SEHEMU YA PILI
Katika sehemu ya kwanza ya mjadala wetu, hatukupata nafasi ya kujadili kwa undani dhana ya ‘demokrasia’ na kuihusisha na dhana ya ‘uchumi’. Badala yake, tulijikita zaidi kujadili uhusiano baina ya ‘ukuaji wa uchumi na ushindani wa kisiasa’. Lakini kama tutakavyoona katika sehemu ya tatu ya mjadala wetu, hali imechangiwa zaidi na uhalisia kwamba kama dhana, ‘demokrasia’ na ‘vyama vyama vya siasa’, hizi ni dhana mbili tofauti na zinazojitegemea in ‘theory’. Lakini kabla ya kujadili hilo katika sehemu ya tatu, katika sehemu hii ya pili tutajadili kwanza uhusiano uliopo baina ya dhana za ‘demokrasia’ na ‘uchumi’.
Mjadala kuhusu aina ya uhusiano uliopo baina ya - “demokrasia na ukuaji wa uchumi” ni mjadala ambao umeendelea kuwepo kwa karne nyingi, hasa kuanzia enzi za mijadala mikali baina ya
wanafalsafa wakubwa duniani - Plato & Aristotle. Hadi leo mjadala unaendelea kuhoji juu ya mfumo sahihi wa utawala (demokrasia au autokrasia) ambao unaweza kuleta faida zaidi za kisiasa na kiuchumi kwa nchi/taifa. Hata hivyo, licha ya uwepo wa swali hili kwa karne nyingi, watafiti bado hawajafikia muafaka kwamba – mfumo wa ‘ki-demokrasia’ (in and of itself) unaleta faida zaidi kiuchumi kuliko mfumo wa ‘ki-autokrasia’.
Kwa kipindi kirefu watafiti mbalimbali wameendeleza juhudi zao kupata majibu kwa swali hili muhimu kupitia mbinu mbalimbali za kitafiti.
Kwa upande mmoja:
Zipo tafiti zinazo tegemea on – ‘cross-country comparisons’. Tafiti hizi zina hoji ‘umuhimu wa Demokrasia kwa ukuaji wa uchumi. Kwa mfano, kazi za watafiti - Sirowy & Inkeles 1990, Przeworski & Limongi 1993, Helliwell 1994, Barro 1996, Tavares & Wacziarg 2001.
Kwa upande mwingine:
Zipo tafiti za karibuni zaidi, ambazo zinategemea on
‘panel data’. Tafiti hizi zinalalia zaidi au zinaunga mkono nadharia (theory) kwamba kwa kiasi fulani, mfumo wa demokrasia una athari kwa ukuaji wa uchumi. Kwa mfano,kazi za watafiti - Rodrik & Wacziarg 2005, Papaioannuo & Siourounis 2008, Persson & Tabellini 2009, na Acemoglu 2014.
Kufuatia kumalizika kwa vita baridi duniani (Cold War), lakini hasa kufuatia kuangushwa kwa ukuta wa Berlin na kusambaratika kwa lililokuwa taifa la KISOVIETI (USSR), zilifanyika tafiti kubwa zilizolenga nchi zaidi ya arobaini (40) duniani. Nchi zilizolengwa kitafiti ni zile ambazo zilikumbwa na
wimbi la mageuzi ya demokrasia kufuatia kumalizika kwa vita vya baridi (cold war), katika kipindi cha miaka ya 1980s- 1990s. Tafiti hizi zinaonyesha kwamba nchi zilizopitia mabadiliko ya kidemokrasia zili ‘experience’ - ‘average annual per capita growth rate’ ya karibia 0.005%. Matokeo haya (kitafiti) yanaonyesha kwamba, kitakwimu (statistically), ukuaji wa uchumi baada ya wimbi husika ni mkubwa kuliko kipindi cha awali (kabla ya mageuzi ya kidemokrasia), japo kwa tofauti ndogo.
Kwa kutazama haraka haraka ni rahisi kuhitimisha kwamba Demokrasia ina athari chanya kwa ukuaji wa uchumi wa taifa. Lakini wapo watafiti ambao wamemua kulitafiti kwa kina zaidi suala hili kupata ushahidi juu ya mahusiano ‘chanya’ baina ya Demokrasia na ukuaji uchumi. Juhudi hizi za kitafiti zimebaini kwamba “endogeneity factors” zinaweza kuwa kazini kuelezea na kuonyesha uwepo wa uhusiano chanya. Hivyo kwa kuzingatia “endogeneity”, watafiti (kwa mfano O'Donnell 1973, Linz 1978, Cavarozzi 1992, Remmer 1993, Gasiorowski 1995, Haggard & Kaufmann 1995), wanajadili kwamba ‘msukosuko wa uchumi’ (economic crisis) ndio chanzo au sababu ya mageuzi mengi ya kidemokrasia.
Maana ya tifiti hizi (rejea hapo juu) ni kwamba -
lower & negative’ GDP growth rate kabla ya mageuzi ya kidemokrasia inaweza kuwa ni ishara kwamba mwenendo mbaya wa kiuchumi (‘poor economic performance’) ndani ya nchi husika ilisukuma au ilichochea kuanguka kwa mfumo/utawala wa ‘autokrasia’ au wa chama kimoja cha siasa. Kwa mfano, watafiti wanajadili kwa kina suala la mtikisiko uliotokana na kupaa kwa bei ya mafuta duniani (Oil shocks) miaka ya 1970s. Pia wanajadili kuongezeka kwa mikopo ya kutoka nchi tajiri duniani kwenda nchi maskini (international lending), na vile vile migogoro ya madeni katika nchi maskini (the debt crises in poor countries), pia kama ni chanzo au sababu ya wimbi la mabadiliko ya kidemokrasia katika nchi husika.
