinazotolewa na wahisani kwenye miradi ya mazingira zinakaguliwa na CAG na hakuna popote palipoonyesha ubadhirifu au upotevu. Kama upo uweke hadharani kama sisi tulivyoweka hadharani ubadhirifu wa TZS 1.5 Trilioni. Wacha wahisani, Serikali yako haijaweka hata senti tano kwenye miradi ya mazingira nchini. Mimi ni Mbunge na ninapitia kila Bajeti ya Serikali na Taarifa za CAG. Hujawahi kutenga fedha za Mazingira. Kwa kifupi, tunajua wewe binafsi sio mpenzi wa mazingira na umesema hivyo mara kadhaa. Hata huyo January mwenyewe “ulimtupa” kwenye mazingira ili apotee lakini ghafla kila Mtanzania leo anaongea mazingira. Hata wewe nawe leo unayaongea.

Bwana Rais hulazimiki kutoa sababu unapomuondoa Waziri. Kwa kutafuta kutoa sababu zisizoshiba leo, umeonyesha kwamba umesikia hisia za Watanzania kuhusu kuondolewa January Makamba. Umeondoa Waziri kipenzi cha Watanzania na Waziri weledi. Tunajua umemfukuza kwasababu nyingine, sio uchapakazi. Watanzania wote tunajua kwamba siku zote alikuwa anatafutiwa sababu tu ya kuondolewa. Ukisema uchapakazi ndio sababu Watanzania tunakushangaa kwasababu hawa mawaziri umewateua wewe lakini tathmini tunafanya sisi Watanzania. Na January Makamba ndiye alikuwa Waziri mbunifu na bora kabisa. Na ataendelea kuwa maarufu miongoni mwa Watanzania. Hakika ana nafasi kwenye uongozi siku sio nyingi sana zijazo. Mabadiliko ni lazima na January naamini atakuwa sehemu ya mabadiliko ili kujenga Tanzania inayojali watu wake na yenye Demokrasia iliyokomaa

Zitto ZR Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini
Akili kubwaaaaa
 
January katolewa kwa uhaini brother. Kuna vitu siyo vya kuongea every where. Just know hata wewe uliposaliti Chadema walikutoa pamoja na mazuri yote. Kumbuka tu msaliti ni zaidi ya mchawi.

Januari ni msaliti

Usaliti!? Uhaini!?
 
Vijana mtanipinga sana ila nawaambia ni rahisi sana kua maarufu kwa harakati za maneno ya kukosoa siasa au serikali za Africa sababu matatizo ni mengi.....ila ngumu sana kua maarufu kwa namna za kina Ruge,Mengi, Mo, bakhresa, Kusaga...na Hawa ndio hubadili maisha ya vijana wengi.

Nasimama na Dr John
 
Makamba yupo vizuri hao jamaa wa NEMC walikua kikwazo sana kwenye viwanda na faini za hovyo hovyo na mambo mengi ya ajabu ajabu sema ndio hivyo kufanya kazi na watu wasiotaka maendeleo wanataka siasa hawawezi kukuelewa kabisa...kama Makamba hafai hakuna anaefaa huko
 
Back
Top Bottom