Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

Jino la mwisho la mkulima litakuwa linaonekana kwa kicheko cha furaha
 
Mchimba kisima kaingia mwenyewe, afisa habari Prof.Kabudi yuko wapi?!

Tulizoea yeye ndiye hutuletea taarifa za ndege kukamatwa na kuachiwa.
 
Jino la mwisho la mkulima litakuwa linaonekana kwa kicheko cha furaha
Gharama za kutuma mawakili Afrika kusini si bora tusingemfukuza mkulima halafu tungeketi nae ili atupunguzie deni kimya kimya halafu mambo yangeenda bila chenga
Sasa huu ubabe utafanya hata wanaotudai wengine nao waende mahakamani
Halafu asset rahisi ni hizo ndege zetu zinazipasua anga
 
Tuliwaambia itaachiwa mkasema mkulima anakabidhiwa hiyo ndege sasa limebuma naona kiroho chenu kinawauma kweli hasa msaliti namba moja Tundu Lissu. Awamu hii mtanyooka tu! Hapa kazi tu!!

Uliwaambia akina nani? Huyo mkulima hajateka hiyo ndege, bali alishikilia mpaka alipwe chake. Yeye hahitaji ndege anahitaji hela yake, kama ameshalipwa aishikilie ili iwe nini kwa mfano? Ujumbe wetu ulikuwa wazi, uonevu na kutofuata sheria mnaweza kuufanya huku ndani kwenye vyombo visivyo huru, lakini mkienda sehemu sheria zinapofuatwa lazima haki itendeke, na hilo limefanyika. Hata haya mnayofanya sasa ya kuchezea box la kura, na kumnyanyasa kila asiyekubaliana na mitazamo ya watawala ni mambo ya muda, ila ipo siku itafika mwisho.
 
Hivi bongo hatuna majajusi kaliba ya Jack Bauer
 
Leta proceedings za mahakama kama kweli amelipwa la sivyo utakuwa unatoa mapovu bure!!

Leta proof kama imeachiwa tu bila kupewa chake. Baada ya kukamatwa A. Kusini na kuachiwa Tambo zilikuwa nyingi kuwa tumemshinda, hizo Tambo huko Canada zimeishia wapi?
 
Boss gango2 Hongera Mh. Rais na Jamhuri na Serikali na Wananchi na WaTanzania, Huu ni Ushindi mwingine mzuri na mkubwa kwa Taifa na Nchi.
Ushauri tu, Tumalizane kabisa na huyu Mkulima. Tunajua dawa ya deni ni kulipa, lakini pia MDENI hafungwi.


Rais Magufuli akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi leo amesema Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa huru na itatangazwa siku itakapopokelewa. Pia Rais Magufuli amesema safari hii ndege hii itapokelewa Mwanza (tarehe itatangazwa).

“Ndege yetu iliyokuwa inashikiliwa Canada imeachiliwa, wananchi watatangaziwa tarehe ya kuwasili ili wakaipokea na tutaipokelea hapa Mwanza.” Alisema

Itakumbukwa Mamlaka nchini Canada zilikamata ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400. Kutokana na shauri la kesi iliyofunguliwa na mkulima mstaafu raia wa Namibia Hermanus Steyn



ZAIDI SOMA:
 
Gharama za kutuma mawakili Afrika kusini si bora tusingemfukuza mkulima halafu tungeketi nae ili atupunguzie deni kimya kimya halafu mambo yangeenda bila chenga
Sasa huu ubabe utafanya hata wanaotudai wengine nao waende mahakamani
Halafu asset rahisi ni hizo ndege zetu zinazipasua anga
Lazima waanze kuvizia mkuu maana mkulima kasha wapa mwanga!
 
Lazima waanze kuvizia mkuu maana mkulima kasha wapa mwanga!
Shida yote imeletwa na mkuu wa nchi kusema kwa mbwembwe kuwa nchi ni tajiri na inafedha
Mkulima alikua anasinzia sinzia aliposikia hivyo ghafla akasogea kwenye tv baada ya hapo akaenda kukaza hukumu
Just my imagination
 
Hakuna jambo litokealo bila kuwa na sababu, hata kifo chochote kile lazima kiwe na sababu. Hata wale walio toka gerezani juzi ni kwa sababu ya msamaha wa kikatiba ulio tekelezwa na Rais kwa mujibu wa sheria.

Ndege yetu ilikamatwa na mkulima huko Canada na tuliambiwa mawakili wetu wameenda huko kutetea kesi hiyo baada ya kumuita Balozi na "kumuonya" hii tabia yao ya kuruhusu kamatakamata kama ya wapinzani kwa ndege zetu.

Leo tunatangaziwa ndege imeachiwa bila ya kupewa ukweli wa kilichotokea.

Je, tumeshinda kesi kama "tulivyoshinda" SA hivyo tungoje akakamate tena Mumbai? Au tumelipa hayo mabilioni hivyo tusubiri tuu serikali kupeleka maombi ya ziada bungeni?

Na mwisho tuambiwe kama Kabudi kamshawishi mkulima atusamehe deni ili nasi tumpe tuzo Kabudi na shukrani kwa muzungu!

Usiri wa nini sasa wakati ndege inarudi na sherehe mnafanya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka mwanzo tulishauri umuhimu wa kutatua tatizo kikamilifu kuliko kufanya ujanja ujanja unaotoa suluhisho la muda mfupi.

Tumepoteza muda wetu mwingi kwa kuruka ruka lakini mwishoni tumeishia pale pale - KULIPA.
 
Tungeshinda kesi "Prof. Jalalani" angeweza kujizuia kutamba kweli mpaka muda huu? Mkubwa ukivuliwa nguo, chutama!

But muhimu kwa sasa ni ndege yetu imerudi. Na tutaipokelea mwanza.

Ushamba mzigo!
 
Tatizo ni kama kuna kitu mlitamani na kusubiri kitokee,hakijatokea.

Wewe subiri ikikamatwa nyingine ndio utajua kumbe still hata huko canada kwenye uhuru wa mahakama,serikali ilitumia ubabe wake wa ktz,ikachukua ndege yake au lah,kama ilivyotokea kwa SA.
 
Back
Top Bottom