Tukirejea matokeo ya utafiti wa hapo juu (rejea utafiti wa nchi zaidi ya ‘40’ hapo juu), watafiti wanatuonyesha kwamba
uhusiano chanya uliopo baina ya ‘demokrasia’ na ‘ukuaji wa uchumi’ unaweza akisi/reflect kwamba aidha:
Demokrasia inasababisha uchumi kukua zaidi. Hii hoja pia leo inaungwa mkono na tafiti nyingi duniani; au:
Mgogoro wa kiuchumi unasababisha kuibuka kwa tawala za kidemokrasia. Hii hoja pia leo inaendelewa kujadiliwa kwa kina in ‘political science research circles); au:
Kwa kiasi au kiwango fulani, masuala yote mawili hapo juu.
Pamoja na ukweli kwamba kutenganisha hii ‘causality’ baina ya Demokrasia na ukuaji uchumi ni kazi nzito, watafiti wanahimiza juu ya muhimu wa kuendelea kutafiti na kutafuta uelewa zaidi juu ya athari ya kweli ya demokrasia kwa ukuaji wa uchumi.
Kufuatia wito huu, taasisi maarufu ya utafiti nchini Marekani inayojulikana kama – “
The Brookings Institute” imelenga kutegua kitendawili cha ‘endogeneity’ tulichokijadili awali.
Lengoni kuchunguza kwa kina zaidi nchi zilizopitia wimbo la mageuzi kufuatia kumalizika kwa vita baridi (old war) kama tulivyogusia awali. Utafiti wa ‘Brookings’ umetumia ‘methodology’ ya ‘survey’ inayojumuisha watafiti, wataalam na wanazuoni wa demokrasia zaidi ya mia moja na hamsini (150) kutoka taasisi na mataifa mbalimbali duniani. Swali muhimu la utafiti linalenga kubaini -
‘the underlying forces’ zilizopelekea ujio wa demokrasia katika nchi husika. Utafiti wa ‘Brookings Institute’ umegawanya mageuzi ya kidemokrasia katika makundi makuu mawili kama ifuatavyo:
KWANZA - Mageuzi ya kidemokrasia yanayo sababishwa na mgogoro wa kiuchumi. Hizi wanaziita “endogenous factors”.
PILI - Mageuzi ya kidemokrasia ambayo yapo ‘exogenous’. Exogeneous factors husika ni pamoja na kufariki au kuondoka madarakani kwa ‘autocratic president or leader’ wa nchi husika, lakini pia factors nyingine zinavyohusiana na
politics & institutions ndani ya nchi husika.
Matokeo ya Utafiti wa BROOKINGS INSTITUTE – ni kama ifuatavyo:
Kwenye kundi la kwanza
i.e endogenous factors:
- Utafiti wa Brookings Institute unaonyesha kwamba – demokrasia haisababishi ukuaji wa uchumi. Watafiti wanajadili kwamba jamii za kidemokrasia ambazo hazipo ‘contaminated’ (hazijachafuliwa) na ‘endogeneity concerns’ hazina athari kwa ukuaji wa uchumi. Watafiti wanaenda mbali zaidi kuonyesha kwamba, kitakwimu (STATISTICALLY), kasi ya ukuaji uchumi ‘kabla’ na ‘baada’ ya mageuzi ya kidemokrasia katika nchi hizi ni sawa.
Kwenye kundi la pili
i.e exogenous factors:
- Utafiti wa Brookings Institute unaonyesha kwamba athari za demokrasia kwa ukuaji wa uchumi zinaendeshwa na ‘endogenous democratizations’. Kwa maana nyingine – uhusiano chanya ambao umekuwa ukihusishwa baina ya ‘Demokrasia’ na ‘Ukuaji wa uchumi’ katika mataifa mbalimbali, uhusiano huu unaendeshwa zaidi au unatokana na makosa/mapungufu ya kitafiti kuhusisha ‘endogenous democratic transitions’ katika juhudi watafiti kukisia athari za mfumo wa utawala/kisiasa kwenye ‘performance’ ya uchumi wa nchi. Brookings institute wanahitimisha kwa kujadili kwamba tabia hii katika tafiti inaleta au inajenga picha isiyo sahihi kwamba - ‘demokrasia inasababisha ukuaji wa uchumi’.
Baada ya kuangalia uhusiano uliopo baina ya Demokrasia na Ukuaji wa Uchumi, sehemu inayofuata (sehemu ya tatu) inajadili uhusuano baina ya ‘Vyama Vya siasa na Demokrasia’.
SEHEMU YA TATU
Kwa ujumla wake hoja kwamba “Vyama vya Siasa ni NGUZO muhimu kwa Demokrasia” ni hoja inayokubalika sio tu miongoni mwa wanazuoni wengi, bali pia watunga sera (policy makers) mbalimbali wenye jukumu muhimu la kulea na kukuza demokrasia katika nchi mbalimbali duniani. Na hii sio tu katika changa kidemokrasia, bali pia hata katika nchi zenye Demokrasia iliyokomaa.
Mwaka 1942, mwanazuoni mmoja wa masuala ya siasa, “Elmer Schattschneider” alipata kutamka maneno yafuatayo:
[“The political parties created democracy, and modern democracy is unthinkable save in terms of the political parties”.]
Karne kadhaa zilizopita kipindi kile vyama vya siasa vinaibuka kwa mara ya kwanza katika mataifa ya Magharibi, jamii katika mataifa haya hayakuchukulia ‘vyama vya siasa’ kwamba vitu vya lazima, vitu muhimu, vitu visivyokwepeka au vitu vya kutamanisha. Katika dunia ya leo, ikiwa ni karibia karne mbili baadae, hali hii ni tofauti kwa maana ya kwamba – katika dunia ya leo, vyama vya siasa vinachukuliwa kama ndio ‘nguzo kuu’ na ‘mzizi’ wa demokrasia katika mataifa yote, yale yaliyokomaa kidemokrasia, lakini vile vile hata yale yenye demokrasia changa na yale yasiyo ya kidemokrasia. Kufuatia umuhimu huu, leo hii vyama vya siasa vinatazamwa kama
‘a sina qua non’ (an essential condition or absolutely necessary) for the arrangement of ‘modern democratic polity’ na pia ‘for the expression of political pluralism’.
