Tetesi: Rais Magufuli kufuta ubunge viti maalum, ni kwa kurejesha mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba

Tetesi: Rais Magufuli kufuta ubunge viti maalum, ni kwa kurejesha mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba

japokuwa wabunge wengi wa viti maalum ni uwezo wao ni mdogo na wanachangia kwa emotions zaidi kuliko reason, siungi mkono kufutwa kwao, labda wangepunguza idadi sio kufuta, na madiwani pia......Wanawake wasshirikishwe kwenye siasa wakuu wana mchango mkubwa sana kwa jamii
Vifutwe vyote,sioni faida yoyote ya hivyo viumbe zaidi ya kulinda maslahi ya waliowapa ULAJI.Kwenye uchaguzi kuwepo na nafasi mbili me na ke afu waingizwe kwenye kinyanganyiro...Full stop
 
Ccm hawataki kusikia ile katiba ya Warioba sijui kwanini
Inasikitisha Sana nipoona michango Kama huu wa kwako, watu wate waliochangia wamechangia bila kuonyesha uvyama, Kama kweli tunapongeza nia njema na tunakosoa kwa nia njema, basi muda Mwingine tuache vyama pembeni. Hii mada mzuri ila nia yako uiaribu, kila mtu ataelekea upande wake hapa, kwani mnapewa nini hivi vyama vyenu. Mpaka mnapumbazika kabisa unaweza mkuta mtu njiani, ukimwangalia tu unaona kabisa shida zimemkaba, lakini anakiwaza chama kuliko watoto wake.
 
ikifika pahala mtu anakosa hoja na kumfanya mtu kuwa ndo hoja yake ujue taifa lina shida kubwa,wewe ni shida moja wapo katika taifa....................
USICHOJUA WEWE NI KWAMBA KUMUONGELEA JESSICA NI KUWAONGELEA WATOTO WA MASIKINI WALIOITWA VILAZA NA HUKU WATOTO WA MATAJIRI WAKITUMIA HUOHUO UKILAZA KUSOMA VYUO VIKUU, TENA SIO DIPLOMA KAMA HAWA WA MASIKINI BALI NI DEGREE YENYEWE
 
Hiyo ni tetesi tu ambayo imeletwa na mtoa mada,halijadhibitishwa na hata kama likipita si kwa kipindi hiki ila itakuwa ni kwa mwaka 2020.

Mkuu..
Hili Litetesi alielileta nae Ni Ki.Va.Vi..
Sina imani nayo japo kama mamlaka Watatatoa tamko Rasmi nitaunga mkono asilimia 200%

Hivi viti ni Mizigoo kwenye Taifa..
 
Ikiwa ni kuondokana na gharama zisizo za msingi, serikali ya Magufuli inasemekana iko tayari kuanza mchakato wa katiba mpya kwa kuanza kuleta upya mapendekezo ya tume ya jaji Warioba yaliyotupiliwa mbali awali. Ambapo pamoja na mambo mengine ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima wabunge wa viti maalum hawatakuwepo, kama ilivyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba..

"Wabunge hawa wa viti maalum hawana kazi wanayofanya zaidi ya kuliingizia taifa hasara" Dr. Bana alipoulizwa kuhusu mapendekezo ya Warioba kurudiwa upya

Pamoja na hilo, Rais pia kadhamiria kurudisha miiko ya uongozi kama moja ya njia ya kurudisha nchi katika misingi ya uwajibikaji na uzalendo....

Mytake: Rais Magufuli kama unataka ubaki katika historia ya nchi hii, basi tunaomba utuletee upya mapendekezo ya Jaji Warioba...
Viti maalumu vifutwe kabisa hakuna umaana wowote. maana kwasasa wanasema wanaweza wacha nao wapambane sio kugeuka kua wakubebwa kma kweli wanaweza basi wasisubiri kubebwa kwa viti maalumu ni kupambana kma akina Esta na wengineo. Wacha vifutwe tu maana hakuna namna nyingine
 
Lumumba wanataka kutuondoa kwenye hoja ya Jessica!!
mkuu,wewe ni genious!njoo uku iramba nikupe nyama ya punda na mafuta ya alzeti!
You must be genius mkuu,haswa hilo ndo lengo.
hawa watu hawafai,ahahaha!ila tunawashukuru kujua kuwa limewagusa hili la ukilaza wa first daughter!
Wanatutoa kwenye hoja ya msingi tumewashtukia hawa vilaza wa ccm
ahahaha,mkuu nashukuru umenishtua namie!
Baba kilaza katika ubora wake
ahahaha
 
Hiyo ni tetesi tu ambayo imeletwa na mtoa mada,halijadhibitishwa na hata kama likipita si kwa kipindi hiki ila itakuwa ni kwa mwaka 2020.
Ila atakuwa kawajibika dhidi ya shutma za Rais kuteua watu wake kwa malengo elekezi
 
viti maalumu ni chaka la viongozi wa vyama kuwabeba watu wasio na sifa hata chembe ya kuwa wabunge samahan kwa wale wanaopata nafasi hizo kwa uwezo na sio kubebana. Najiuliza hivi inakuwaje mtu kama Mukya na yule mkwe wa Ndesambulo walipata nafasi ya kuwa wabunge wa viti maalum alafu mtu kichwa kama mama Anna Mghwira akakosa
Usichanganye watu wa vyama tofauti. Kwanza wanaopata ni wale walioomba. Hawezi kuchukuliwa ambaye hajaomba na hataki. Siasa yetu ni ngumu na watu wengi hawashiriki. Hata wewe inawezekana unapiga domo hapa Jf tu lakini hushughuliki na ujenzi wa demokrasia ktk vyama hivyo. Wa TZ tunapaswa kushiriki ujenzi wa siasa kwa matendo na si kupiga domo pembeni na kulaumu mfumo ambao wewe husaidii kuuimarisha
 
Na kama anataka watanzani tumwone mzalendo ahakikishe Jesca John Magufuli anafukuzwa pale UDOM.
 
Kati ya RAS, RC, DC na MD wawili hapo nao ni mizigo, wawili tu wanaweza kufanya kazi ya hao wote wanne
Kumekucha ila kwa sisi watoto wa hawa watu mnatuonea tutakua tunapanda gari za stk wapi, Hahahahhahahahahaha kimenuka waue
 
Wabunge viti maalum wajengewe bunge maalum. La sivyo watafute alternative

mkuu inshu hapa ni mzigo kwa walipa kodi, je kwa hili wazo lako tutakuwa tumetua mzigo? mi naona tutakuwa tumeongeza mzigo
 
viti maalumu ni chaka la viongozi wa vyama kuwabeba watu wasio na sifa hata chembe ya kuwa wabunge samahan kwa wale wanaopata nafasi hizo kwa uwezo na sio kubebana. Najiuliza hivi inakuwaje mtu kama Mukya na yule mkwe wa Ndesambulo walipata nafasi ya kuwa wabunge wa viti maalum alafu mtu kichwa kama mama Anna Mghwira akakosa
Pia inakuwaje kwa baadhi ya wabunge wa viti maalum CCM kupata nafasi hizo kwa kubebwa au rushwa ya ngono.
 
Back
Top Bottom