Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

Kumbe hata huko jela ulikuwa unafuatilia habari za ndege kuzuiliwa,naona umetoka kwa msamaha wa raisi,hapohapo na kuanza kusifia,karibu sana uraiani
 
nimesoma comments nasikitika kusema vibaraka wa MABEBERU ni wengi sana na kila siku wanajaribu kuweka vikwazo huku wakitumika na via azaki vyao kujifanya wanatufundisha demokrasia
 
Angeendelea kutwambia ni hatua zipi zilizochukuliwa mpaka ndege hiyo kuachiwa. .. Kama tumelipa basi tuambiwe ni kiasi gan? Kama tumeshinda kesi basi huyo mkaburu atatulipa sh ngapi.

Sent using Jamii Forums mobile app

UAMBIWE WE NANI?WESUBIRI KUIPOKEA TU, WENYE NAYO WANAJUWA KILICHOFANYIKA, ACHA KUHOJI YASIYO KUHUSU.
 
Ndege yetu iliyokamatwa Canada imeachiwa.
ilipokamatwa tulitangaziwa nani ameikamata na kwa sababu zipi (Madai ya Mkulima Steyn ya pesa zake).
Tuliambiwa mkulima amefungua shauri mahakamani huko Canada iliyoweka stop order ndege yetu ikamatwe mpaka mkulima alipwe hela yake.
Profesa Kabudi akatueleza kuwa atapambana mahakamani ili ndege yetu iachiwe.

Sasa tumetangaziwa kuwa ndege yetu imeachiwa na itakuja soon, Ila kitu ambacho hatujaelezwa ni
1. Je Tumemalizana na Mkulima Steyn kwa kumlipa madai yake?

2. Au Je tumemshinda mkulima Steyn Mahakamani?

Hizi taarifa ni muhimu tukajua kwa sababu hizi pesa zinazonunua hizi ndege ni kodi zetu.

Serikali itoe maelezo ili tujue kuwa tishio la mkulima Steyn kukamata mali zetu huko nje ya nchi halipo tena.

Serikali isifiche
 
MKULIMA AKIONA KUKAMATA NDEGE HAITOSHI ATAANZA KULENGA VIONGOZI WAKUBWA WA SERIKALINI WAKIFANYA ZIARA NJE YA NCHI
 
Haina hata haja ya kujiuliza, kwa wanavyopenda sifa tungekua tumeshinda kesi hadi samaki sa hivi wangekua wanajua... Lazima tutakua tumelipa yote au tumekubaliana utaratibu wa kulipa deni.
 
Back
Top Bottom