Rais Magufuli kamaliza kabisa mahakama na vyombo vya usalama

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Serikali bila kujua imeharibu kabisa imani ya wananchi kwa mahakama na vyombo vya usalama. Sababu kubwa iliyosababisha ni kuingiza siasa kwenye hivi vyombo muhimu.

Kwanza kwenye mahakama JK amechagua majaji ambao hawakuwa mahakimu na wengi kuona hakuna umuhimu kuwa hakimu kama majaji wanachaguliwa kisiasa na sio kutokana na rekodi.

Jaji mkuu mfano kuna kesi ngapi alisikiliza kabla ya kuwa Jaji Mkuu. Hivyo utamaduni wa zamani ni kama umetenguliwa majeshi vilevile yote wamechanganyikiwa. Mfano kumtoa kiongozi kutoka jeshini kwenda kuwa Mkuu wa Magereza bila uzoefu wowote ni uamuzi wa kisiasa badala ya kiidara.

Sasa wale polisi au magereza ambao kwa muda walifikiri watakuja kuwa juu hawana uhakika, yaani DCI unapelekwa kuwa Mkurugenzi wa Mkoa, wapi na wapi! wakati mpaka kuwa DCI si chini ya miaka 20 ndani ya jeshi la polisi.

Vilevile hii pigapiga ya upinzani inawasaidia upinzani, inawaharibia serikali na vyombo vyote. Lakini wananchi wanajenga fikra kwamba upinzani ndiyo majasiri hasa wanawake. Kijana anaona wanawake viongozi wanapigwa na polisi halafu kesho unamwambia hao wapigaji awaheshimu. Kwenye mahakama kesi zinachukuwa miaka mingi na gharama kubwa bila sababu halafu uamuzi unakuwa wa kisiasa.

Magufuli anafikiri na wenzake wanajenga vyombo vya usalama lakini iko siku watagundua wameharibu sana. Rafiki yangu mwanajeshi aliniambia wanajeshi walichukia sana kupelekwa kwenye mashamba ya mkorosho kule kusini.
 
Watu wamefanya kazi muda mrefu kwenye halmashauri, na wamejiendeleza kielimu ili siku moja wapande ngazi wanashangaa wanaletewa DED mpya aliteuliwa kwa misingi ya ukereketwa wa chama, unafikiri watu watakuwa na moyo wa kufanya kazi
 
Halafu alichotufanyia wananchi hata atukioni, ananunua tu wabunge wetu badala ya kutuletea dawa hospitalini.
 
Huyu jamaa anajiona ana akili sana,alishasema hashauriki!
 
Kamundu, umetupa somo kubwa sana sisi wasomaji na wanJF. Hakika JamiiForums ndipo unaweza kupata uchambuzi wa kina kupita vyombo vingine vya habari ambavyo wao wa kusikiliza na kuripoti bila uchambuzi.
 
Serikali bila kujua imeharibu kabisa imani ya wananchi kwa mahakama na vyombo vya usalama. Sababu kubwa iliyosababisha ni kuingiza siasa kwenye hivi vyombo muhimu.

Kwanza kwenye mahakama JK amechagua majaji ambao hawakuwa mahakimu na wengi kuona hakuna umuhimu kuwa hakimu kama majaji wanachaguliwa kisiasa na sio kutokana na rekodi.

Jaji mkuu mfano kuna kesi ngapi alisikiliza kabla ya kuwa Jaji Mkuu. Hivyo utamaduni wa zamani ni kama umetenguliwa majeshi vilevile yote wamechanganyikiwa. Mfano kumtoa kiongozi kutoka jeshini kwenda kuwa Mkuu wa Magereza bila uzoefu wowote ni uamuzi wa kisiasa badala ya kiidara.

Sasa wale polisi au magereza ambao kwa muda walifikiri watakuja kuwa juu hawana uhakika, yaani DCI unapelekwa kuwa Mkurugenzi wa Mkoa, wapi na wapi! wakati mpaka kuwa DCI si chini ya miaka 20 ndani ya jeshi la polisi.

Vilevile hii pigapiga ya upinzani inawasaidia upinzani, inawaharibia serikali na vyombo vyote. Lakini wananchi wanajenga fikra kwamba upinzani ndiyo majasiri hasa wanawake. Kijana anaona wanawake viongozi wanapigwa na polisi halafu kesho unamwambia hao wapigaji awaheshimu. Kwenye mahakama kesi zinachukuwa miaka mingi na gharama kubwa bila sababu halafu uamuzi unakuwa wa kisiasa.

Magufuli anafikiri na wenzake wanajenga vyombo vya usalama lakini iko siku watagundua wameharibu sana. Rafiki yangu mwanajeshi aliniambia wanajeshi walichukia sana kupelekwa kwenye mashamba ya mkorosho kule kusini.
Hiyo ya kupelekwa kwenye korosho, wanajeshi wengi walichukia, tena makamanda wa vyeo vya juu.

Kuna askari wengine hawajawahi kuiona korosho ikiwa kwenye mti wake au hata hajawahi kuiona ikivubwa, kulala na kuamka unaambiwa, nunua korosho, na ubangue!!
 
Back
Top Bottom