Tetesi: Rais Magufuli kufuta ubunge viti maalum, ni kwa kurejesha mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba

Tetesi: Rais Magufuli kufuta ubunge viti maalum, ni kwa kurejesha mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba

Akiileta Katiba Pendwa Ya Tume Tutamsamehe Mapungufu Yake Yote Aliyoonyesha Huko Nyuma
 
Hahahahahaaaaaa! Unatafuta ugomvi na viti maalum wewe. Bunge halitakalika

..mtoa mada amelenga kupotosha.

..kama sijakosea tume ya warioba ilipendekeza kila jimbo liwe na mbunge mwanaume na mbunge mwanamke.

..nadhani ingekuwa na maana zaidi kama viti maalum vingewekewa ukomo kwamba mhusika asigombee zaidi ya vipindi viwili.

..unajua kuna wanawake wa shoka wamekomaa kwenye chaguzi tatu mpaka wameshinda. Kuna mama kaboyoka wa cdm amepambana chaguzi 3 amekuja kushinda mwaka jana. Wanawake wanapaswa kujiamini.
 
CCM hawataki kusikia ile katiba ya Warioba sijui kwanini
Kwasababu hawapendi kuona MAZURI yakifanyika,wao wanafaidika kwa kufanya MABAYA.Na UKWELI ni sumu kali sana kwao,ukiwa mzuri lazima utakua ADUI yao tu.Mzee wa watu Warioba alikua na nia nzuri sana kwa FAIDA ya kila Mtanzania matokeo yake wakawatuma vijana wao wampige yule mzee, ni laana hi bro....
 
Wabunge wa viti maalum wanawekwa kwa makusudi maalum. Wanachokifanya bungeni ni kwa maelekezo maalum ambayo yana manufaa kwa serikali oliyopo madarakani. Wakati mwingine wanawekwa ili kuibua hoja ambayo inalenga kuweka mambo sawa katika uongozi wa juu. Mnasema ni mzigo kwani wanafika 50 humo bungeni? Mimi nashauri waendelee kuwepo ili wamsaidie rais utendaji kazi. Wapo pale kwa manufaa ya rais. Hii ni kwa mtazamo wangu tu ninavyohisi.

Mshua
 
japokuwa wabunge wengi wa viti maalum ni uwezo wao ni mdogo na wanachangia kwa emotions zaidi kuliko reason, siungi mkono kufutwa kwao, labda wangepunguza idadi sio kufuta, na madiwani pia......Wanawake wasshirikishwe kwenye siasa wakuu wana mchango mkubwa sana kwa jamii
Wagombee ndio 50/50 hiyo wanayodai. Muda wa affirmative umekwisha
 
Katika Bunge la Katiba CCM waliyapinga haya kwa hali na mali ,msituchezee akili tunajua haiwezekani ...

Hata hivyo hii habari itasalia kuwa tetesi
 
Ikiwa ni kuondokana na gharama zisizo za msingi, serikali ya Magufuli inasemekana iko tayari kuanza mchakato wa katiba mpya kwa kuanza kuleta upya mapendekezo ya tume ya jaji Warioba yaliyotupiliwa mbali awali. Ambapo pamoja na mambo mengine ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima wabunge wa viti maalum hawatakuwepo, kama ilivyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba..

"Wabunge hawa wa viti maalum hawana kazi wanayofanya zaidi ya kuliingizia taifa hasara" Dr. Bana alipoulizwa kuhusu mapendekezo ya Warioba kurudiwa upya

Pamoja na hilo, Rais pia kadhamiria kurudisha miiko ya uongozi kama moja ya njia ya kurudisha nchi katika misingi ya uwajibikaji na uzalendo....

Mytake: Rais Magufuli kama unataka ubaki katika historia ya nchi hii, basi tunaomba utuletee upya mapendekezo ya Jaji Warioba...
yahani una mahanisha anakubali kui-attenuate ccm???.................
 
japokuwa wabunge wengi wa viti maalum ni uwezo wao ni mdogo na wanachangia kwa emotions zaidi kuliko reason, siungi mkono kufutwa kwao, labda wangepunguza idadi sio kufuta, na madiwani pia......Wanawake wasshirikishwe kwenye siasa wakuu wana mchango mkubwa sana kwa jamii
Viti maalumu...vifutiliwe mbali ili kupeana..kwa offer za Ngongo kufe..na u baby baby uishe!
 
Mh. Rais nitakusifu sn iwapo utarudisha ile rasimu ya katba ya jaji Walioba, iliyotokana na maoni ya wananchi .sio ile ya wapga dili ya kile chama kikongwe kilichokosa mwelekeo, kilichotufanya hadi leo tunaishi maisha ya taabu
 
ikifika pahala mtu anakosa hoja na kumfanya mtu kuwa ndo hoja yake ujue taifa lina shida kubwa,wewe ni shida moja wapo katika taifa....................
Acha hoja muhimu ya Jessica ikamilike kwanza
 
Kati ya RAS, RC, DC na MD wawili hapo nao ni mizigo, wawili tu wanaweza kufanya kazi ya hao wote wanne
Futa hao waliopo kisiasa RC na DC, acha wabaki watendaji tu RAS, DAS na MD ndio watendaji......hiyo mizigo miwili tupa kule
 
japokuwa wabunge wengi wa viti maalum ni uwezo wao ni mdogo na wanachangia kwa emotions zaidi kuliko reason, siungi mkono kufutwa kwao, labda wangepunguza idadi sio kufuta, na madiwani pia......Wanawake wasshirikishwe kwenye siasa wakuu wana mchango mkubwa sana kwa jamii
Kama Halima Mdee kwa mfano alishinda na kumshinda mwanamume unadhani kwa nini waendelee kupewa dezo. Wapiganie hizo nafasi. Wavifute tu. Zibakie nafasi za uteuzi za Rais nayo iseme wazi ni kwa ajili ya mawaziri sio wabunge. Na wawe vetted na Bunge
 
Back
Top Bottom