Tetesi: Rais Magufuli 'kuutumbua' Mwenge wa Uhuru

mtumishi Hewa Number moja huyu hapa
 

Attachments

  • IMG-20160403-WA0083.jpg
    23.5 KB · Views: 110
sirahisi kufuta mwenge maana umekaa kiccm zaidi na sisi kina gogo lashamba tulishawaambieni Makufuli hawezi kufanya lolote kwenye mambo yanayohusu ccm,hapo ataifanya hana uwezo nako kama alivyofanya kwa yule aliyepeleka zuio feki kwenye uchaguzi wa meya wa Dar, mwenye masikio na asikie
 
Mwenge ni kitu muhimu sana katika Taifa hili. Mwenge ndio unaotupa mwanga katika Taifa letu na kutuepusha na majanga.

Kuuondoa maana yake wanataka Taifa letu liwe Giza.

Hizo ni njama za watu wenye mapepo na wasiokuwa na Dhamira njema katika Taifa letu. Tuwapuuze!

Ushauri; Kutokana na Rushwa (Giza) kuendelea kushamiri katika Taifa letu, ni vyema sasa Mwenge ukawa unawashwa mara Tatu kwa mwaka ili kupunguza tatizo la Rushwa katika Taifa letu.

Asante
 
Majukumu yanayodhaniwa kutekelezwa wakati wa mwenge, ni yale yanayopaswa kutekelezwa na viongozi na watendaji kama wajibu wao wa kila siku. Job descriptions zao zinatosha. Hakuna sababu ya hamasa ya ziada.
 
Reactions: MTK
Anayepinga mwenge kukimbizwa na kutumika kuzindua miradi ambayo tusingejua kama IPO si mwenzetu. Ni mgeni.
 
Sijui ni ngapi zitaokolewa hapo, kama atafuta bora ungepigwa mnada tena wa sotherby auction maana tutapata hela za uhakika hapo
 
Kuna uvumi ambao pengine hata wengine mshawahi usikia kwamba kila kiongozi wa mbio za mwenge lazima afe, kuna ukweli wowote ktk hili?
 
Nimeipenda taadhari yako MKUU.
 
 
Hakuna kitu kina tudhalilisha kama kukimbiza mwenge tena kwa gharama kubwa kwani kama ni uzinduzi wa miradi huwezi kufanyika bila Mwenge? Vijijini watu wanateseka sana na michango lukuki. Nasema na ufutwe kabisa kwani unatudhalilisha sana.
 
Na utatumbuliwa tu.

Hatuwezi kupoteza mamilioni ya pesa huku..

1. Watanzania hawana hospital na zahanati vijijini. Wamama wajawazito na wengi wanapotez maisha kila siku kwa kukosa huduma za afya then tuendelee kuishi kwa hotuba na usanii kwenye mwenge. Hzo hela zikajengee vituo vya afya vijijini

2. Hospitali nyingi hazina dawa na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma ya afya. Bado tunganganie kupoteza mamilioni ya hela kukimbiza mwenge.

3. Wapo watoto wengi wa masikini vijijin na baadhi ya miji hawana madarasa ya kusomea na hata walio na madarasa hawana madawati ya kusomea. Bado unatetea nadharia ya kukimbiza mwenge kuwa ni maendeleo.

4. Shule nyingi hazina vitabu na vifaa vingine kwa ajili ya kuendeleza elimu yetu. Elimu.ndo mkombozi mkubwa kwa taifa. Kama ilivgokwisha kuanishwa ujinga ni adui wa mtanzania. Hatuwezi kuondoa ujinga kwa kukimbiza mwenge tunatakiwa kuinvest hela nyingi kwenye elimu. Kwanini tuendelea kupoteza hela kukimbiza mwenge wakati tunaweza kutumia hiyo hela kuinua elimu yetu?

5. Wapo wanafunzi wengi wenye uwezo wa kiakili wa maskini lakini wanakosa kujiunga vyuo kila mwaka kwa kukosa ada. Kwanin hii hela isiende katika fungu la kuwasaidia na kundi hili linalokosa elimu?

6. Miundo mbinu mingi haijakaa vizuri. Hizo hela zinaweza kujenga barabara kadhaa lami katika mikoa mojawapo Tz. Why tupoteza hii hela bila msingi wowote?

7. Tanzania sasa hvi haina ndege hata moja. Hii hela nina imani inaweza angalau ikanunua hata ndege moja au mbili. Kwa miaka mitano kama tukiamua kuinvest hii hela sehemu.moja tuseme kwenye Aviation industry baada ya miaka mitano tutakuwa mbali sana. Baada ya miaka kumi tukifanya tadhimini hela ambayo tumewekeza kwenye Industry kama hii tutakuwa mbali sana. Na tunaweza kuwa na kitu cha kujivunia tofauti.na kupoteza hela bila mpango wowote.

Watanzania hebu tuwaze kama watu waliokatika ulimwengu unaenda kwa kasi kubwa sana ya maendeleo. Tusiwaze kama watu walio katika miaka 1961 ya kupata uhuru. We are in another era that needs changes of minds. We real need to think out of the box. Tusifungwe na sera ajabu ajabu.

Me namkubali Mh Magufuli maana anafanya maamuzi ambayo kweli mengi ni katika kutuondoa katika mfumo wa kuwaza kizamani zamani tu. Viongozi wanakuwa na sera za kizamani ambazo hazimkomboi mtanzania.


Kitaeleweka tu hata kwa kulazimishwa.
 
hili ni pigo kwa wacheza viduku wa CCM walikuwa wananufaika na hiki kibatari.
 
Wapinzania huwa nawashangaa sana maana mawazo yao yapo katika kupinga kila kitu, sasa mkishamaliza hili la mwenge mtahamia na jingine mpaka mtakapo kuja tambua kwamba tatizo sio vitu bali ni mtu ukweli ni kwamba watanzania ni wavivu na hatupendi kujishughulisha hivyo tunapenda kusingizia kila kitu kua ndio vinavyotusababishia umaskini wetu kumbe sio, kwa tabia hii ya kinafiki tutasingizia mpaka wanyama wa serengeti ndio wanaotusababishia umaskini wetu tubadilike.
 

Kila mtanzania anayejitambua anafaufahamu mwenge.
Huu ni muda wa kujiendeleza kiuchumi badala ya kuendeleza yaleyale ya siku zote tukitegemea mabadiliko, Mheshimiwa Mwenge upigwe chini, manake hakuna namna
 
Unaropoka tu....tueleze katika karne hii hizo ritual zinasaidiaje taifa ....pia tueleze faida za kuonekana za mwenge....

Uachage unoko bhana....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…