Tetesi: Rais Magufuli kutangaza uraia pacha akifunga kongamano la siku mbili la diaspora hapa Zanzibar!

Tetesi: Rais Magufuli kutangaza uraia pacha akifunga kongamano la siku mbili la diaspora hapa Zanzibar!

Status
Not open for further replies.
Uraia ni suala la katiba na kisheria hawezi kutoa tamko bila kubadilisha katiba na sheria kwanza.
Kufuta mikutano ya kisiasa ambayo ipo kikatiba ilihitaji kubadilisha sheria na katiba?
 
Mleta mada unaota.Uraia pacha Tanzania sahau.Tena sahau kabisa.Watu wenye uraia pacha ndio waliopindua nchi zote za kiarabu kwenye yale mapinduzi yanayoitwa Arab springs.Kuanzia Libya,TUnisia,misri,Iraq nk kote.Hata mapinduzi ya Irani ya akina Ayatolah yaliongozwa na watu wenye uraia pacha.Ukienda Uganda ,rwanda,Congo,Burundi,ghana,liberia,nigeria kote huko waliopindua serikali ni watu wenye uraia pacha.Walikuwa na uraia wa nchi zingine wakajiunga huko walikokuwa nchi zao ziliporuhusu wakajiunga na wakoloni baba zao kwennda kupindua hizo nchi.Sehemu kubwa ya Afrika hakuna success story ya watu wenye uraia wa nchi mbili.

Uraia wa nchi mbili kuruhusiwa ni hadi bunge lipitishe sio swala la raisi kutangaza kama hujui.

Hilo la uraia wa nchi mbili Zanzibar mnalipigia debe mnataka yule sultani wa Zanzibar na vizazi vyao vilivyoko Oman vilivyopinduliwa warudi Zanzibar kama kizazi cha mfalme wa Libya KILICHOPINDULIWA na Gadafi kilivyorudi Libya na kuirudisha bendera ya mfalme wa Libya na kuiondoa bendera ya akina Gadafi?
Kampeni yenu ya uraia wa nchi mbili sahauni sio kipau mbele cha nchi yetu kwa sasa kwenye HAPA kazi tu
Kwani mikutano ya kisiasa si ipo kikatiba na imekuwa provided kwenye sheria inayohusu mambo vyama vya siasa na siasa kwa ujumla?

Mbona imefutwa na kuombwa isubiri 2020 Bunge lilikaa lini kufanya amendment ya hizo Sheria na Katiba?

Au vifungu na Ibara za sheria na katiba vinavyohusu Siasa vimekuwa Repealed pale Ukawa waliposusa Bunge?
 
Sijibu ulichoandika ila ninataka kusema umemishangaza sana na uchambuzi wako usio na mashiko. This is the best nonsensical argument for 2016!
Kakopi sehemu huyo [emoji23] kuna wafuasi wa vyama vyetu vya SIASA WANATIA KINYAA KWAKWELI!

Ni kama wamefyatuka akili, sio wafuasi wa CCM wala Opposition ni wale wale wao nyekundu inaweza kuwa Khaki muda wowote ule provided kazungumza KIONGOZI WAKE.

Mfano huyu anasema Mpaka Bunge liridhie kuwa na uraia pacha ndio itawezekana, hapa anataka kusema WABUNGE WA CCM watapinga Kauli ya Mtukufu asiyejaribiwa akiamua kukubali uraia pacha katika Nyumba yake?

Anapinga kwamba uraia pacha hauwezi kuwa hata kama raisi atatoa baraka zake mpaka Bunge likubali, mbona kafuta Mikutano ya vyama vya siasa kwa tamko moja wakati hiyo mikutano ya vyama vya siasa ipo kikatiba?

Vijana wakiTanzania tunasafari ndefu sana kuelekea Mapinduzi ya kiuchumi na kifikra.

Mpe assignment akiweza ajichange change zikipungua aje nimepe akafanye ziara Ethiopia ilivyofaidika na DUAL CITIZENSHIP.

Mchwa Shababi
 
Uraia ni suala la katiba na kisheria hawezi kutoa tamko bila kubadilisha katiba na sheria kwanza.

Kupiga marufuku mchanga wenye madini kwenda nje ya nchi ni suala la kisheria. Ilaalikataza badae akaumbuka.
 
Mnaanza kumwekea Rais maneno mdomoni sijui nani kawaroga nyie watu.
 
Uraia ni suala la katiba na kisheria hawezi kutoa tamko bila kubadilisha katiba na sheria kwanza.

