Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Kutisha watu sio suruhisho dawa hapa ni kutafuta Kwann usalama wa Taifa unahusishwa na maswala hayo ya utekaji?
una ushahidi kuwa Usalama wa taifa ndio wanahusika na utekaji? haya ndio Mh. Rais amesisitiza watu kama ninyi mchukuliwe hatua..

Hakika mnaudhi sana..
 
una ushahidi kuwa Usalama wa taifa ndio wanahusika na utekaji? haya ndio Mh. Rais amesisitiza watu kama ninyi mchukuliwe hatua..

Hakika mnaudhi sana..
Unapokaa kimya maovu yakiendelea kujirudia rudia ukiwa na uwezo wa kuyazuia unakwepa vipi lawama ya kuwa sehemu ya uovu
 
Ingekuwa ni utekaji unaowakumba na hao wenye machungu ya kuhisi wanasingiziwa ingekuwa sawa ila kwa sababu ni unidirectional wanayo haki ya kuendelea kuwasema ili waumie waache.
NB
Yule Zaccharia mkurya kama wangemuweza huenda angepotea ila kwa kuwa aliwabainisha waliona aibu na ku state clearly what they were and who was on the hunt.

Shame upon all those who deny the truth!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelekezo maalumu kwa mahakama kuhusiana na rufaa ya serikali kwenye kesi ya abdu nondo.
Abdu Nondo unakwenda jela mtaniambia
 
Hapo sawa kabisa maana vyombo vyetu vinachafuliwa hovyo
Nani wanapaswa kuvisafisha kama siyo wao wenyewe kwa kufanya kazi kwa weledi na siyo kwa maagizo ya watu fulani kwa maslahi yao?? Watanz sio wajinga.

Hapa naona dalili ya Watu fulani kupotea/kutoweka/kutekwa. Kwnini watu wafungwe midomo yao hivi sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo mengine tukisema ya kijinga hatueleweki! Yule mwenyekiti wa kule Kibondo wa CCM anaitwa Kangoye kama sikosei, alichukuliwa mchana na DSO na maofisa wake mchana na mpaka Leo hajaonekana anataka watu waseme kachukuliwa na Alshababu? Roma alitekwa na akaachiwa baada ya siku tatu na faili la uchunguzi hata kufunguliwa halikufunguliwa jee alienda kwa jimama na kupigwa huko?

Azory jee? Gari lililo mchukua limefahamika ni la serikali anataka watu waseme ni RENAMO ya Msumbiji?
Kule kwa Zakaria kama asinge washuti wale waliotaka kumchukua tungejua ni usalama? Na mbona hakushtakiwa kwa kushambulia bali kutakatisha fedha na uhujumu?

Mambo ni mengi sana awamu hii na yote yameweka uadui mkubwa kati ya hiyo taasisi yake na Watanzania makundi yote.
Ni hatari sana tukiingia ugomvi na adui wa nje maana hiyo taasisi itapataje ushirikiano toka kwa RAIA wasio wapenda ili kupata habari?

Wakati wa Amin, nakumbuka askari wetu walikuwa wanashangiliwa na RAIA wa Uganda hadi kupewa siri kwani serikali ya Amin ilikuwa inawafanyia raia wake uonevu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Magufuli ni miongoni mwa watekaji! na sasa hataki kusikia kelele za anao waumiza". Anacho fanya ni intimidations ili watu tukae kimya huku tukiona wenzetu wakipotea! Kuna matukio mengine ya wazi kabisa yanayo wahusisha usalama wa taifa, kama lile la Zakaria....yapo mengine yasiyo kuwa na majibu na mengine yenye majibu ya kitoto masikioni mwa wenye timamu.
 
Return Of Undertaker,
Mheshimiwa ameshagundua kuwa watanzania tunajua kila kitu kuhusu utekaji na utesaji. hivyo vyombo mbona vineshindwa kukamata hata mhalifu mmoja huu mwaka wa tano sasa.

Ni vyombo kweli au?.
 
Ni sawa kabisa, tena itungwe sheria Kali dhidi ya vyombo vya habari vinavyohusika kutoa taarifa za uzushi kama hizi ili Iwe mwisho wa upuuzi huu,mtu amekamatwa let's say na polisi mijitu inasema ametekwa,mtu yuko offline kwa matatizo ya mtandao wanadai ametekwa,hatuwezi kufika kwa kuendekeza upuuzi kama huu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpaka watu waone nini ndio waseme ametekwa? Kwa USA mtu asipoonekana masaa 48 bila kuonekana mazingira ya utatanishi ndio unaruhusiwa kufungua jalada missing person na polisi wanaanza kumtafuta!
 
Back
Top Bottom