Tetesi: Rais Magufuli 'kuutumbua' Mwenge wa Uhuru

Ili kuenzi historia yetu MWENGE WA UHURU WAWEZA KUKIMBIZWA PALE UWANJA WA UHURU MNAMO TAR. 9 Desember
 

Ni kweli, Mwenge una historia nzito sana. Maneno ya Mwalimu J.K. Nyerere kuhusu Mwenge ni haya: "Tutawasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike mpaka nje ya mipaka yetu, ulete matumaini pale pasipo na matumaini, upendo pale palipojawa na chuki na heshima pale palipojaa dharau" Lakini ukiangalia kwa makini, wakati wake, Nyerere alifanya kweli. Tanzania ilikuwa inawaka nje ya mipaka yake. sisemi kwamba alifaulu alivyotaka, au kwamba hakufanya makosa, hapana, alifanya makosa mengi tu, lakini unaweza kuona alichopanga na alichokusudia na alichofanya. kwa hiyo Mwenge ni ishara ya yale ambayo nchi ilikuwa inafanya.

Lakini hivi sasa sisi kama nchi tunasimamia nini? tumeendesha operesheni kimbunga kuwafukuza "watu wasio raia" ambao kwa hakika ni waafrika wenzetu, isipokuwa ni mkoloni tu ndio alituambia wewe mkongo, wewe mtanganyika, wewe mkenya. wapi misimamo ya umajumui? tumeendesha vituko huko Zanzibar ambavyo tumeviita "uchaguzi wa marudio", nchi inapigwa kila kona huku viongozi wakiongoza upigaji. hapo kuna "kuleta matumaini pale pasipo matumaini"? watanzania tuna matumaini gani kiasi kwamba tuwasaidie na wengine? Kwa kweli kwa mazingira yetu ya sasa, wala hatuhitaji kujifanya tunawamulikia wengine, hivyo zoezi la Mwenge lisitishwe kwanza mpaka hapo tutakapoamua vinginevyo.
 
Hakuna mwenge wala nini kwa sasa,wananchi tuna hali ngum sana ki ukweli. Na vile tumeanza kukataa misaada basi ni bora tu ibaki kua history ili hizo pesa zifae kwa maendeleo ya kujenga nchi. Ila mzee ifikie time asitishe ili ikiwezekana izo ela achimbe ata visima kila mkoa. Na pesa ikipatikana ya ziada basi aipeleke kwenye mashirika mfano tanesco ata ewura ili mafuta yapungue bei coz itakua nafuu kwa mwananchi
 
Sisi tumekwisha kuwasha Mwenge,
Tumekwisha kuwasha mwenge. X2
Na kuuweka juu ya mlima,
Mlima Kilimanjaro. X2

Chorus: kuwasha Mwenge, kuwasha Mwenge, na kuuweka Kilimanjaro. X2

Umulike hata nje ya mipaka yetu,
Ulete tumaini. X2
Pale ambapo hamna matumaini,
Upendo mahali ambapo pana chuki
Na heshima ambapo pamejaa dharau. X2

Mwenge upelekwe Mlima Kilimanjaro, upitie Arusha. Magufuli arudishe Azimio la Arusha rasmi.

Call me whatever you want, but I have my values. Kitu kilichokuwa kinafanya kazi iweje kifanyiwe matengenezo?
 

Mwalimu alifanya kazi kisayansi kwenye kujenga jamii kama ulivyoelezea sababu zake za uwepo wa mwenge. Naambiwa kuna watu vijijini miaka hiyo mwenge ulikuwa ukienda unapokelewa na shamra shamra za ajabu na inakuwa kama sababu ya kukusanyika na kufanya sherehe mpaka unaondoka.

Sasa utamaduni wa aina hiyo sio kwamba watu wanakaa nazo mwaka mzima mwenge ukipita kila mtu anaendelea na yake hila hisia za uzalendo zinakuwa tayari zimeshakuwa implanted ndani mwao at the back f their minds.

Leo mwenge una maana kwa UVCCM tu na wale wanaoukimbiza ndio maana wengi awaoni mantiki kwa nini? kwa sababu serikari aifanyi jitihada zozote za kuuwekea maanani kwenye kuiuza concept ya mwenge, kuujengea umuhimu kitaifa na mambo mengi. Binafsi sikuwahi kuukimbiza mwenge lakini nilikua na hamu ya kuuona na nilikua najua baadhi ya nyimbo zake leo sidhani kama vijana wanazijua nyimbo za mwenge.

Ukienda nchi za wenzetu viongozi wao wakiona watu wanaaza kuwa detached na symbolism and rituals za nationalism, wanaweza kutafuta ata msaada wa makampuni makubwa kama 'Saatchi and Saatchi' wapo tayari kulipa hela wawafanyie market strategy wanaiuza vipi concept.

Vitu aviwezi kuwa na maana baada ya muda mrefu kama jamii inashindwa kuona umuhimu wake; watu wengi awana uzalendo wa vile leo kwanini wasione mbio za mwenge kama upotezaji wa hela tu.

That is enough of a concern hawa jamaa inabidi watafute mbinu mpya za kuuza mwenge kwa kizazi cha leo demographic and perception imebadilika asilimia kubwa kwenye jamii yetu mwenge wameukuta umeshazaliwa na hakuna jitihada zozote zinazotumika kuujengea fikra za propaganda hili ndio tatizo. Sasa tena kuufuta na huo mwenge wenyewe ndio sijui serikari inabaki na tool gani ya propaganda hizi ndio sababu unakuta watu leo wapo loyal either kwa CCM, vyama vya siasa au dini zao; lakini loyalty ya taifa hakuna sana.

Lazima tukubali hivi vitu sio cheap kuviweka lakini faida zake zinatakiwa kujenga uzalendo kama rate inapungua; serikari lazima iangalie wapi inakosea na inarekebisha vipi lakini kufuta ritual za kitaifa sio option kabisa.
 
IMEANDIKWA......."Ole wao wakimbizao mioto na mwenge maana watapata laana vizazi hadi zizazi" .............
Mh.Rais usipate taabu ni nani aliyetuloga.......




Kumbeeeee mkuu kitabu gani hiko nisaidie u.ajua nilikiwa nahisia tu
 
mkuu kwanza binafsi niungane nawe kuwa mwenge hauna manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi, sana sana unaongeza maambukizi ya ukimwi, au ghalama zisizo kuwa na maana, hlo nakubaliana nawe

sasa hoja ni moja kuu, kwa nn mwenge unaendelea kuwepo, watawara huwa wanatoa jib jepesi kuwa ni ishira ya kupata uhuru, na kuonesha kuwa hii nchi ni ya amani, jambo ambalo binafsi haliniingii akilini, anyway tufanye ni kweli lkn faida zake hakuna, matokeo yake imekuwa kitanzi kwa wananchi, hasa wafanyabiashara, waalim na wanakijiji..

nionavyo, kwa kuwa rais anania ya dhati kupana matumizi afanye kubadili hzo sherehe, badala ya kukimbizwa nchi iwekwe kwenye makumbusho mahali ambapo ni katkt kama dodoma, kila mmoja awe huru kwenda pale na kufanya tambiko au kuuona.

mwisho, kunamdau mmoja aliwahi kutoa historia ya mwenge humu jf, kama ni kweli rais wangu magufuri hawezi kuuondoa maana ni zindiko, hakuna namna inabidi tekeleze, sina uhakika kama ataweza kuuondo mwenge, na kama ataweza, hyo ndiyo itakuwa historia kubwa kuliko zote kuwahi kufanyika tz, na huenda akatawala na kuondoka kwa kung,atuka kam alivyofanya nyerere, i mean huenda akafanya kama alivyo fanya mbeki SA..

mwenge ni zaidi ya tuujuavyo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…