Katika hili namuunga mkono Mh.Rais wa JMT Dr.John Pombe Magufuri.
Binafsi nilikutana na taarifa kama hii maeneo ya Mahina jijini Mwanza ambapo bwana mmoja kwa jina kapuni aliyetoweka nyumbani kwake usiku kwa kumuaga mkewe kuwa anaenda kununua vocha usiku wa saa tano baada ya kutoka safari.
Mkewe alimsubili pasipo kuona dalili ya kurejea nyumbani,siku ya pili alianza kumtafuta kwa kuuliza ndugu,jamaa na marafiki ambao walimshauri atoe taarifa ofisi ya serikali ya mtaa kwa ushauri na maelekezo mengine.
Cha kushangaza siku iliyofuata iligundulika kuwa jamaa siku aliyoondoka kutafuta vocha alikwenda kwa kimada wake na kufungiwa ndani kwa mahaba motomoto.