Kwa ujumla wake, kuna muafaka miongoni mwa watafiti juu ya hili. Lakini licha ya muafaka husika, yapo baadhi ya maeneo mahususi ambayo bado hayana muafaka; eneo muhimu likiwa ni kuhusu – utendaji kazi (Performance) ya Vyama vya Siasa. Watafiti wengi wanajadli kwamba vyama vya siasa - kama TAASISI ZA KISIASA, vinazidi kutetereka. Kwa mfano, mtafiti Schmitter, (2001) anajadili kwamba – ‘Political Parties are not what they once were’. Schmitter anajadili kwa kuvipa vyama vya siasa sura kuu tatu kama ifuatavyo:
(i) Vehicles of representations.
(ii) Instruments of mobilization.
(iii) Channels of interest articulation and aggregation.
Pia yapo maeneo juu ya ‘performance’ ya vyama vya siasa ambayo wanazuoni wamefikia muafaka. Muafaka muhimu ni kwamba - vyama vya siasa vinaendelea kuwa na umuhimu mkubwa katika masuala makuu mawili:
i) Control over candidates recruitment.
ii) Organization of parliament and government.
Linapokuja suala la shughuli (functions) za vyama vyama vya siasa, watafiti wanazitenganisha maeneo makuu mawili:
Upande wa kwanza ni - ‘representative functions’.
Upande wa pili ni - “procedural and institutional functions”.
Utafiti wa Bartolini & Mair –[ “Challenges to contemporary political parties” (2001)], unaliangalia suala hili kwa undani zaidi. Watafiti hawa wanajadili kwamba - ingawa inawezekana kwamba ‘representative functions’ za vyama vya siasa inaendelea kudumaa na kutetereka, lakini the ‘procedural role’ ya vyama vya siasa sio tu bado ipo imara, bali pia inaweza kuwa inazidi kuimarika tofauti na kipindi cha nyuma. Bartolini & Mair wanajadili suala hili kwa sura ya ‘Paradox’, kwamba:
Kwa upande mmoja:
Pamoja na kwamba vyama vya siasa vinaendelea kuaminiwa kama taasisi muhimu/taasisi za lazima/taasisi zisizokwepeka katika kutumikia jukumu lake la
‘representative democracy’ (demokrasia wakilishi);
Kwa upande mwingine:
Vyama vya siasa pia vinaonekana kuendelea kupoteza uwezo wa kutimiza kikamilifu jukumu lake la ‘representative democracy’, jukumu ambalo watafiti wanajadili kwamba ni la muhimu sana kwa afya na utendaji kazi wa demokrasia katika vyama, jamii na taifa kwa ujumla.
Mtazamo huu unatoa ishara ya uwepo wa ‘incompatibility’ (kutoendana/kugongana/kupishana) baina ya mapendekezo makuu mawili yafuatayo:
Upande mmoja – Vyama vya siasa ni taasisi za lazima for
‘Representative Democracy’
Upande wa pili – Katika kutimiza jukumu muhimu la ‘representative democracy’, utendaji kazi au ‘performance’ ya vyama vya siasa katika utimizaji wa jukumu hili unazidi kudorora na kutetereka.
Suala hili lina – ‘reflect’muendelezo wa mabadiliko ya kifikra na kimtazamo katika dunia ya leo, juu ya ‘vyama vya siasa’, kama ‘dhana’, kwa maana ya– political parties as a ‘concept’.
Sehemu inayofuata tutajadili kwa undani juu ya ‘Vyama vya siasa’ vya awali (karne ya kumi na tisa).
Vyama Vya Siasa vya Awali:
Kipindi kile (karne ya kumi na tisa/19th Century) wakati vyama vya Siasa vilipokuwa vinazaliwa kwa mara ya kwanza barani ulaya, vyama husika vilianza kama ‘Voluntary Associations’ (kujitolea au hiyari). Kwa maana nyingine, leo hii ambapo - uelewa, imani na mtazamo juu ya vyama vya siasa kwamba - ni taasisi muhimu, taasisi za lazima na taasisi zisizokwepeka kwa ajili ya kuhudumia ‘demokrasia’, imani, uelewa na mtazamo huu haukuwepo kipindi kile vyama vya siasa vinazaliwa/ibuka kwa mara ya kwanza duniani.
Vyama vya siasa kama dhana ilizaliwa peke yake, kabla hata dhana ya demokrasia haijaibuka. Udugu na uhusiano tunao uona leo hii baina ya dhana ya ‘vyama vya siasa’ na dhana ya ‘demokrasia’, uliojitokeza na kuja kujengwa baadae sana. Kupitia utafiti wake Van Biesen, (2004) – [“Political parties as public utilities”], analisema hili kwa maneno kwamba:
“Matukio ya hivi karibuni katika anga ya demokrasia nchi za ulaya kusini na ulaya mashariki ya kuvipatia vyama vya siasa ‘previledge position in legal and constitutional terms’…, ambapo serikali imekuwa ni sehemu kubwa ya maamuzi juu ya ruzuku za vyama pamoja na udhibiti wa shughuli ya vyama, yote haya ni
masuala mapya katika muktadha wa demokrasia ya kiliberali”.
Hii ndio sababu ya msingi kwanini ndani ya ‘literature’ juu ya ‘Democracy Theory, lipo jambo moja la kustaajabisha kidogo. Jambo hilo ni kwamba –
‘Democracy Theory’ inazungumzia vyama vya siasa kwa juu juu sana; Isitoshe, ndani ya ‘literature’ juu ya ‘democratic theory’,
vyama vya siasa vinatazamwa au vinaangaliwa kama obstacle (kizuizi) kwa ‘demokrasia’. Kwa maana nyingine:
Pamoja na kwamba leo hii dhana mbili muhimu – dhana ya ‘Vyama vya Siasa’ na dhana ya ‘Demokrasia’ zinatazamwa na kuchukuliwa kama ni vitu vinavyotegemeana na visivyoweza tenganishwa, ‘literature' juu ya ‘democracy theory’ na literature juu ya ‘political parties’, zimeendelea kufuata njia.
