Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Mbona waliopotea na kurudi kumekuwa na ukakasi walikuwa wapi?Halafu jukumu la Ulinzi na usalama ni la wewe Amiri Jeshi Mkuu.Sasa kama hivyo vitendo havikomeshwi nani wa kulaumiwa kama sio wewe?
Ajawahi kemea popote.Atoe neno tu nao utakoma
 
Mheshimiwa Rais yupo sahihi naunga mkono
Hapana ndugu yangu; husimpe kicha! Rais amekosea sana kusema hivyo. Kuwapiga watu marufuku kutuhumu vyombo vya dola maana yake ni anajenga kinga kwa vyombo vya dola ambavyo vinaweza kuhusika na uhalifu.

Lakini ifahamike kuwa watu wanafikia kutuhumu vyombo hivyo kutokana na mtindo wao wa kukamata wahanga/washukiwa kwa mtindo wa "kimafya" (utekaji). Zaidi wanaoteka watu hujitambulisha kuwa wao ni watu wa usalama.

Nasema Rais amekosea kwa kuwatisha raia na badala yake kuvikinga vyombo vya dola. Ni muhimu kuelewa kuwa wahanga wa matukio ya utekaji ni raia wa kawaida bila kujali wanaoteka ni watu wa yombo vya dola au wahalifu.

Rais alitakiwa kwanza oneshe kuguswa na usalama wa raia wake kwa kukemea matukio haya na kuviwajibisha vyombo vya dola kutimiza wajibu wake wa kulinda usalama wa raia. Rais anatambua sana kutokea kwa matukio ya utekaji lakini amekuwa kimya bila kukemea.

Bila shaka Rais hayupo pale kutetea raia wanyonge bali kulinda vyombo vyake vya dola dhidi ya raia wa kawaida. Hafai!
 
Vyombo vyetu vimeshindwa haviwezi pambana na wasiojulikana wana nguvu kuliko dollars
 
Hata mkiwasilence hamuweziubadili ukweli
 
The Lost.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oya wanangu eeh, Safari hii mtanyoka haki ya Mungu, Kichaa kakabidhiwa Rungu..

Mi ndo yule Halfcast ya Kinyakyusa na Kichaga,

Mbeya City Stand up, Moshi Stand up...
 
Kisicho julikana ni kwamba baada ya sera zote kupokwa wenzenu wamepata pa kushika ni hatari kunyang'anya hata hii kwani wasipo tafuta huruma ya wananchi kupitia utekaji watakuwa hawana ajenda mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…