Mleta mada unaota.Uraia pacha Tanzania sahau.Tena sahau kabisa.Watu wenye uraia pacha ndio waliopindua nchi zote za kiarabu kwenye yale mapinduzi yanayoitwa Arab springs.Kuanzia Libya,TUnisia,misri,Iraq nk kote.Hata mapinduzi ya Irani ya akina Ayatolah yaliongozwa na watu wenye uraia pacha.Ukienda Uganda ,rwanda,Congo,Burundi,ghana,liberia,nigeria kote huko waliopindua serikali ni watu wenye uraia pacha.Walikuwa na uraia wa nchi zingine wakajiunga huko walikokuwa nchi zao ziliporuhusu wakajiunga na wakoloni baba zao kwennda kupindua hizo nchi.Sehemu kubwa ya Afrika hakuna success story ya watu wenye uraia wa nchi mbili.
Uraia wa nchi mbili kuruhusiwa ni hadi bunge lipitishe sio swala la raisi kutangaza kama hujui.
Hilo la uraia wa nchi mbili Zanzibar mnalipigia debe mnataka yule sultani wa Zanzibar na vizazi vyao vilivyoko Oman vilivyopinduliwa warudi Zanzibar kama kizazi cha mfalme wa Libya KILICHOPINDULIWA na Gadafi kilivyorudi Libya na kuirudisha bendera ya mfalme wa Libya na kuiondoa bendera ya akina Gadafi?
Kampeni yenu ya uraia wa nchi mbili sahauni sio kipau mbele cha nchi yetu kwa sasa kwenye HAPA kazi tu
Haupo sahii kwa hayo kwa sababu Hitler hakuwa na uraia pacha kutaka kupindua dunia nzima, Addi Amini hakuwa na uraia pacha kutaka kuchukua kagera ile sehemu ya Uganda. Na wengine wengi
Dunia ya sasa ni vigumu kuwa hata na mawazo ya kufanya mapinduzi kwa sababu demokrasia inakuwa kwa kasi kubwa.
Uraia pacha hauna uhusiano wote na hayo mawazo yako maana wote wanaofanya uhalifu hata sasa hivi Tanzania ni hao walio ndani ya nchi.
Walio mafisadi na wadanganyifu, na wanao batili vyeti vya shule na wafanyakazi hewa, wote hao ni watanzania waliokuwa ndani ya nchi. Hivo kama ni mapinduzi mtu asiyekuwa mwaminifu na sio mtu kwa sababu ya uraia pacha.
Sisi watanzania tulio nje ya nchi utakuta ni wazalendo zaidi kuliko hata walio ndani maana sisi hatuwezi hata kuiibia nchi yetu kwa jinsi tunavyoipenda na junsi tunavoisaidia hata sasa kupitia Diaspora.
Labda tukuelimishe kwamba uraia pacha utatusaidia kufanya biashara nje ya nchi kirahisi, kusafiri nchi mbali mbali na passport ya tanzania kuna mlolongo mrefu wa kuomba visa na kukataliwa hivo biashara zetu zinasimama. Uraia kama wa nchi za dunia kwanza utakuwezesha kuokoa mda mwingi kwenye biashara, kuingia na kutoka nchi za nje kwa biashara.
Kingine, uraia pacha unasaidia watanzania wenzako kulipa pesa ndogo kwenye shule za nje na huduma nyingi kubwa za nje ya nchi ambazo kama tunajua nyie mlio nyumbani umekuwa mkilalamika matumizi makubwa wa viongozi kwenye hospitali za nje. Kama unafahamu Raisi kapiga marufuku safari hizi kwa sababu matumizi makubwa. Ila wenye uraia pacha wanatibiwa bure nchi hizi au kwa pesa ndogo sana hivo inawasaidia kimaisha na kuwapunguzia mzigo wa kifedha. Labda kama useme hili La mtanzania nwenzako kupata benefits hizi linakukera.
Watanzania walioko nje ya nchi kwa taarifa yako hawana hata haja ya kazi za serikali au kuingia kwenye siasa tanzania. Nia yao ni kunufaika kibiashara kwa uraia pacha ili watulie hizi pesa nchini Tanzania kuleta maendelea na manufaa kwa kufungua biashara kama wazaelendo.
Mwisho, uraia pacha utawezesha serikali kukusanya mapato hata kwa watanzania walio nje ya nchi kuchangia shuguli za maendeleo. Sasa hivi huwezi kumchangisha mtu au kumpa sheria hiyo atoe kodi wakati hata humtambui kama mtanzania. Hivo inayokosa manufaa ni Tanzania kwa ujumla na Mtanzania mwenzako unamuwekea ugumu usio na lazima.
Tufunguke mawazo sasa, sote tunaipenda tanzania hivo wala msituelewe vibaya. Sisi tukifanikiwa na nyie mnafanikiwa maana biashara tunazoanzisha zina ajiri ndugu zako na pesa za kodi zitajenga barabara, hospitali nk ili hata wewe unayesoma email hii upate nafuu ya kulipa kodi. Yaani kila mtanzania ndani na nje ya nchi achangie maendeleo ya nchi yetu.
Hili ni jambo la maendeleo ungeni mkono uraia pacha bungeni nchi yetu ipige hatua tuache siasa sasa maana siasa zinawagawanya wananchi na kuleta mifarakano bila maendeleo. Kenya, South Africa na nchi nyingi za africa zina uraia pacha na tazameni pesa zinavoingia. Uzalendo sio kukaa tanzania miaka yote tu, nakuwagomea wengine maendeleo kisa tu wanatumia uraia pacha kibiashara, mzalendo ni yule aliye tayari kuitumikia nchi yake popote alipo akihitajika na nchi yake, kwa ajili ya nchi yake.