Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,207
Salaam Wandugu,
Kwa taarifa nilizozipata,Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anategemea kufanya ziara Mkoani Kilimanjaro hasa Wilaya ya Siha kuanzia tar 1-9-2016.
Taarifa hizo zinadai atafanya mkutano wa hadhara katika mtaa wa Mji mwema,kijiji cha Roseline, kata ya Ndumeti tarafa ya Siha Magharibi. Na moja ya ajenda itakua ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami kutoka Sanya-Juu kupitia Ngarenairobi mpaka Elerai kuelekea huko Kamwanga.
Je,ziara hii ya Rais itakuwa dawa tosha ya matatizo yanayowasibu Wananchi wa maeneo hayo? Je,wawekezaji wasio na tija katika taifa ukiwepo wa Endarakwai unaweza kutumbuliwa?
Je Mgogoro waArdhi usiokwisha baina ya wafugaji jamii ya Kimaasai na mwekezeji Peter Jones utatolewa ufumbuzi?
Je,ufisadi wa milion 250 zilizoripotiwa kufanywa na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Ndg Rashid Kitambulio na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la madiwani Mh. Nassari utazungumziwa?
Je,ukodishwaji wa eneo kubwa ardhi kwa matajiri huku wananchi wakilalama wasipate hata pa kukodisha unaweza kupatiwa ufumbuzi?
Yote hayo na mengine mengi tutajua pale atakapowasili Mkuu wetu wa Kaya.
Tusubiri na tutaona.
Msiha.