Rais Magufuli mtumbue Bosi wa TTCL anaihujumu kampuni

Mimi niko Kahama tena hapa Mjini..... Ila kupata Vocha tu TTCL ni mtihani..... Sasa unanishawishi vipi nitumie TTCL????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niko Kahama tena hapa Mjini..... Ila kupata Vocha tu TTCL ni mtihani..... Sasa unanishawishi vipi nitumie TTCL????

Sent using Jamii Forums mobile app

Nunua kwa TPESA, yaani weka hela kwenye mpesa yako kisha itume kwenye ttcl then nunua bando juu kwa juu. Vocha ndo tatizo lao kubwa ni vyema this time wasitoe gawio kwa rais, hilo gawio watengeneze vocha wazisambaze nchi nzima.
 
mie ndio nna hasira nao kabisa, juzi nimenunua bando la internet la buku sikutumia hata kb 1, yaani data roaming mpaka muda imeisha na bando lao wakasepa nalo
 
Mbona yeye Mganga anaihujumu nchi lakini tunamvumilia tu
 
Ndio ashndwe hata kuweka vocha za kutosha mtaani!?
Namba hazidanganyi,

Kindamba kaikuta TTCL mahututi mbapaka sasa inatoa gawio serikalini. Tatizo kuu lilikua ni mtaji na hakupewa,anafanya maboresho kutokana na mtaji mdogo uliopo,hata awekwe mwingine hataweza kufanya zaidi ya huyu Kindamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
niliomba uwakala wa TPesa....sasa ni mwakka mzima wanajichanganya...nimefuatilia mpaka nimenyoosha mikono...sijui wanakwama wapi hawa jamaa
tafuta uzi uliletwa na jamaa nani sijui wa buza huko alilalamika alitoka buza mpaka posta makao makuu ya ttcl kwa ajili ya kununua vocha ya 500 na akaambiwa zipo za 1000
kaka vocha za TTCl unaweza pata kupitia T.PESA, selcom point, mawakala wa CRDB, NMB,pia kupitia TIGO, AIRTEL, VODACOM, Mawakala wa Mobistock, Kagaconnect.siku hizi naona wanakampeni ya kuongeza mawakala wa kuuza vocha za kukwangua.
 

Attachments

  • ERDiQmPWAAEmC7V.jpg
    63.5 KB · Views: 2
Utamuonea bure. Anatakiwa kupeleka GAWIO kwa lazima hata kama hajatengeneza faida la atumbuliwe. Hayo maboresho atayafanyaje? Mumwambie na huyo mtumbuaji aweke SIASA mbali na biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TTCL haiwezi kushindana na kampuni binafsi, juzi nimewakuta sehemu ambayo kunamkusanyiko mkubwa wa watu wamekwenda kutangaza shirika na kuuza laini za simu cha ajabu sikuona hata wakitangaza gari inapita kimya kimya , hapo gari inatumia mafuta na wamelipwa night lakin hakuna hata laini moja iliyouzwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sijawahi kuona vocha yake hata barabarani tu ikipeperuka au kukanyagwa,vodacom .tigo wana wateja wengi ila hawajawahi kuridhika na soko,wanashindana haswa,wanatembea masokoni,stendi minadani na kila mahali kuhakikisha tu wanapata wateja wapya na kuwashika kwa vifurushi mbalimbali,TTCL sasa naikumbukaga nikiona vile vibanda vyao vilivyotelekezwaga,yaani imekuwa kama ya kuja kusimuliwa kwenye somo la historia,kwa ujumla shirika hili ni mali kale,lipelekwe makumbusho.Wameshindwa kunyanyuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…