Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

gango2

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2011
Posts
1,956
Reaction score
2,274
Rais Magufuli akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi leo amesema Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa huru na itatangazwa siku itakapopokelewa. Pia Rais Magufuli amesema safari hii ndege hii itapokelewa Mwanza (tarehe itatangazwa).

“Ndege yetu iliyokuwa inashikiliwa Canada imeachiliwa, wananchi watatangaziwa tarehe ya kuwasili ili wakaipokea na tutaipokelea hapa Mwanza.” Alisema

Itakumbukwa Mamlaka nchini Canada zilikamata ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400. Kutokana na shauri la kesi iliyofunguliwa na mkulima mstaafu raia wa Namibia Hermanus Steyn

1576136762424.png


ZAIDI SOMA:
 
Rais Magufuli amesema Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa nchini Canada imeachiwa na itapokelewa jijini Mwanza hivi karibuni.

Rais Magufuli akiwa Mwanza kushiriki Semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, amesema kwamba 'Kwa taarifa tu, Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa siku ya kuipokea na itapokelewa hapa Mwanza”
 
Na Mbowe na CHADEMA rasmi wamemtosa Tundu LiSsu, sasa yuko (Tundu Lisu) mwenyewe, uongo huzunguka tu lakini haujawahi kumfikisha mtu popote mbele ya safari.
 
Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imekamatwa nchini Canada imeachiliwa na wananchi wajiandae kuipokea katika Uwanja wa Ndege jijini Mwanza. Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama tawala cha CCM leo Alhamisi Desemba 12, 2019 jijini Mwanza, Rais Magufuli amesema, “ndege yetu iliyokuwa inashikiliwa Canada imeachiliwa, wananchi watatangaziwa tarehe ya kuwasili ili wakaipokea na tutaipokelea hapa Mwanza.” Novemba 23, 2019, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa mabalozi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi alisema, “ndege imekamatwa na kesi ipo mahakamani. Aliyesababisha ni yuleyule (Steyn) aliyesababisha ndege yetu kuzuiwa Afrika Kusini.”

Alisema aliyesababisha Bombardier kukamatwa ni Hermanus Steyn, raia wa Afrika Kusini ambaye alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini akidai fidia ya dola 33 milioni. Kesi hiyo ilisababisha Mahakama hiyo kuizuia ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kuondoka nchini humo Agosti, 2019. Steyn, anadai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980. Hata hivyo, Septemba 3, 2019 mahakama hiyo iliamuru ndege hiyo iliyokuwa imezuiwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo kuachiwa baada ya Serikali kushinda kesi bila kutoa fedha yoyote.
 
Back
Top Bottom