Tetesi: Rais Magufuli 'kuutumbua' Mwenge wa Uhuru

Sababu zake zinajulikana. Na kauli mbio yake inaeleweka "Tutawasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike mpaka nje ya mipaka yetu, ulete matumaini pale pasipo na matumaini, ..." Haya yanaweza kuhamasishwa bila gharama kubwa kama kukimbiza mwenge nchi nzima, au ikafanyika mara moja kwa miaka mitano. Tunaweza pia kuweka vipindi maalum kwenye radio za TV za TAIFA kuhusu kuhamasisha uzalendo n.k. Kwamba ulianzishwa na akina Nyerere haimaanishi hatuwezi kubadisha mfumo bila kupoteza maudhui. Usimdhalilishe mwalimu aliyekufundisha kwa kukalili tu matukio.
 
Zaidi ya mafuta ya taa na chakula na malazi kwa kiongozi wa mwenge gharama zingine ni zipi?
 
Kila mtanzania anayejitambua anafaufahamu mwenge.
Huu ni muda wa kujiendeleza kiuchumi badala ya kuendeleza yaleyale ya siku zote tukitegemea mabadiliko, Mheshimiwa Mwenge upigwe chini, manake hakuna namna
Tatabhyala....umesema vyema sana....hatuwezi kama taifa kuendelea na Yale Yale ya kila siku ambayo yanachangia maambukizi ya UKIMWI...

ni vyema tukawa na tafakuri mpya yenye kuibua vyombo vipya ambayo vitachangia maendeleo ya wananch....sio porojo kila siku na kutengeneza mazingira ya watu kupiga pesa ...

obhe nomolembe poti,,,,,,
 
Bila kuondoa hiyo sanamu.jitihada za kubana matumizi itakuwa kazi bure
 
Unaropoka tu....tueleze katika karne hii hizo ritual zinasaidiaje taifa ....pia tueleze faida za kuonekana za mwenge....

Uachage unoko bhana....


Kazi ya kuwakaririsha watu nationalism propaganda sio rahisi wala cheap, tusione vya wenzetu vinaelea vimeundwa.

Jaribu kuingia huko kinyume na siasa zao halafu uone moto wao wanaacha ugomvi wao wowote wewe ndio unakua hadui kwanza wakimalizana na wewe wanaendelea na yao.


Jana CUF wamesema awamtambui Dr Shein kama raisi, viongozi wa serikari yake, wala uchaguzi; halafu unategemea kufuta sikukuu za muungano wa taifa lako na ritual zako ambazo zinafaida kwako kama tools which build nationalism awareness aint that just pathetic.

Haya mambo sio rahisi kabisa na bei yake wala sio nafuu ndio maana kuna tofauti kubwa sana kati ya Tanzania aliyoicha Nyerere na mataifa walioachiwa majirani zetu baada ya maraisi wao wa kwanza kutoka hela na akili ilitumika kwetu mpaka hapa tulipo.
 
Mwenge wa Uhuru ni maagano ya kuzimu. Kwa dunia ya leo ni ujuha kuendekeza ushirikina ambao si tu una viashiria dhahiri vya kudumaza fikra chanya kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia bali pia unaendekeza matumizi mabovu ya pesa na kuteketeza nguvu kazi ya taifa kwa maambukizi ya ukimwi!

Napendekeza mwenge uteketezwe kwa kuchomwa moto hadharani kisha jivu lake limwagwe baharini tuondokane na laana hii.
Hakuna haja hata ya kuuweka makumbusho make tutachekwa na vizazi vijavyo.
 
Nadhani ni vyema ushauri huu ungeuelekeza kwa Mheshimiwa Rais kwamba alichofanya si sahihi, sisi wengine tupo hapa kumuunga mkono Rais katika juhudi zake za dhati za kuirudisha nchi kwenye mstari.

Kama woga wako ni kukosa zile posho za kukimbiza mwenge nchi nzima na kusambaza virusi njoo kule jukwaa la ujasiriamali tutakufundisha namna ya kujitegemea kwa kuanza ujasiriamali kwa mtaji mdogo tu.

Ifike wakati haya maisha ya ujanjaujanja kujikomba kwa wanasiasa yafike mwisho, sasa vijana mjitume na msitumie all the day mitandaoni una assets gani wewe?
 
Tatizo lako umejikuta huko kwenye amani ambayo hujui misingi yake ndio maana uwezi kuelewa jitihada wenzako walizotumia kukufanya wewe utambe leo la sivyo ungewepa heshimu mawazo yao kuweza kufikiria amani yako kabla aujazaliwa.

