Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

X-bar,
Kumbuka hii tabia ilishazoeleka vibaya na kuleta taharuki kwa jamii kuna baadhi ya watu wanafanya kwa malengo na kuchafua taswira ya vyombo vya ulinzi na usalama na taifa kwa ujumla.

Unakumbuka tuliambiwa CAG sijui kafanywa nini na mwanasiasa fulani? Na unakumbuka alichojibu mwenyewe CAG alivyohojiwa? Sasa watu dizaini hii wanaoleta taharuki zisizo na msingi wakiachwa inakuwa mazoea ujenga tabia mwishowe inakuwa tabia as usual.
 
Mama yako anaweza akaisaidia polisi kwa maelezo yake kama lini alikuona wewe mara ya mwisho? Ulivaa nguo gani? Uliondoka katika mazingira gani? Nakadhalika na kadhalika. Alafu wao wanaendelea zaidi mpaka upatikane au uachiwe huru na huyo lijimama wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ujinga wewe. Hivi huwa una umri gani? Naona leo hujaweka kibwagizo cha kuwa na ndugu Ujerumani.
Yaani kweli umri huu, una-assume watu bado tunaishi na mama zetu! Yaani mimi nipotezwe na hayo mashetani yenu halafu waende wakamuhoji mama yangu!
 
Hivi mtu anakamatwa na watu wanaojitambulisha kuwa ni polisi lakini hawataki kupita serikali ya mtaa, baadaye polisi wanakana kumkamata mtuhumiwa tajwa, baada ya siku mbili polisi wanakubali kumkamata na kumshikilia mtuhumiwa waliyemkana,

kwa alama za picha ina maanisha nini?

Wapo waliokamatwa baadaye wakaonekana, na wapo waliokamatwa kwa mtindo huo huo na hawajaonekana,

Je, unatofautishaje Wasiojulikana na Polisi?
 
Return Of Undertaker,
kesho wakija kwako kwanjia hiyo usije kusema umeonewa

-unajua kuna mambo mengine ndiyo unawapa watu kutumia njia hiyo kupoteza watu.
mfano mzuri sasa kesi za kuhujumu uchumi ndizo polisi wanazo bambika watu utakuwa umepata habari kuna polisi walivo naswa kubambika mtu na takukuru alafu kesho angekuwa amekamatwa ungekubali kuwa ilikuwa sahii.

-utekaji nyara wakukamata watu kwa mtindo huu hata uganda ulitumika sana kipindi cha idi amini.kumbuka kama mtu hana takiwa na jeshi la polisi kupelekewa shitaka na kwenda.

kufanya hivo ni mtindo kuwa umeshindwa kukubaliana unayo yakosea kwa wananchi wako.
ni kikosa mimi nifungulie kesi nije nikamatwe sio kunichukua kama kagashoki kisa nimekukosea.
kuna mda mwengine serekali utengeneza maadui au vikundi vitakavo wapinga wakijiona wao ni wema kumbe ndio walio taka yafike hapo.

kiufupi wasio julikana ni serekali mbona wanapo zidiwa na wananchi katika kutaka kufanya yao wanajitambulisha kwa kutumia nguvu.

tafakari tu.

nilikuwa na pitia usa ,iran,iraq na kwengine mitindo yao kwenye nayo eleza


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Lwakini akae akijua watu wengi wanapotea wanapatikana Vituo vya Polisi,

Kwanza mimi kuanzia Roma atekwe na kuambiwa atapatikana kabla ya siku fulani, nikatokwa kabisa na imani na hii Serikali,

Swali Dogo, kwanini wakosoaji wa Serikali Ndio wapotee, wapigwe Risasi, wawe Ndio wahujumu uchumi?

Yote kwa yote, Matamko ya Mabebetu yamemtisha, bado anataka misaada yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio nzurii ....shime watanzania tuungane tuwe wamoka kwelikweli kwenye hili....tufanye lolote lijalowezekana tuwe wapole kama huwa Na wakati huhohuo wakali kama nyoka...ukiona au kuhisi Kuna dalili Za utekaji tumia chochote kujeruhi au hata kuuwa ili kuokoana wenyewe kwa wenyewe
Kama ni hivyo nami nashauri watanzania tujihami na hao watekaji kwa kupiga yowe la majambazi ili hata kama ni vyombo vya usalama basi wakaendeleze utekaji peponi. Zakaria was very right to shoot them. Wananchi walitakiwa wawaponde mawe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom