Unakubali kwamba TZ iko kwenye uchumi wa kati kufuatana na GNI. Unaendelea kusema kwamba dira ya Taifa ni kwamba ifikapo mwaka 2025 GNI iwe USD 3,000. Kitu nisichokielewa ni hiyo sentensi yako ya mwisho inayotuomba tuache propaganda kuwa tumefikia uchumi wa kati kabla ya lengo. Wewe mwenyewe umekiri tumefikia uchumi wa kati mwaka 2020. Kuna propaganda gani hapo? Kuhusu wastani wa pato uliopangwa ufikie USD 3,000 ifikapo 2025, bado tuna miaka mitano ndiyo useme kama tumefikia lengo au la.
Kufuatana na vipimo vya World Bank vya Julai 2019, ambavyo nimeviangalia kwenye Google dakika chache zilizopita, nchi inawekwa kwenye makundi yafuatayo:
Mpaka USD 1,025: Low Income
USD 1,026-3,995: Lower Middle Income
USD 3,996-12,375: Upper Middle Income
Zaidi ya USD 12,375: High Income
Hitimisho. Tumeingia uchumi wa kati kabla ya tarehe iliyopangwa. Hakuna propaganda hapo. Kitu ambacho hatuwezi kukitathmini kwa sasa ni kuwa kwenye uchumi wa kati wa wastani wa USD 3,000. Hilo tutafanya baada ya miaka mitano. Kulingana na kasi iliyoonyeshwa katika miaka mitano inayokwisha sasa, sina shaka hilo litafanikiwa, kama tukiupa utawala wa Magufuli miaka mingine mitano mwezi ujao.