Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Kinachomsumbua rais wetu ni vyombo kutuhumiwa; siyo watu kupotea!
 
Ni kwanini wanaitwa wasiojulikana?

Majeshi ya Ulinzi na Usalama wao ndio wanatakiwa kutuhakikishia kuwa sio TISS kwa kukamata wale wote wasiojulikana ili jamii itokane na dhana hiyo.
Naunga mkono hoja
P
 
Hapo sawa kabisa maana vyombo vyetu vinachafuliwa hovyo

Mhe. Rais Magufuli anasikitisha sana kwa kauli kama hizi mie niziite ni za rejareja! Rais anaongea kwa mzaha au kuleta utani kwene serious issues za kitaifa!

Kuna Watanzania ndugu zetu mpaka leo hawajulikani wako hai au wametangulia mbele ya haki: Ben Saanane na Azory Gwanda. Je, hawa nao bado wako kwa vimada au waganga wa kienyeji?

Kuna cases kama kutekwa kwa Mo Dewji na mpaka kesho haijulikani nani walimteka Mo na Rais mwenyewe amewahi kuwaambia.Polisi kuwa.Watz sio Wajinga!

Lakini pia kuna kesi kama ya Kutekwa kwa mwana muziki Roma Mkatoliki bado walomteka "hawajulikani"!
Rais atuambie nani anafanya kazi hii haramu ya kuteka na kupoteza watu wasio na hatia? Na hata kama wana hatia kwanini sheria na taratibu za nji zisifuatwe!
 
Huko mbeleni Nina mashaka makubwa. Napata ukakasi kuandika.
Vyombo vyetu vya dola vina jukumu Hilo hasa polisi na Kama watashindwa Wana wajibu wa kuomba msaada kwa wakubwa wao.

Huwa natamani Sana kila raia wa tz apewe paja la kuku kujilinda ili kusaidiana na polisi wenye jukumu la kulinda raia na Mali zao.

Ingekuwa hivi kwangu kuvamiwa na majambazi na kuniteka wangeniteka nikiwa maiti maana sikubali
 
That devil has a devilish plan in his head, let us wait and c. Kuna mtu aliandika humu kwamba hilo lishetani Lina ugonjwa wa usonji.
 
Kwa mwendo huu wa kuwabeba wanausalama, raia wa kawaida tutajiju!
 
Kama ni hivyo nami nashauri watanzania tujihami na hao watekaji kwa kupiga yowe la majambazi ili hata kama ni vyombo vya usalama basi wakaendeleze utekaji peponi. Zakaria was very right to shoot them. Wananchi walitakiwa wawaponde mawe
Kwa wakurya nadhani watu siku hiyo mapanga hayakuwa karibu,wangekuwa nyama za buchani nadhani
 
Ubishi wetu tulionywa

Hivi karibuni, baada ya huu msamiati wa "deep state" kuibuka kwenye mitandao ya kijamii binafsi nimetafakari sana kuhusu maana yake kwa taifa letu kisiasa.

Tafakuri yangu ilipelekea kuamini kuwa "deep state" kweli imetuathiri kisiasa na kujenga nadharia kuwa pengine haya tunayoshuhudia sasa katika siasa na utawala wa nchi yetu yametokana na vyombo kutuchagulia viongozi wa kisiasa. Nadharia hii iliongezewa nguvu na makala moja niliyosoma mwaka 2016 ambapo mwandishi alidai kuwa ingawa tulichagua viongozi 2015 sasa tunatawaliwa na vyombo.

Huu mtazamo wa kuwaona wananchi maadui wa taifa lao siyo wa kawaida kwa wanasiasa waliochaguliwa; huo ni mtazamo wa vyombo ambao kazi yao huwa ni kutafuta watu wanaodhaniwa ni tishio kwa watawala na dola. Hali hii inaashiria kuwa uongozi wa nchi yetu umewekwa na kudhibitiwa na vyombo. Nadhani hili ndiyo chimbuko la watu kutekwa, kupotezwa, kushambuliwa na kufunguliwa mashtaka ya kesi za kuwapora uhuru wao.

Hata ulinzi wa rais wetu unaashiria kuwa vyombo vimeshika hatamu. Ulinzi mkali kwa rais wetu unatutisha hata sisi wananchi na sidhani kama hata yeye mwenyewe anaufurahia.
 
Back
Top Bottom