Rais Magufuli kuvunja Jiji la Dar es Salaam

Jiulize, ni nani kaamua mtu gani awe diwani wa DSM City Council? Bila shaka, madiwani wa DCC wawanachaguliwa na madiwani wa zile manispaa sita za mkoa wa DSM. Kwa maneno mengine, hakuna mwananchi aliyempigia kura mtu fulani kuwa diwani wa DCC. Hapo ndipo kauli “...hawakuchaguliwa na wananchi...” inapoanzia!
Unaowaelimisha wameishaweka gea ya kuvukia Mto Mara....haijalishi aliyetagulia katafunwa na mamba au kasombwa na mkondo mkali wa maji, nyumbu style!
 
Hivi who cares about this guy?

So destructive

Anaacha real problems with real people anaenda kuvamia vitu hata hajatumwa wala havisadii lolote....

Jiji sio jiji,wilaya sio wilaya,hivi who cares nchi hii hakuna UZALISHAJI which is the basis of life prosperity?
Unaposhindwa ku-solve real problems, una-create stupid ones and focus on them!!That must be his motto 🙂
 
Geografia haibadilishwi. Kinachobadilishwa ni kabaraza kalikokuwa kanaitwa halmashauri ya Jiji. Yaani ile Administration inaondolewa.
Kwa majibu haya mazuri naomba uzi watu wenye upeo wa kufikiri wawaachie uzi vichwa panzi wanaoongozwa na mihemko waendelee kujiliwaza hadi 2025!
 
IMG-20210224-WA0025.jpg
 
Kinachowachanganya wengi ni neno Jiji.

Majiji yote hapa nchini ni sehemu ya serikali za mitaa, ni halmashauri kama zilivyo halmashauri za miji, manispaa na halmashauri za wilaya. Kila halmashauri inakuwa na eneo la utawala, mfano Halmashauri ya Ubungo eneo lake la utawala ni Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Kwembe, Saranga, Sinza, Manzese, Mabibo, ubungo nk, zipo kata 14. Vivyo hivyo Kinondoni ina kata kadhaa zinazounda Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Kata zote zinaongozwa na madiwani ambao wanachaguliwa na wananchi kupitia uchaguzi mkuu.

Sasa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yenyewe haina eneo la utawala kikata, yenyewe inajumlisha manispaa zote za mkoa wa Dar es Salaam. Haina miradi linayosimamia kama vile hospitali, shule za msingi na za sekondari, masoko nk, badala yake lina vyanzo vya mapato kama vile stendi ya ubungo (sasa ya Mbezi aka ya magu), chanzo cha tozo za parking walikua wanavuta vuta magari. Mapato yanayopatikana katika Halmashauri yanatakiwa kufanya shughuli za maendeleo kama kujenga shule, hospitali nk, sasa kwa vile Halmashauri ya jiji la Dar haina hata ardhi wala jukumu la mashule, fedha hizo zikawa zinalipa vikao tu vya madiwani na posho za watumishi. Pia kwa kuwa haina kata, haina hata madiwani wa kuchaguliwa kupitia uchaguzi mkuu badala yake ina madiwani waliochaguliwa baada ya uchaguzi mkuu na madiwani kutoka madiwani wa manispaa zote 5. Yaani Diwani wa H/Jiji ni diwani wa Kata fulani katika H/Manispaa mojawapo. Anaingia vikao vya H/ Manispaa na anaingia vikao vya H/jiji kujadili mambo yaleyale yanayojadiliwa katika vikao vya H/Manispaa aliyotoka, na ndio sababu kuu ya JpM kusema kuwa madiwani hao wa H/jiji hawajachaguliwa na wananchi.

Kumbuka hivi vyanzo vya mapato vya jiji vipo katika maeneo ya Halmashauri za Manispaa, mfano stendi ya Ubungo ipo katika manispaa ya ubungo, ingeweza kabisa kuendeshwa na kusimamiwa na Manispaa ya Ubungo. Kwa hiyo ni kujiongezea gharama na kuwapa ulaji watu kwa kazi ambayo ingeweza kufanywa na H/ za Manispaa.

Majiji mengine kama Tanga, Mbeya, Mwanza nk yana maeneo ya utawala (kata na madiwani). Huwezi ukasema Wilaya ya Rungwe ipo jijini Mbeya utakua unakoasea, H/jiji la Mbeya inaishia Uyole. Sasa kwa Dar ukisema Manispaa ya Temeke ipo ndani ya H/jiji la Dar unakua upo sawa kitu ambacho hakina maana kiutawala. Zaidi ya watu wa jiji kugombana na Manispaa wakitaka vyanzo vya mapato ili tu hela inayopatikana waitafune bila kuifanyia miradi ya maendeleo kwa wananchi.
 
Jiji la Ilala ndani ya mkoa wa Dar?! Mkuu unajua sifa za mkoa na jiji na lipi ni kubwa kuliko mwenzake kweli?
Mkoa ni mkubwa kuliko Halmashauri ya jiji. Dar kuna mkuu wa mkoa wa Dar (RC), halmashauri ya jiji inaongozwa na Mkurugenzi ambaye yupo chini ya mkuu wa Mkoa.
 
We we umefunga Uzi. Naomba niwe wa nwisho kukomenti kwenye huu Uzi.
 
Mkoa ni mkubwa kuliko Halmashauri ya jiji. Dar kuna mkuu wa mkoa wa Dar (RC), halmashauri ya jiji inaongozwa na Mkurugenzi ambaye yupo chini ya mkuu wa Mkoa.
Nimeelewa mkuu 🤝
 
... Dar-es-Salaam utabaki kuwa mkoa ambao utakuwa na jiji la Ilala na manispaa za Ubungo, Temeke, Kinondoni na Kigamboni.
Kama nimekuelewa hivi, kwa sababu ukisema jiji la Dar es salaam ni Manispaa ya Ilala maana yake jina moja hapo litakufa automatically.
Dar es salaam inabaki kama mkoa, Ilala jiji zilizobaki Manispal Council
 
Avunje mara ngapi? JF hamuwezi kwenda na speed ya JPM. Khe khe he kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Hapana Dar litakuwa Jiji kibiashara na siyo kiutendaji! Alyetia uzi huu hakufafanua sana alivyoeleza Mhe Rais! Litabaki jiji la Dar lakini kihalmashauri hakutakuwa na halmashauri ya Jiji la Dar!
Likiwa jiji lazima iwepo mamlaka ya jiji, hapo ndo Rais hataki hayo matumizi yasiyo na lazima.
Kwa Jiji kuwa Ilala maana yake watendaji wote wa Ilala watabaki kuwa wale wale kuanzia Mkurugenzi mpaka Meya. Tofauti ni kuwa sasa watakuwa sio manispaa tena bali Jiji. Ni jubadilisha Mihuri tu na nembo pale juu.
 
Back
Top Bottom