Ndio maana ni ngumu sana kuona athari za mambo unayo yaona rahisi; wazungu
wanamsemo wao its only easier if only you know it.

Just stick na siasa za CDM na CCM au mambo ya ufisadi mambo usiyoyaelewa madhara yake achana nayo.
 

Maana kubwa ya mwenge ni matambiko tu hamna namna nyingine.
 
Kama mh Magufuli akiutumbua mwenge atakuwa ni rais wangu wakuigwa yaani akitoka Nyerere anayefuata Magufuli
 
Utumbuliwe bila ganzi
 
kazi yake ni kusambaza ukimwi
 
Kwakuwa umekuwa muungwana kutaka kujuwa ngoja nikupe siri, mimi binafsi mwaka 2000 gari yangu nilipewa pande iwepo kwenye msafara wa mbio za mwenge najuwa pesa niliyolipwa na cha juu alichochukuwa yule kada aliyenipa pande.

Ni hi kiongozi mkuu wa mbio za mwenge mmoja lakini Team ni kubwa na hiko hivi;

Team ya kitaifa, hawa wakimbiza mwenge nchi nzima.
Team ya mkoa
Team ya wilaya
Team ya kata
Polisi
Usalama
Hizo Team zote hapo wanalipwa posho kwa kazi hiyo ya kukimbiza mwenge, na mafuta ya mwenge ni kidogo sana hata mimi naweza kuyagharamia, tatizo ni mafuta ya msafara wa magari lukuki posho za madereva na gharama za chakula kwa hao wote niliyowaorodhesha hapo pamoja na kuwalipia Hotel,motel whatever u can wanapozunguka mikoani na mawilayani, ndio maana ili serikali isishtuke ufisadi wa mbio za mwenge ubunifu umefanyika kuwakamuwa wafanyiabshara na wenye viwanda nchi nzima ili waendeleze huu ujambazi wao hata serikali ikisema haina pesa wao wana uwezo wa kuwadhurumu raia ili mradi wamalizie miradi yao binafsi.
 


Huo mwenge hauna lolote la maana zaidi ya ku brainwash watu, kusambaza maradhi ya ngono na ufisadi. Miradi ya maendeleo ikizinduliwa bial mwenge haileti maendeleo?

Kuenea kwa kauli mbiu ama vipaumbele vya kitaifa kwa karne hii ambako kila sehemu kuna mawasiliano,kunahitjai mtu akimbize mwenge na kuongea na watu sura kwa sura? Watu wangapi wanasikilizaga hayo maneno zaidi ya kushangaa vijana wanaokula moshi wa mafuta hatimaye kufupisha maisha yao?

Kama kuna kauli mbiu yakitaifa ambayo kila mtu anatakiwa imfikie, tumia vituo vya televisheni, tumia redio, tumia jamii forum, mitandao ya udaku ambayo hata wauza baa ni wanachama, tumia jumbe za simu, si mna number zote za simu? Hii biashara ya kusambaza magonjwa ya zinaa, na kutumia fedha za umma kwa ufisadi huku watu wakilazimishwa kuchangia kwa kitu kisicho tija, halikubalikil.

Ninaumga mkono hoje, mwenge ufutwe labda uwekwe makumbusho kama kumbukumbu ya matumizi ya kufiksha habari kwa watanzania kipindi mawasiliano yalikuwa magumu. Hakuna Nyongeza!.
 

Kuna wengine hapa na hasa wengi wao hawakuwepo wakati wwe na nyerere mnaanzisha mwenge. Kwa kuwa wewe unajua, toa hapa sababu hizo ili wtu wakuelewe na wasimamie kutetea ukimbizwaji wa huo mwenge. Kama hujui, nyamaza. hakuna nyongeza.
 
kazi yake ni kusambaza ukimwi
Hapana kazi yake ni kukuamsha wewe mtanzania kwamba sisi sio koloni la mtu ni nchi huru na tunayojitegemea na kila raia anajukumu la kulinda uhuru wa Tanzania hizo ndio sababu za mwenge; na kila mwaka unapita kwa sababu ya kukumbushana sasa ukiona mtu anaupinga hajui Tanzania imejengwa vipi au huo umoja umejengwa vipi.
 
Tukiachana na kua hili jipu la mwenge linatugharimu sana financially, lakini pia Watoto wengi wasio na Baba wanazaliwa kupitia hili jipu pamoja na kuongezeka maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya zinaa ukiwemo UKIMWI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…