Mbona tayari masula mengi ya kikatiba yanaendelea kuvunjwa? Haishangazi na hili likitokea maana mambo ni kwa mfumo huo huo tu wa one man's show
 
Mleta mada unaota.Uraia pacha Tanzania sahau.Tena sahau kabisa.Watu wenye uraia pacha ndio waliopindua nchi zote za kiarabu kwenye yale mapinduzi yanayoitwa Arab springs.Kuanzia Libya,TUnisia,misri,Iraq nk kote.Hata mapinduzi ya Irani ya akina Ayatolah yaliongozwa na watu wenye uraia pacha.Ukienda Uganda ,rwanda,Congo,Burundi,ghana,liberia,nigeria kote huko waliopindua serikali ni watu wenye uraia pacha.Walikuwa na uraia wa nchi zingine wakajiunga huko walikokuwa nchi zao ziliporuhusu wakajiunga na wakoloni baba zao kwennda kupindua hizo nchi.Sehemu kubwa ya Afrika hakuna success story ya watu wenye uraia wa nchi mbili.

Uraia wa nchi mbili kuruhusiwa ni hadi bunge lipitishe sio swala la raisi kutangaza kama hujui.

Hilo la uraia wa nchi mbili Zanzibar mnalipigia debe mnataka yule sultani wa Zanzibar na vizazi vyao vilivyoko Oman vilivyopinduliwa warudi Zanzibar kama kizazi cha mfalme wa Libya KILICHOPINDULIWA na Gadafi kilivyorudi Libya na kuirudisha bendera ya mfalme wa Libya na kuiondoa bendera ya akina Gadafi?
Kampeni yenu ya uraia wa nchi mbili sahauni sio kipau mbele cha nchi yetu kwa sasa kwenye HAPA kazi tu

Sasa haraka ya kuleta Tetesi usizo kuwa na uhakika nazo ni wa nini. Kama ni kweli alikuwa amepanga si akisoma humu au akiambiwa si ataghairi kutangaza? Mimi naunga Mkono Hoja ya Uraia Pacha.
 
Halafu mtu kasema tayari habari "zisizozakuaminika..." kwa wakati huu tutazichukua hivyo hivyo tu nategemea kuwa zitakuwa kweli.
 
Tanzania itajengwa na Watanzania.... Nyie Diaspora mkae huko huko... Mmeikimbia Tanzania mnataka uraia wanini tena??

Kwani nyie mnachangia kutuletea tabia za ajabu ajabu... Mpigwe marufuku hata ardhi ya Tanzania msifiki mkiwa hai ama mmekufa..
 
KIAZI at its best! Ninamashaka sana na uelewa wako kiasi siamini hata unaweza kutumia keyboard. Labda umeandikiwa. Umeshapewa Mifano ya nchi zenye uraia pacha na kuonyeshwa jinsi nchi hizo zinanufaika lakini bado unakuja hapa na kuandika ujinga. By the way, unajua maana ya www unayoiona kwenye internet? Ina maana hii- World Wide Web. Hivyo huhitaji diaspora kuja Tz kuleta hizo tabia unazosema. Internet inatosha na Kama unayo nyumbani hiyo ndiyo inatakiwa upambane nayo na sio diaspora. Umenielewa?
 
Unampa mgeni uraia wa kitanzania wakati hatakiwi kuukana wa kwao hata akikurudishia passport yake yeye Bado ni raia wa huko alikotoka
Ila hamtaki tuwapatie uraia pacha watanzania wenzetu waliotuacha bongo na wakaenda kutafuta maisha ughaibuni.
Tuna upungufu wa kufikiri sababu ugali na ma vumbi yameshatuadhiri
 
Mleta mada unaota.Uraia pacha Tanzania sahau.Tena sahau kabisa.Watu wenye uraia pacha ndio waliopindua nchi zote za kiarabu kwenye yale mapinduzi yanayoitwa Arab springs.Kuanzia Libya,TUnisia,misri,Iraq nk kote.Hata mapinduzi ya Irani ya akina Ayatolah yaliongozwa na watu wenye uraia pacha.Ukienda Uganda ,rwanda,Congo,Burundi,ghana,liberia,nigeria kote huko waliopindua serikali ni watu wenye uraia pacha.Walikuwa na uraia wa nchi zingine wakajiunga huko walikokuwa nchi zao ziliporuhusu wakajiunga na wakoloni baba zao kwennda kupindua hizo nchi.Sehemu kubwa ya Afrika hakuna success story ya watu wenye uraia wa nchi mbili.

Uraia wa nchi mbili kuruhusiwa ni hadi bunge lipitishe sio swala la raisi kutangaza kama hujui.

