Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
3,880
Reaction score
11,134
Wanabodi,

Kwa mujibu wa Rais Magufuli wametuma sample za mimea na wanyama kwa kuzipa majina ya binadamu kwenye maabara kuu ya Taifa Dar es Salaam kwa siri bila wapimaji kufahamu baada ya kupimwa zimetest positive yaani zina corona

Hapa ndipo Magufuli ameprove uwana-science wake.
Je? Tatizo ni vipimo tulivyonavyo au Tatizo ni utalaamu wa watu wa maabara
Je?Ni nani alituuzia hivyo vifaa

Kwa hiyo nchi za Marekani,China na ulaya ni waongo kwa idadi za vifo wanavyotutangazia na yale mazishi ni maigizo

Je? Ni wakati wa kuacha kula mbuzi,mapapai na vyote vilivyoonyesha Positive

Magufuli ameonyesha uwezo mkubwa na kushauri nchi zingine zijaribu kupima sample zingine za mimea na wanyama kwa kutumia vipimo vya corona.

Soma hapa > Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria - JamiiForums
 
Ameyasema hayo leo wakati wa kumuapisha Waziri wa Sheria na katiba kuwa vyombo vya usalama vilipenyeza sampuli kutoka kwenye mananasi, mafenesi, mbuzi, kondoo, nk kwa siri na kuzifanya ni za binadamu. Jambo la kushangaza matokeo ya baadhi ya sampuli hizo au yalionyesha yana maambukizi ya corona.

"...tunawasiliana na Madagascar na wamehaidi kututumia dawa inayotibu covid 19...." JPM
Mambo ni mengi ngoja niweke clip ya video!

Chanzo ITV....
 
Nashangaa anawalaumu waliokuwa wanapima kule maabara ya kitaifa kuwa wanamhujumu, kwa kutoa matokeo positive Ya corona, anadai kuwa walionekana ni positive ni uongo, eti alipeleka sample Ya Mbuzi, papai, na vitunguu eti wale watu Wa maaabara ya taifa walimuhujumu, eti na hizo sample hao wa maaabara Walisema ni positive aiseee anaone kuwa hakuna corona anasema hata ligi ya mpira atairuhusu iendelee aisee huyu mzeee akishindwa Jambo anasingizia mabeberu na kuwa anazungukwa, yani hahahahaha, Halafu nashangaaa anaenda anasema corona kweli ipo halafu anasema vipimo ni vya uongo watu waliokuwa wanapima wachunguzwe yani mmmmh simwelewi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli akimuapisha Mwigulu Nchemba alisema, kuna haja ya kuangalia Laboratory yetu inayopima Corona maana serikali ilifanya sample ya vipimo mbalimbali kutoka kwa Mbuzi, Kondop, Papai, Fenesi na Oil na majibu yakatoka tofauti tofauti.

Amesema matokeo ya vipimo vya Mbuzi ni positive - ana corona, Papai lina corona, na Fenesi pia huku kondoo na oil ikionekana 'unspecified"...

Amesema hao wataalam wa maabara ni ama wanatumika na Mabeberu, miundombinu ya maabara ni mibovu au hawana utaalam katika eneo hilo.

Amemwelekeza Mwigulu wakashirikiane kutatua jambo hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe akiongea maneno kumi unakuta moja tu ndio la kweli, angekuwa kama anavyosema corona ni ugonjwa mdogo angekuja zake dodoma aendelee kuchapa kazi.

Kwamba unapima mananasi wakati watu wanalalamika vipo havitoshi sababu maabara ni moja watu wapo Arusha wanatuma sumpuri Dar halafu wewe unaweka jam kupima mananasi!

Ni upumbavu, narudia tena ni upumbavu kuapisha waziri kwenye makazi binafsi ya Rais wakati Ikulu ipo Geita, Mwanza.

Taasisi ya urais sio mali ya mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom