Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 3(1) inasema hivi nanukuu "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi itakayofuata mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu
Tumekuwa tulimsikia mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli, Mara kwa mara katika kampeni zake, akiwatisha wananchi wa maeneo hayo kuwa hataleta maendeleo, iwapo wananchi wa maeneo hayo watachagua wawakilishi toka vyama vya upinzani!
Nimekuwa nikifuatilia namna Tume ya Taifa ya uchaguzi namna ambavyo imekuwa ikionya kuwa wagombea hawatakiwi kuwabagua wananchi kwa jinsia yao, dini zao na itikadi zao za kisiasa, na wanaendelea kusisitiza kuwa mgombea yeyote ambaye atathibitika kuwa ametoa matamshi ya kibaguzi, basi Tume yao haitasita kumfuta mgombea huyo kuendelea kugombea kiti hicho
Sasa swali langu kwa Tume yetu ya uchaguzi, je hamjamsikia mgombea wa CCM, John Magufuli, namna anavyowatisha wananchi kuwa hataleta maendeleo kwenye maeneo ambayo wamechagua upinzani?
Jambo lingine ni je mgombea huyo wa CCM anaposema hataleta maendeleo kwenye maeneo watakayochagua wapinzani, je pia atasitisha kuwatoza kodi wananchi hao watakaochagua wapinzani?
Kwa kuwa inaeleweka wazi kuwa pesa inayoleta maendeleo sehemu mbalimbali nchini, hazitoki mifukoni mwake, mgombea huyo John Magufuli, Bali ni pesa ya walipa kodi wa nchi hii, bila kujali itikadi zao za kisiasa.
Swali kingine ninalomuuliza mgombea Urais wa CCM, je haoni kwa kuwatisha wananchi hao kutoleta maendeleo kwenye maeneo yao, anavunja Katiba ya nchi waziwazi, Katiba ambayo aliapa kuitii na kuiheshimu, kabla hatujamkabidhi wafhifa huo wa Urais wa Taifa hili?