Mwanazuoni Bryce (1921) - [‘Modern Democracies’], anajadili hili kwamba – “hakuna mtu aliyeweza kuonyesha jinsi gani ‘representative government’ inaweza kufanya kazi”.
Pamoja na uwepo wa muafaka miongoni mwa watafiti kuhusu ‘performance’ ya vyama vya siasa, yapo baadhi ya maeneo ambayo wana tofauti kubwa kimtazamo, hasa kuhusiana na maana ya dhana ya ‘D
emokrasia’, na
nafasi ya Vyama vya Siasa katika Demokrasia.
Wanazuoni wengi wamekuwa wakihoji the ‘value’ (thamani) ya demokrasia na jinsi gani demokrasia inapaswa kufanya kazi. Kama tulivyoona awali, kinachosukuma baadhi ya wanazuoni kuhoji hili ni kutokana na kukatishwa tamaa juu ya jinsi gani ‘perfornance’ ya vyama vya siasa imeendelea kuzorota. Mbali ya hili, katika mataifa mbalimbali yanayofuata na kutekeleza mfumo wa ‘Demokrasia ya Vyama’, matukio yafuyatayo yamekuwa yakijitokeza:
- Ongezeko kubwa la wananchi wanaojitenga/punguza ushiriki/interest juu ya masuala ya Siasa za Vyama;
Ongezeko kubwa la Wananchi wasioridhishwa na ‘performance’ ya vyama vya siasa;
Kasi kubwa ya wananchi kupunguza imani zao kwa viongozi/wanasiasa; na pia
Suala la kudhoofika kwa ‘representational and governmental roles ya vyama vya siasa, hasa kutokana na matatizo yanayohusiana na
accountability, responsiveness and legitimacy.
Kufikia hapa tunaweza hitimisha kwamba:
Iwapo kuna ukweli kwamba ‘representative democracy’ inahitaji uwepo wa vyama vya siasa huku vyama vya siasa vikiendelea kupoteza uwezo wa kufanya kazi kama mawakala wa uwakilishi (‘agents of representation’), basi ni dhahiri kuwa hali hili ina athari kubwa ‘for the nature of democracy’. Njia pekee ‘to address this fundamental tension’ baina ya - kwa upande mmoja -
umuhimu wa vyama vya siasa na kwa upande mwingine -
kuendelea kutetereka kwa uwezo wa vyama vya siasa kufanya kazi zake katika ‘modern democracy’, ni kuangalia kwa undani ‘theories of democracy’. Kwa kufanya hivyo, tutapata mwanga na uelewa zaidi juu ya nafasi ya vyama vya siasa, hasa ‘in contemporary democracy’.
Tunajadili hilo katika sehemu inayofuata.
Lakini kabla hatujaendelea ni muhimu tukasisitiza mambo matatu yafuatayo:
Kwanza - Chama kama taasisi ya kisiasa ni dhana ngeni. Dhana za -
‘Chama cha siasa’ na
‘demokrasia’, hizi dhana mbili hazikuzaliwa pamoja siku moja. Badala yake, zilizaliwa katika nyakazi tofauti, huku ‘theory’ ya kila mmoja iki – ‘grow’ na kuendelea kwa kujitegemea.
Pili - Kipindi kile vyama vya siasa vya awali vinazaliwa na kuibuka kwa mara ya kwanza duniani (miaka ya 1800s), jamii husika hazikuvipokea vyama vya siasa kama ni taasisi za lazima au taasisi zinazohitajika, au taasisi zisizokwepeka au taasisi zinazotamainisha uwepo wake. Sana sana wakati vyama vya siasa vinaibuka kwa mara ya kwanza kule mataifa ya magharibi, vyama hivi vilionekana kama ‘threat to general interest’, kwani vilifunika interests of ‘individual’.
Tatu, na muhimu ni kwamba - kimsingi, uwepo au ujio wa vyama vya siasa sio tu ulionekana ‘incompatible’ (kwa maana yakutoendana/kugongana/kupishana) na ‘R
adical Democratic Tradition’ - ‘inspired’ na
Jean Jacques Rousseau, lakini vile vile
‘Liberal Democratic Tradition’ - inspired na
John Locke. Tangia kipindi hicho, imeendelea kuwa vigumu kuoanisha Falsafa hizi mbili (falsafa za Rousseau na Locke) na ‘taasisi za kisiasa’ (partisan institutions). Sababu kubwa ni kama tulivyogusia awali kwamba – vyama kama ‘taasisi za kisiasa’ sio tu kwamba zinafukia ‘individual interests’ ndani ya jamii, lakini pia uwepo wa ‘taasisi za kisiasa’ unapingana/unagongana/inapishana na ‘volonte generale’ (will of the people as a whole).
Ni muhimu tukaangalia kidogo falsafa za
Jean Jacques Rousseau na
John Locke zinasimamia mambo gani.
Jean Jacques Rousseau aliishi katika kipindi cha (1712 – 1778).
Historia juu ya Rousseau ina sura mbili. Rousseau anapongezwa lakini pia analaumiwa kwa kuchochea
mapinduzi ya ufaransa ya mwaka 1789 – 1799. Pamoja na mengineyo, Mapinduzi haya Ufaransa yalipelekea kutokomezwa kwa utawala wa kifalme nchini Ufaransa na kupisha muundo mpya wa utawala kupitia Katiba ya ‘Jamhuri’ (Republic)’. Utawala wa aina hii unasimamia nguzo muhimu kama vile:
-Usawa
-Uhuru
-Haki ya wananchi kupiga kura nk.