Hilo la uraia wa nchi mbili Zanzibar mnalipigia debe mnataka yule sultani wa Zanzibar na vizazi vyao vilivyoko Oman vilivyopinduliwa warudi Zanzibar kama kizazi cha mfalme wa Libya KILICHOPINDULIWA na Gadafi kilivyorudi Libya na kuirudisha bendera ya mfalme wa Libya na kuiondoa bendera ya akina Gadafi?
Kampeni yenu ya uraia wa nchi mbili sahauni sio kipau mbele cha nchi yetu kwa sasa kwenye HAPA kazi tu

Haupo sahii kwa hayo kwa sababu Hitler hakuwa na uraia pacha kutaka kupindua dunia nzima, Addi Amini hakuwa na uraia pacha kutaka kuchukua kagera ile sehemu ya Uganda. Na wengine wengi
Dunia ya sasa ni vigumu kuwa hata na mawazo ya kufanya mapinduzi kwa sababu demokrasia inakuwa kwa kasi kubwa.
Uraia pacha hauna uhusiano wote na hayo mawazo yako maana wote wanaofanya uhalifu hata sasa hivi Tanzania ni hao walio ndani ya nchi.
Walio mafisadi na wadanganyifu, na wanao batili vyeti vya shule na wafanyakazi hewa, wote hao ni watanzania waliokuwa ndani ya nchi. Hivo kama ni mapinduzi mtu asiyekuwa mwaminifu na sio mtu kwa sababu ya uraia pacha.

Sisi watanzania tulio nje ya nchi utakuta ni wazalendo zaidi kuliko hata walio ndani maana sisi hatuwezi hata kuiibia nchi yetu kwa jinsi tunavyoipenda na junsi tunavoisaidia hata sasa kupitia Diaspora.

Labda tukuelimishe kwamba uraia pacha utatusaidia kufanya biashara nje ya nchi kirahisi, kusafiri nchi mbali mbali na passport ya tanzania kuna mlolongo mrefu wa kuomba visa na kukataliwa hivo biashara zetu zinasimama. Uraia kama wa nchi za dunia kwanza utakuwezesha kuokoa mda mwingi kwenye biashara, kuingia na kutoka nchi za nje kwa biashara.

Kingine, uraia pacha unasaidia watanzania wenzako kulipa pesa ndogo kwenye shule za nje na huduma nyingi kubwa za nje ya nchi ambazo kama tunajua nyie mlio nyumbani umekuwa mkilalamika matumizi makubwa wa viongozi kwenye hospitali za nje. Kama unafahamu Raisi kapiga marufuku safari hizi kwa sababu matumizi makubwa. Ila wenye uraia pacha wanatibiwa bure nchi hizi au kwa pesa ndogo sana hivo inawasaidia kimaisha na kuwapunguzia mzigo wa kifedha. Labda kama useme hili La mtanzania nwenzako kupata benefits hizi linakukera.

Watanzania walioko nje ya nchi kwa taarifa yako hawana hata haja ya kazi za serikali au kuingia kwenye siasa tanzania. Nia yao ni kunufaika kibiashara kwa uraia pacha ili watulie hizi pesa nchini Tanzania kuleta maendelea na manufaa kwa kufungua biashara kama wazaelendo.

Mwisho, uraia pacha utawezesha serikali kukusanya mapato hata kwa watanzania walio nje ya nchi kuchangia shuguli za maendeleo. Sasa hivi huwezi kumchangisha mtu au kumpa sheria hiyo atoe kodi wakati hata humtambui kama mtanzania. Hivo inayokosa manufaa ni Tanzania kwa ujumla na Mtanzania mwenzako unamuwekea ugumu usio na lazima.

Tufunguke mawazo sasa, sote tunaipenda tanzania hivo wala msituelewe vibaya. Sisi tukifanikiwa na nyie mnafanikiwa maana biashara tunazoanzisha zina ajiri ndugu zako na pesa za kodi zitajenga barabara, hospitali nk ili hata wewe unayesoma email hii upate nafuu ya kulipa kodi. Yaani kila mtanzania ndani na nje ya nchi achangie maendeleo ya nchi yetu.

Hili ni jambo la maendeleo ungeni mkono uraia pacha bungeni nchi yetu ipige hatua tuache siasa sasa maana siasa zinawagawanya wananchi na kuleta mifarakano bila maendeleo. Kenya, South Africa na nchi nyingi za africa zina uraia pacha na tazameni pesa zinavoingia. Uzalendo sio kukaa tanzania miaka yote tu, nakuwagomea wengine maendeleo kisa tu wanatumia uraia pacha kibiashara, mzalendo ni yule aliye tayari kuitumikia nchi yake popote alipo akihitajika na nchi yake, kwa ajili ya nchi yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom