Rais Magufuli jinsi Mamlaka ya Maji ya Mwanza (MWAUWASA) unavyokuhujumu usipate kura zetu

Rais Magufuli jinsi Mamlaka ya Maji ya Mwanza (MWAUWASA) unavyokuhujumu usipate kura zetu

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Kwa siku za karibuni tangu uanze kampeni zako Mamlaka ya Mji wa Mwanza (Mwauwasa) umekuwa na huduma mbaya kwa wateja wengi wa maji katika jiji hili.

Tangu Injinia Sanga atoke kwenye Mamlaka hii na kupewa wadhifa mwingine huduma zimekuwa mbaya sana.

Nitoe mfano hai, tangu ijumaa mpaka leo maeneo ya Mwananchi, Mahina hatuna maji kabisa ukichukulia kuwa kesho kutwa ni siku ya uchaguzi.

Ni mwananchi gani atakwenda kupiga kura badala ya kwenda kutafuta maji kwa ajili ya familia yake.

Tunakuomba utakaporudi madarakani uanze na kufumua uongozi wa Mamlaka hii ili wananchi wapate huduma inayoridhisha.
 
Mhina amekutuma uje upige porojo hapa.
 
Magufuli hana chochote katawala kwa ulaghai tu kwa miaka mitano

Hatumpi mitano tena
 
Hapo ni kama km 5 kutoka ziwani mnapata maji kwa shida ..hii njiaa ina mambo mengi ya hovyo
Sasa mkuu mimi ni mwenyeji wa mwanza na nimezunguka baadhi ya mikoa Tanzania hii sijaona mkoa wenye tatizo la maji kama mwanza kama kuna anayebisha aseme kuwa mkoa fulani unashida ya maji kuliko mwanza.
Wa kazi wa Buhongwa karibu na lilipo ziwa Wana wiki hawana maji.
 
Na cha ajabu mikoa inayopata huduma ya maji kutoka mwanza kama Shinyanga, kahama mpaka Nzega tatizo la maji kwao limekuwa historia ila sasa njoo mwanza kama huna tangi la maji hutaoga wiki
 
Sasa mkuu mimi ni mwenyeji wa mwanza na nimezunguka baadhi ya mikoa Tanzania hii sijaona mkoa wenye tatizo la maji kama mwanza kama kuna anayebisha aseme kuwa mkoa fulani unashida ya maji kuliko mwanza.
Wa kazi wa Buhongwa karibu na lilipo ziwa Wana wiki hawana maji.

Buhongwa kipindi fulani mna subiri maji hadi usiku wengine wakilala wafunge na koki zao ndio yatoke.. wanasiasa wanaishia kujimwamba faii tuu
 
Buhongwa kipindi fulani mna subiri maji hadi usiku wengine wakilala wafunge na koki zao ndio yatoke.. wanasiasa wanaishia kujimwamba faii tuu
Hili tatizo la maji Mwanza ni tatizo la muda mrefu na wanasiasa hapa ni wachumia tumbo tu.
 
Back
Top Bottom