Katika dunia ya leo nchi nyingi duniani zinafuata mfumo na muundo huu wa utawala – kwa maana ya-
‘Jamhuri’.
John Locke aliishi katika kipindi cha (1632 – 1704)
Kimsingi, falsafa John Locke ilihusishwa na imani kwamba – serikali zina wajibu mkubwa wa kutumikia wananchi na kulinda maisha, uhuru na mali zao. John Locke pia ‘advocated’ kupunguza nguvu za serikali katika jamii
(rejea suala la ‘state vis a vis society’), na vilevile aliunga mkono ‘representative government & rule of law’.
Kufikia hapa, swali linalofuata ni - kama hali ndio hivi, je:
UHUSIANO BAINA YA VYAMA VYA SIASA NA DEMOKRASIA ULIJENGWA NA KITU GANI?
Uhusiano baina ya dhana ya ‘chama cha siasa’ na ile ya ‘demokrasia’ ulianza kujengwa kufuatia kuibuka kwa mahitaji ya ‘Mass Democracy’ (Demokrasia Ya Umma) katika nchi ulaya magharibi kipindi cha nyuma. Ndani ya jamii hizi uhusiano baina ya
‘the state’ and ‘individual citizens’ uliendelea kudhoofika na kuacha pengo kubwa. Kuibuka kwa mahitaji ya ‘Mass Democracy’ kulifanya uhusiano wa moja kwa moja (‘direct connection’) baina ya ‘state na ‘raia’ kuwa mgumu zaidi. Katika sintofahamu hii, vyama vya siasa vikaonekana kuleta suluhisho. Kwa mara ya kwanza, VYAMA VYA SIASA ‘vikahalishwa’ rasmi kuwa
taasisi kiungo (‘intermediary institutions’) baina ya
‘raia mmoja mmoja na serikali’ (state).
Awali tuliona kwamba kipindi kile ‘democratic theory’ ilipokuwa inaibuka kwa mara ya kwanza, ‘democracy theory’ ilivitazama Vyama vya siasa kama kizuizi (obstacles) vya demokrasia. Lakini kama tutakavyoona baadae, KIMSINGI, reflections za wanazuoni mbalimbali juu ya vyama vya siasa vya awali (miaka ya 1800s), hazikuwa zinapinga uhalali wa demokrasia ya vyama vya siasa (‘democratic legitimacy’). Badala yake, wasiwasi miongoni mwa wanazuoni wengi ulikuwa ni juu ya
ukosefu wa demokrasia ndani ya vyama vya siasa, hasa juu mienendo inayominya demokrasia ndani ya vyama, pamoja na mienendo iliyoendekeza na kujenga mifumo ya oligachia (‘oligarchy systems)’. Maana rahisi ya neno “Oligarchy” ni -
Kikundi cha watu wachache kuhodhi madaraka ya chama, hasa ndani ya vyama vya umma au ‘Mass Political Parties’. Tutatizama hili kwa undani baadae kidogo.
Moja ya tafiti kubwa zilizofanyika juu ya suala hili ni pamoja na ule uliofanywa na Mwanazuoni ‘Mosei Ostrogorski’ (1902) – [
“Democracy and Organization of Political Parties”[. Utafiti wa Ostrogorski uliangazia zaidi vyama vya siasa vilivyokuwepo katika nchi za
Marekani ya kaskazini (North America) na Uingereza. Ostrogorski anajadili kwamba - ‘organized political parties’ viliibuka ili kuhudumia mahitaji ya demokrasia ya umma (mass democracy). Ostrogorski anaongeza na kuonya kwamba -
‘party organization in itself is harmful’. Onyo la Ostrogorski lilikuja ‘dominate’ fikra na mitazamo juu vyama vya siasa na Demokrasia kuelekea karne ya ishirini.
Katika utafiti wake, Ostrogorski anakubali kwamba ndani ya jamii ya kidemokrasia, vyama vya siasa vilifanikiwa kuhakikisha usimamizi na utendaji mzuri wa kazi za kila siku wa Serikali. Ostrogorski anasisitiza kwamba, tofauti na kipindi cha awali, mafanikio ya vyama vya siasa juu ya usimamizi na utendaji mzuri wa kazi wa serikali yalikuwa yakiongezeka siku hadi siku. Lakini licha ya mafanikio hayo, Ostrogorski bado hakuwa na matumaini au imani na vyama vya siasa kwa asilimia mia moja.
Ostrogorski anajadili hilo kwamba – pamoja na mazuri yake, vyama vya siasa vilishindwa kusimamia nguvu za raia ipasavyo (upholding power of citizen). Kwa maana nyingine, sambamba na kufaninikiwa
‘in their procedural and institutional roles’, Ostrogorski anasema kwamba vyama vya siasa vilifeli
‘in their representational functions’. Anatoa sababu za kufeli huko kwamba; nayo ni kwamba – ‘party organization’ inafifisha ‘individuality’ na kupelekea ‘individual autonomy’ kutoweka. Ostrogorski anaongeza kwamba – ‘Party organization’
inafuta ‘the individual’ na badala yake inajenga
‘loyalty’ (uaminifu) kwa chama na falsafa zake. Anaongeza kwamba - hali hii ina athari kubwa, hasa - kufuta uhuru wa mawazo, individual initiative and political conscience.
Ostrogorski anakuja na pendekezo la kutatua hali hii. Nalo ni kwamba – ipo haja ya kutengeneza “a polity” isiyokuwa na
vyama vya siasa vya kudumu. Badala ya uwepo wa vyama vya siasa vya kudumu, Ostrogorski anapendekeza viwepo vyama vya muda au vya kipindi kifupi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zilizopo katika wakati husika; mara tu baada ya changamoto husika kupatiwa ufumbuzi au malengo husika kufikiwa, vyama vya siasa ‘as a party organizations’ zivunjwe. Ostrogorski anasema – kwa njia hii, uaminifu (loyalty) wowote kwa chama cha siasa unakuwa sio wa kudumu au unakuwa ni uaminifu wenye kikomo.
