Rais Magufuli: Msichague wanasiasa wanaohubiri chuki, vurugu zikitokea wao watakimbia kwenda kuishi kwingine

Rais Magufuli: Msichague wanasiasa wanaohubiri chuki, vurugu zikitokea wao watakimbia kwenda kuishi kwingine

Kilichotokea ktk chaguzi za serikali za mitaa nadiriki kusema kuwa uyu ndie mleta vurugu na mgawanyiko namba moja ktk hii nchi
Hapana shaka tuko pamoja rais wetu kipenzi cha wengi ,lazima umwadabishe yule jamaa aliyetoka ughaibuni akitaka kutuharibia amani ya nchi yetu halafu yeye atokomee tena atuache tukiomboleza,huyu tutamuadhibu kwa kipigo cha kenge.
 

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kutochagua wanasiasa wanaohubiri chuki na kutoa maneno ya vitisho.

Kiongozi huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 14 Agosti 2020, katika maadhimisho ya miaka 13 ya moto kwenye Mkutano Mkuu wa Kanisa la Assembly of God (TAG) jijini Dodoma.


Katika kusisitiza hilo, Rais Magufuli amesema “wanafanya hivyo kwa vile hawana sera za kuwaambia wananchi, lakini wanajua vurugu zikitokea wao wanapakwenda kuishi.”

Rais Magufuli amesema, serikali anayoiongoza itahakikisha kwamba uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, unakuwa huru na haki.

Pia amewataka viongozi wa dini kuhakikisha wanaliombea Taifa ambalo ni miongoni mwa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Pamoja na kuzungumzia masuala mbalimbali, Rais Magufuli amegusia suala la uchaguzi mkuu akisema, “uchaguzi ni zoezi muhimu katika kupata viongozi kwa njia ya kidemokrasia.”

Amewasihi viongozi wote wa dini nchini kutumia nafasi walizonazo kuhimiza waminini kushiriki katika uchaguzi huo utakaofanyika siku ambayo si ya kusali kwa wamumini wa dizi zote “siku hiyo itakuwa ya mapumziko.”

“Hatuna budi kumwomba Mwenyezi Mungu atupatie viongozi wenye maono, wachapa kazi na wazalendo kwa Taifa letu, tusiangukie mikononi mwa viongozi wabadhirifu, wabinafasi au vibaraka,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, kazi ya viongozi kama hao huwa ni kubomoa badala ya kujenga, kung’oa badala ya kupanda na kutawanya badala ya kukusanya “hivyo Mwenyezi Mungu atujalie hekima ili tufanye maamuzi yaliyo sahihi.”

Rais Magufuli amesema, katika baadhi ya nchi, wakati mwingine zoezi la uchaguzi imekuwa chanzo cha kuzuka kwa vurugu na fujo.

“Niwaombe viongozi wa dini kuliombea na kuliweka Taifa letu katika mikono ya Mungu ili tumalize salama uchaguzi na kubaki na amani, umoja na mshikamano kama taifa.”

“Kwangu mimi naliona Taifa la Tanzania muhimu zaidi kuliko mifarakano ya mambo mengine. Napenda kuwathibitishia kama Serikali nilivyoahidi hapo nyuma, tumejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu unakuwa huru na haki,” amesema na kuongeza:

“Sisi kama Watanzania tusimame kama Taifa moja, vyama visitugawe na dini zisitugawe na makabila yasitugawe, sisi tuishi. Nina imani viongozi wa dini wakisimama sisi tutavuka salama,” amesema Rais Magufuli.
Hivi Magufuli aliwahi kutoa tamko lolote kuhusu mauaji ya Binti Akwilina ?
 
Usimuamini muongo hata kama akiongea ukweli..

Tuna kiongozi wa hovyoo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kauli ya Rais kwa watu wanaojiteka na kujiumiza, kisa siasa!
Huo ni upotevu wa muda
Sugu leo kajiteka na kujitesa..... Alifungwa jela kwa amri kutoka juu na aliyemfunga akapandishwa cheo....

HONGERENI sn kwa huu uchumi wa kati
 
Hapana shaka tuko pamoja Rais wetu kipenzi cha wengi ,lazima umwadabishe yule jamaa aliyetoka ughaibuni akitaka kutuharibia amani ya nchi yetu halafu yeye atokomee tena atuache tukiomboleza,huyu tutamuadhibu kwa kipigo cha kenge.
Acha Uchochezi wewe
 
Nakumbuka ITV mwaka 1995 walikuwa wanaonyesha mauwaji ya Rwanda kila siku...Sasa wako wapi TZ itakuwepo hata Jiwe akiondoka
 
Hapana shaka tuko pamoja Rais wetu kipenzi cha wengi ,lazima umwadabishe yule jamaa aliyetoka ughaibuni akitaka kutuharibia amani ya nchi yetu halafu yeye atokomee tena atuache tukiomboleza,huyu tutamuadhibu kwa kipigo cha kenge.
Tena???
 
Mtaishi kama mashetani.!
Sikuleta Tetemo!
Sipangiwi ! Ukisema ndio umeharibu!

Hivi hilo koba la pesa linalobebwa zinatoka mfuko gani?? Hazina bajeti. WaTZ twaliwa mchana kweupeeh.!
 
Sifa zote alizozitaja anazo yeye, ni kweli tumepanga kutomchagua kutokana uovu wake mwingi tu.
 
Yeye ndio chanzo cha matatizo katika nchi hii kwa kuleta sera za chuki dhidi ya watu wenye mitizamo tofauti na yeye.

Wengine walipigwa risasi na anazuia uchunguzi usifanyike halafu anatudanganya eti anahubiri amani. Hatumtaki hata bure.
What a hypocrisy.
 
Jiwe hana aibu kabisa yaani nafiki balaa , linachoongea na kutenda tofauti kabisa mbingu na ardhi.
 
Angesema chagueni watu wanao wabagua watu kwa ukanda. Hawa ndio wangu walinipa kura usiwaguse. Nyie subirini kwanza. Pia wabomolee na nyumb zao bila fidia. Hawaku nipa kura. Ndie JPM huyo. Hakuja miaka mitano ni sawa na kesha la jana...
 
Watanzania wenzangu nawaomba tuwapige na kuwakataa watu wanaotaka kuvuruga amani yetu. Amani tuliyo nayo ni muhimu sana katika maendeleo ya Tanzania, kuna watu wenye nia ovu huku wakijificha kwenye mwavuli wa chama chao wakidai wanatafuta haki; haki gani mnayoitafuta?

Watanzania tunachotaka nimaendeleo na tayari tumempata Rais mwenye uchungu wakuleta maendeleo. Katika awamu ya kwanza ya miaka mitano ya Raisi Magufuli amefanya mengi mfano vituo vya afya kila kata, hospitali za wilaya, hospitali za kanda zimejengwa, umeme karibia vijiji vyote Tanzania vina umeme, miundo mbinu ya reli na barabara kila kona ya nchi yetu inajegwa, mikopo kwa wanafunza wa elimu ya juu imetolewa kwa kiasi kikubwa.

Nidhamu kazini kwa wafanyakazi, mishahara mwaka huu imeongezwa, ametimiza ndoto ya baba wataifa kuhamia Dodoma, Magufuli kaweza kuthibiti majizi ya Rasilimali zetu.

Nawaombeni Watanzani tuwakatae kwa nguvu zote hawa watu na hichi chama kinachotumiwa na mabeberu kuharibu Amani ya nchi yetu. Tumchague JPM kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
 
Back
Top Bottom