Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imeshikiliwa nchini Canada imeachiliwa, athibitisha Rais Magufuli asubuhi hii jijini Mwanza. Asema siku ya kupokelewa itatangazwa.
“Kwa taarifa tu, Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa siku ya kuipokea na itapokelewa hapa Mwanza” Rais Dkt John Magufuli
Semina ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC)
 
Angeendelea kutwambia ni hatua zipi zilizochukuliwa mpaka ndege hiyo kuachiwa. .. Kama tumelipa basi tuambiwe ni kiasi gan? Kama tumeshinda kesi basi huyo mkaburu atatulipa sh ngapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, tumelipa kidogo, halafu tumefanya makubaliano ya kuendelea kulipa kidogo kidogo..

Hii iwe Siri, hawa wengine tutawambia tumeshindwa kesi, sawa?
 
Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imeshikiliwa nchini Canada imeachiliwa, athibitisha Rais Magufuli asubuhi hii jijini Mwanza. Asema siku ya kupokelewa itatangazwa.
“Kwa taarifa tu, Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa siku ya kuipokea na itapokelewa hapa Mwanza” Rais Dkt John Magufuli
Semina ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC)
Ishu sio kuachiwa, ni under what terms ineachiwa ndilo muhmu
 
Dawa ya deni ni kulipa

hata kwa kulipa kimya kimya..
 
Details za nini mkuu? Sasa hivi ni kushangilia na kusifu tu, baadaye hata tukiambiwa mkulima kalipwa tutashangilia vile vile, tena tutamsifu sana raisi wetu kuwa kafanya jambo la maana sana kwa kawaumbuwa mabeberu ambao walifikiri tutashindwa kulipa hivyo vijisenti vya hako kabeberiu kadogo ambako hakajaota hata ndevu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Napata tabu sana kuelewa kwamba kweli mtu anaweza akawa na mawazo ya kipumbavu kama haya?
Au anakuwa amepewa pesa ili ashawishi watu waanze kusifia ujinga huu?
Tunataka kujua ndege yetu imeachiwa kwa njia gani kama pesa amelipwa mkulima tujue na hata kama mkulima amelipwa watajitokeza wengine wanaotudai kukamata hizo ndege


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumemlipa beberu kimyakimya kama lile gwaride la kimya kimya.
 
Inawezeka yule balozi aliyeitwa na kabugi bila tashwishwi alipanik na kuwachangisha mabalozi wenzake wakamlipa beberu mwenzao
 
Usiruke makwanja hapa! Tunajadili ndege yetu inayo kuja ingawa Rais kaongea kwa unyonge bila kueleza imeachiwa kwa sababu zipi!
1. Tumeshinda kesi
2. Tumelipa deni lote
3. Mzungu kasamehe
5. Au makubaliano mengine?
Na safari hii atoe maelezo mwingine sio Kabudi, tumechoka uongo wake!

Sent using Jamii Forums mobile app
Majibu ni muhimu ili walipakodi tujue kama tumesamehewa tupumue kuwa hela zetu zimepona
 
Eti wananchi tutatangaziwa tarehe ya kuwasili ili twende tukaipokee.Na mapokezi ya ndege kitaifa mwaka huu yanafanyika Mwanza. Dah!
 
Mkulima ananyonya mvinyo taratibu ameshazisunda
Tulikuwa tunasema kwa muda sasa kuwa Dawa ya deni ni kulipa pongezi zimuendee JPM kwa ukomavu
 
Leta ruling ya mahakama tusome kama unayosema ni ukweli. Mmezoea kudanganya awamu hii mtanyooka tu! Kama DJ Mbowe amenyooka mtakuwa nyinyi vidagaa!!
Hili suala limefanyiwa nje ya mahakama na Ndege ilikuwa itue siku ya Uhuru lakini mambo hayakwenda vizuri
 
As long as ndege ilizuiwa na mahakama proceedings zitaonyesha kama serikali iliomba wakakubaliane nje ya mahakama acha uongo kawadanganye mbumbumbu wenzako huko ufipa
Mkulima kaambiwa ale pini tehteh shamra shamra za sherehe za uhuru zilikuwa ziende sanjari na ujio wa ndege
Halafu wangegeukiwa viongozi wa Upinzani na kusimangwa.
 
Back
Top Bottom