Kufuatia mapendekezo haya, baadae walijitokeza watafiti wengine walio-hoji na kujadili “practicality” ya nadharia (‘theory’) ya Ostrogorski’. Wanazuoni hawa ni pamoja na:
Katz (1997) – “Democracy and Elections”; Raney (1962) – “The doctrine of responsible party government: Its origin and present state”; na
Robert Michels (1962) – “Political Parties: A Sociological Study of the Oligarchical Tendencies of Modern Democracies.
Robert Michels (1962) alikuwa ni mwanafunzi juu ya uzoefu wa ujamaa wa kiitaliano na kijerumani (German and Italy Socialist experience). Sehemu kubwa ya utafiti wake ilikuwa ‘influenced’ na utafiti wa awali wa mtafiti ‘Cassineli’ (1953) – [“The Law of Oligarchy”]. Ushawishi wa Cassineli unatokana na mijadala yake kama vile:
[“The nature of any organization is such that leadership activities are free from control and can never be fully held accountable by those who hold subsidiary positions in the organization”.]
Hoja ya msingi kutoka kwa Cassineli ni kwamba:
Kwa jinsi jamii inavyozidi kukua/kuendelea, ndivyo inavyozidi kuwa ‘complex’; na katika ‘complex societies and mass democracy’, organizations ni kitu kisicho kwepeka; na kwa jinsi hizi organizations zinavyozidi kukua (experience growth) na kufikia ukubwa wa kaisi fulani na kuanza kuwa ‘complex’, hali hii inazalisha viongozi wanao tengeneza wafuasi; na baadae viongozi husika wanakuja kuwa ‘dominate’ wafuasi husika; hii hali inapelekea athari au madhara yasiyotarajiwa, madhara hayo ni
“oligarchization’’, kwa maana ya - kuzaliwa au kuibuka kwa kundi dogo la watu wachache linalo hodhi madaraka na mamlaka.
Cassineli anaendelea kusema kwamba oligarchanization ni matokeo ya mechanisms mbili:
Technical mechanisms.
Psychological mechanisms.
Anasisitiza kwamba ‘technical’ mechanisms ni muhimu zaidi, kwa vile inahusisha specialization, division of labor, & technical abilities za viongozi wa organizations husika.
Ni kupitia kazi hii ya Cassineli, Robert Michels (1962) baadae akaja na utafiti wake ulioasisi
‘Iron law of Oligarchy’; Theory ya Robert Michels (1962) inasema kwamba:
‘Oligarchy or rule by elite is inevitable as an "iron law" within any democratic organization as part of the "tactical and technical necessities" of organization’.
Msingi wa hoja ya Michels hapa ni kwamba – ‘power of the elites rests upon its organizational abilities’. Anasisitiza kwamba kila organization inazalisha ‘elites’ wake, na kwamba utendaji wa kazi katika hili unakaribiana na ‘law of nature’. Kwa mujibu wa Michels:
“It is organizations that give birth to the
domination of the elected over the electors, of the
mandatories over the mandators, of the
delegates over the delegators. Who says organization says oligarchy”.
Msisitizo wa Michels ni pamoja na kwamba - katika kila ‘organization’, the issue of ‘leadership’ is unavoidable; it becomes a necessity.
Katika utafiti wake juu ya vyama vya kijamaa na vyama vya wafanyakazi, hasa chama cha kijamaa nchini Ujerumani, Michels (1962) anadhihirisha matokeo ya utafiti wa Casinneli (1953). Akitumia chama cha Kijamaa cha Ujerumani kama ‘case study’, Michels anaonyesha kwamba hata ‘party organizations’ zikiwa na mfumo na utaratibu wenye kusimamia na kutekeleza ‘demokrasia ya ndani’, bado mwisho wa siku vyama hivi haviwezi kuzuia kuja kuwa
‘dominated & controlled by big unaccountable elite’. Kwa maana nyingine - ‘iron law’ must apply kwa vyama vyote vya siasa bila kujalisha kama vyama husika vina vinafuata/vinatekeleza au havifuati/havitekelezi demokrasia ya ndani ya vyama.
Mtafiti Michels (1962) anaongezea suala muhimu pia kwamba – ‘iron law’ ni ‘valid & relevant’ sio tu kwa ‘political organizations’, bali ni pia - to any large and complex organizations, hata nje ya masuala ya kisiasa.
Nadharia (theory) ya Michels (1062) inaweza kufanya mtu akahitimisha kwamba - Michels ana halalisha ukiukwaji wa kanuni na taratibu za demokrasia ndani ya vyama vya siasa. Lakini hatupaswi kujiingiza kwenye huo mjadala, angalau kwa sasa. Katika mjadala wetu, suala tunalopaswa kuzingatia hapa ni kutambua umuhimu/relevance ya utafiti wa Robert Michels katika juhudi zetu za kuendelea kutafuta majibu kwa maswali muhimu mbele yetu, kwa mfano, Je:
- Vyama vya siasa ni vizuizi vya Demokrasia?
Kupitia utafiti wake, Robert Michels hatupatii jibu la moja kwa moja kwa swali hili. Tunachopaswa kuelewa, hivyo kuwa hitimisho muhimu kwetu hapa ni kwamba - iwapo ‘internal’ party democracy/demokrasia ya ndani ya chama cha siasa - ‘is
a pre-condition’ ya ufanikishaji wa demokrasia katika taifa, au iwapo ‘iron law of oligarchy’ ni muhimu kwa – ‘the organization of the state’ (serikali), basi mapendekezo ya Michels ni kwamba – tunapaswa kuwa ‘pessimistic’(kuangalia kwa mashaka) juu ya uwezekano wa ‘ultimate realization of democracy’ katika taifa – yani, uwezekano wa nchi/taifa kufanikisha au kutekeleza bila mapugufu dhana ya demokrasia.
