Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019


Naomba kazi boss ili niweze Kulipa kodi, Hizi ofa za mb nazo zinanisumbua boss!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tunataka kujua hiyo ndege imeachiwa kwa utaratibu upi au makubaliano gani? Hii kusema ndege yetu iliyokuwa inashikiliwa Canada imeachiwa haitoshi..!!!Je, imeachiwa baada ya kumlipa Mkulima Steyn 30m USD( about 64 Billions Tshs.) au imeachiwa kwa utaratibu kama ule wa South Africa baada ya Mahakama kutengua zuio kufuatia mvutano Mahakamani kati ya Mahakimu wa Africa Kusini na wale wa Tanzania?

Ukisoma hapa unaona kama kuna kitu kinafichwa hivi ili Watz wasijui kuna nini nyuma ya pazia. Ijulikane kwamba Watzkodi zao ndiyo zimetumika kununua hilo dege......!!!
 
Tuliza mzuka utaeleweshwa....
 

Kuna kitu unatamani kusikia,lakini bahati mbaya huna vigezo vya kukisikia.maana hamna taarifa utakayoipokea kwa wema.

Ukisikia kalipwa,utalaumu kwanini yalifanyika maamuzi ya kijinga 1980 yameleta madhara leo!!

Ukisikia hajalipwa,utalaimu kwanini halipwi pesa take na anatudai kihalali.

Jua ndege imeachiwa,kafanye mambo mengine.
 
Mkuu achana na wapuuzi...
wao kila hatua ambayo itakuwa imechukuliwa watalaumu tu!!!
 
kwenye KICHA CHA LEO ASEME AMEMLIPA DOLA MILIONI NGAPI HUYU MKULIMA NA WAMEANDIKISHIANA ATAMALIZA MWAKA UPI KULIPA ZOTE?
 
Hivi kule mahakama ya South Africa tulilipa au tulishinda kesi?
Naona mnatanua goli fasta fasta ili muwe na hoja angalau hata Kwa muda mfupi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata sielewi umejibu nini, kwamba SA tulishinda kesi automatically na pengine lopote ni lazima iwe hivyo? Nimeuliza ili nijue, kama huna jibu piga kimya.
 
Mwenye taarfa jinsi ndege yetu ilivyoachiwa anijulishe tafadhali, kwa nia njema tu.

Kwa kuwa Canada na SA kote masuala yalikuwa mahakamani, kwa SA tulielezwa mkulima alishidwa kesi hiyo pia rufaa alishindwa.

Canada bado sijui kimetokea nini nafahamu tu suala la mapokezi baada ya kuachiwa.

Ikiwa tumshinda kama SA, la tumeshidwa, aidha tumefikia makubaliano nae juu ya malipo au kama masuala yenye ni siri na mmekubaliana pande zote zisiseme chochote, basi ni vema tukajulishiwa kuwa mambo haya ni siri au vinginevyo, jambo hili linanifikirisha sana, hadi naamua nihoji muda huu

Nasoma maelezo mbalimbali sijafanikiwa kuona maelezo yake naomba mnisaidie kwa hilo.
 
Wengine tulitilia shaka hizo taarifa zilipotoka mara ya kwanza
 

wameamua tulipe yaishe

 
Wengine tulitilia shaka hizo taarifa zilipotoka mara ya kwanza
Nashidwa kufurahi toka moyoni kuwasili kwa ndege yetu, kwa kukosa uwazi na maelezo ya kutosha, nilitegemea kama ilivyoshikwa maelezo ya serikali yalieleweka na hakukuwa na lawama nyingi, hii kuto toa maelezo ni kukaribisha maneno, na maneno hayo yatakuwa sahihi kwa kuwa hakuna maelezo rasmi, Ni mbaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…