Tunamalizia sehemu ya tatu ya mjadala wetu kwa kuangalia utafiti wa mwanazuoni mwingine maarufu na mwenye ushawishi mkubwa katika massuala ya demokrasia na vyama, mwanazuoni Max Webber.
Max Webber anajulikana kwa mchango wake mkubwa katika eneo hili. Kwa mfano, utafiti wake: “Politics as a vocation” (1918), anajadili kwamba – vyama vya siasa vya awali viliundwa kwa lengo la kutumikia matamanio na matakwa ya makundi ya watu mashuhuri katika jamii (elites). Anaendelea kusema kwamba kilicho pelekea kuibuka kwa aina mpya ya vyama vya siasa, kwa maana yavyama vyenye ‘strong & permanent organization’ ilikuwa ni ujio wa ‘mass democracy’(demokrasia ya umma). Anaongeza kwamba aina hii mpya ya vyama vya siasa ndio iliyokuja kujenga na kuimarisha - the
‘psychology of followers’ & ‘charismatic authority of party leader’, na baadae byama hivi kuja kuwa ‘dominated with
a political elite or single leader’.
Webber anatumia historia ya vyama vya siasa nchini Uingereza kama nguzo muhimu ya utafiti wake, na kama tulivyokwisha ona anajadili kwamba - awali, vyama vya siasa viliundwa kwa kusudio la kukidhi maslahi ya watu wachache, ambao anawaita – ‘the notables in the society’, vikiwa na sura na mfumo wa ‘ki - aristokrasia’ (sio ki - demokrasia). Webber anajenga hoja kwamba – ‘originally’, vyama vya siasa kama ‘organized permanent associations’ havikuwepo; badala yake vyama hivi vilikuwa ‘active’ katika vipindi vya chaguzi tu. Anaendeleo kujadili kwamba, mshikamano ndani ya vyama vya siasa ulijengwa kwenye ngazi ya ‘parliamentary delegates’, huku kazi au shughuli za ‘delegates’ husika zikiishia kwenye makao makuu ya chama pekee kwa sababy hawa hawakuwa wanafanya kazi kwa wananchi kama ilivyo zoeleka chini ya mfumo wa kibunge ndani ya demokrasia za leo. Kwa mujibu wa Webber - siasa kama - ‘a profession’ ya kulipwa mshahara na posho, haikuwepo:
“Politics was formally and by far, predominantly an avocation – hobby, not a career”.
Hadi hapa tunajifunza jambo muhimu, nalo ni kwamba - ‘democratization of the franchise’kwa maana ya haki za wananchi kupiga kura au kuchagua au kuchaguliwa, halikuwepo awali wakati vyama vya siasa vinazaliwa kwa mara ya kwanza. Badala yake, ‘democratization of the franchise’ ni matokeo ya ‘modern systems of political organizations’. Katika dunia tunayoishi leo, vyama vya siasa pamoja na mifumo yake ni matokeo ya mambo makuu manne:
-Demokrasia.
-Mass franchise.
-Umuhimu wa kuhamasisha na ku-organize umma.
-Ujenzi wa dhana za dira, mshikamano na nidhamu ndani ya vyama kama taasisi za kisiasa.
Masuala haya ndio yaliyopelekea mabadiliko ambapo ukaibuka UMUHIMU WA WANASIASA KAMA FANI (‘Professional
Politicians’) katika siasa za vyama.
Kwa maana nyingine, ni katika muktadha huo ndio ‘professional politicians’ – kwa maana ya wanasiasa nje ya BUNGE ndipo wanapojitokeza. Wanasiasa hawa huwa ni watumishi wa moja kwa moja wa chama, wakifanya shughuli zao kwenye makao makuu ya vyama husika vya siasa. Kwa kawaida, ‘professional politicians’take control of the party organization; Nguvu ya chama inakuwa mikononi mwao kama watumishi wa kila siku wa chama; Majukumu muhimu ya hawa professional politicians ni pamoja nay ale ya kuandaa na kutoa DIRA na MIONGOZO ya chama‘as an organization’; Pia wanajukumu kubwa ‘
to keep parliamentarians in check’.
Max Webber, kupitia utafiti wake juu ya uzoefu wa siasa za vyama nchini Uingereza, analijadili hili kwamba:
[…matokeo yake ikawa ni nguvu ya chama cha siasa kuhodhiwa au kuwa mikononi mwa watu wachache, na hatimaye mikononi mwa kiongozi mmoja wa chama, huku ‘party machinery’ ikigeuka kuwa ‘oriented to the charismatic personality of the leader’. Ndani ya mfumo huu, kiongozi wa chama anachukua ‘nafasi maalum’, kwani sasa ni yeye ambae chama kama taasisi ndio kinamfuata].
Webber anaongeza kwamba:
[…ujenzi hivi vitu tunavyoviita au tulivyovizoea kama ‘vyama vya siasa’ hupelekea kuibuka kwa
‘plebiscitarian democracy’. Maana rahisi ya dhana hii ya ‘plebiscitarian democracy’ ni mfumo ambao – chama kinachagua kiongozi wake; na mara tu kiongozi husika anapochaguliwa, anakuwa na nguvu kubwa na kauli ya mwisho ndani ya chama husika cha siasa. Hali hii inapelekea bunge kubakia kama ‘rubber stamp’ au kwa maneno ya Webber:
“Parliamentarians are reduced to nothing better than well-disciplined YES MEN”.
Webber anahitimisha kwamba:
“The Plebiscitarian dictator actually stands above parliament…..; by bringing the masses behind the leader by means of the party machine, a state of affairs has been created which one might call – a dictatorship resting on the exploitation of mass emotionality.”
Ukimsoma Max Webber kwa haraka haraka ni rahisi sana kumtafsiri vibaya (‘negatively’), hasa juu ya uhusiano uliopo baina ya ‘uongozi wa kisiasa’ (political leadership) na demokrasia (democracy). Lakini kama tutakavyoona punde, kumsoma Webber kwa umakini zaidi, kunatoa tafsiri chanya.
Awali tulijadili tafiti za ‘Ostrorgosrki’ na ‘Michels’. Watafiti hawa walituonyesha kwamba – ukosefu wa demokrasia ndani ya vyama undermines (una athari) kwa mfumo wa demokrasia katika jamii nzima. Tukirudi kwenye Max Webber (utafiti ambao baadae ulikuja kuendelezwa na ‘Joseph Schumpeter’), Webber anapendekeza kwamba – ‘
strong and responsible leadership is a necessity for the healthy and functioning democracy’. Sababu ya msingi hapa ni kwamba – by ‘virtue of its organizational abilities, bureaucracy inaweza ‘obtain predominant political position’ na kuwa ‘the defacto ruling group’ isiyowajibika kwa umma. Hivyo basi ‘responsible and principled leaders’ wa vyama vya siasa wanahitajika ‘to keep bureaucratic leaders in check’, na kuhakikisha kwamba ‘they take care of impartial administration and don’t engage in politics’.
Mujumuhisho ya sehemu ya TATU
Tumepitia baadhi ya most influential reflections juu ya vyama vya siasa vya awali, vilivyoibuka mwanzoni mwa karne ya ishirini (miaka ya1900). Kwa ujumla wake tumeona jinsi gani watafiti mbalimbali wametuonyesha concerns (hofu/wasiwasi) zao juu ya ‘performance’ ya vyama vya siasa, hasa - ukosefu wa demokrasia ndani ya vyama na uwajibikaji (accountability), ingawa tafsiri za watafiti kuhusu athari za haya mapungufu kwenye demokrasia zinapishana.
Mtafiti Ostrorgorski anaamini kwamba vyama vya siasa vya kudumu ni ‘harmful’, hivyo havipaswi kuwepo. Watafiti waliomfuatia baadae wanakuja na mtazamo tofauti. Wanajenga hoja kwamba - ‘vyama’ kama taasisi za kisiasa, hasa katika muktadha wa ‘mass democracy’, ni muhimu na vinapaswa kuwepo.
Tumeona kwamba kipindi cha awali wakati vyama vya siasa vilipokuwa vinazaliwa au vinaibuka kwa mara kwanza duniani, vyama hivi havikupokewa na jamii kama ni vya lazima au visivyokwepeka (inevitable), au jambo la kutamanisha (desirable). Jambo lililo sababisha vyama vya siasa kuanza kukubalika kwenye jamii ilikuwa ni ujio wa ‘mass democracy’ (demokrasia ya umma). Ni mass democracy ndio ilipelekea kukubalika kwa dhana kwamba – vyama vya siasa ni kiungo muhimu au kiungo cha lazima baina ya - ‘the individual citizens’ (raia mmoja mmoja) and the ‘state’ (na serikali).
Lakini kwa muda mrefu, appreciation juu ya mchango wa vyama vya siasa kwa demokrasia ilihusisha zaidi uwezo wa vyama vya siasa kuratibu ‘large scale democracy’. Ni baadae sana (hasa baada ya vita kuu ya pili ya dunia – baada ya mwaka 1945) ndio umuhimu au mchango wa vyama vya siasa katika jamii ukawa ‘appreciated’ kwa mapana zaidi, hasa ‘attachment’ yake kwa ‘representative democracy’ (demokrasia wakilishi).
Ni baada ya kipindi hiki ndio vyama vya siasa vikaanza kukubalika au kuonekana sio tu kama ‘key institutions’ (taasisi muhimu), lakini pia ‘necessary & positive conditions for modern democracy’. Hili lilijitokeza zaidi baada ya ‘legal codification and constitutionalization’ iliyorudisha demokrasia katika mataifa ya Ujerumani na Italia baada ya Vita Vya Pili vya Dunia. Ni katika kipindi hiki na kufuatia hili, mataifa mengi duniani yakaanza kupitia upya katiba za mataifa yao.
Na hata katika mataifa yaliyo anza kufuata mfumo wa demokrasia katika miongo ya hivi karibuni, hasa kufuatia kusambaratika kwa iliyokuwa nchi ya Kisovieti (USSR) na baadae kuanguka kwa ukuta wa Berlin, kuanzishwa kwa taratibu za mfumo wa demokrasia katika mataifa haya (kwa mfano – nchi za ulaya kusini, ulaya mashariki, Afrika nk), mchakato huo ulihusisha uanzishwaji wa
‘free competition’ baina ya vyama vya siasa, pamoja na kuongezeka kwa uelewa kwamba vyama vya siasa ndio msingi wa mfumo wa kisiasa wa demokrasia.
Awali, Katiba za demokrasia za magharibi (western liberal democracies), zilipuuza vyama vya siasa kwa kipindi kirefu sana. Lakini kufuatia kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia, umuhimu wa vyama vya siasa ukaanza kutambulika kwa mapana zaidi kikatiba kiasi kwamba dhana zifuatazo zimekuja kuwa ‘defined, almost exclusively in terms of political parties:
Pluralism
Political participation
Competition
Pamoja na kwamba vyama vya siasa vya awali havikuwa na uhusiano wowote na dhana ya demokrasia,
leo hii vyama vya siasa vimeweka alama kubwa na isiyofutika ‘on democratic politics’. Wanazuoni Castles and Wilderman (1986) - “Visions and Reality of Party Government”, wana hitimisha hoja hii kwa maneno kwamba:
“20th century democracy can be best described as party democracy.”
Katika sehemu yetu ya NNE na ya mwisho, tutamalizia kwa kuhusisha sehemu tulizojadili awali na fikra za Kisiasa za Mwalimu Nyerere, kwa maana ya Nyerere’s Political Thought.