Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

Rais Magufuli: Ndege yetu Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa Canada imeachiwa, itapokelewa Mwanza, tarehe 14/12/2019

Tatizo ni kama kuna kitu mlitamani na kusubiri kitokee,hakijatokea.

Wewe subiri ikikamatwa nyingine ndio utajua kumbe still hata huko canada kwenye uhuru wa mahakama,serikali ilitumia ubabe wake wa ktz,ikachukua ndege yake au lah,kama ilivyotokea kwa SA.
Tuliza akili na andika kwa utulivu. Jee tumelipa? Tumeshinda? Au tumesamehewa? Hata hilo ni siri?
Na tukio la ndege kuachiwa ni mpaka Rais ndio aseme?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya Magufuli imekosa ukweli na uwazi. Ni serikali full of longolongo.
Mkulima kalipwa mamilioni ya dola, Tena kwa cash kama tulivyonununua majindege yenyewe
 
Wamesema ili kuwashughulikia wasaliti wote walioshiriki ktk sakata hili kwa kukosa uzalendo, wameamua kupiga "kwata ya kimya kimya" (By Kamwele)
 
Chakaza,

Muulize tundu lisu atakuwa anajua au zito kabwe maana hao huwa wanapata taarifa za kweli, ila ukisubili serikali huwa inasema uongo, na pengine hiyo haijaachiwa labda wamenunua ingine ya kutungua kwa keshi ili kutuzuga.
 
Tumeshinda kesi...
IMG-20191212-WA0114.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakaza,
Bandiko lako linaonyesha wazi kwamba wewe sio mmoja wetu kama ulivyobainisha mwenyewe kwa kusema "na sherehe mnafanya." Sasa unataka kujua kama tumelipa au hatujalipa ili iweje,mbona jambo hili halikuhusu,mbona sio lako.Kaa pembeni bwana,tafadhali endelea na hamsini zako na sisi tuache tuendelee na mambo yetu.
 
Mkwara wa Kabudi ulisaidia sana, MABEBERU yakisikia sauti ya mzalendo Kabudi yanaingia hadi chini ya meza kwa uwoga MABEBERU yaliposikia ya kwamba na sisi tumekuwa DONA KANTRE yaliona aibu sana, kongole kwa mawakili wetu

Naambiwa zilionyeshwa hadi picha za utawala katili wa makaburu ambao mkulima naye katokea huko. Vile vita vya korosho tulivyoshinda kwa kutumia jeshi mahiri kabisa duniani viliwatisha MABEBERU HAYO ya Canada yakaona bora yaishe. Mkwara wa Profesa Kabudi kuacha kutoa order za ndege Canada ulisababisha mamia na maelfu ya wacanada kuandika petition kwamba ndege iachiwe maana speed ya Tanzania kununua midege kwa cash tena na mengine yanakuja ni faida kwao na ajira nchini mwao hivyo wakihamia Brazil itawacost sana

Mawakili wetu pia wa li shine sana mahakamani,ilichukua dakika 20 tu judge Smith ku dismiss case huku mkulima akingua kilio na kuambulia patupu. Hongera sana awamu ya tano kwa kushinda kesi na kuwezesha mawakili kuwa na kiwango cha kimataifa

Hongera awamu ya tano kwa kumtoa Profesa Kabudi jalalani bila yeye sijui ingekuwaje kwa kweli, hongera sana mtukufu two phd's holder dr John Pombe Joseph Magufuli. Dege la nane linatua Mwanza ambapo nataarifiwa jiji limezizima likiisubiria kwa hamu kubwa na mapokezi hayo yanatarajiwa kuwa livestreamed nchi zaidi ya 75 duniani ambapo wengi wanashangazwa na KASI KUBWA NA KISHINDO KIZITO cha awamu ya tano kama vile ujenzi wa ma flyovers, viwanda 4000 ndani ya miaka 4, viwanda 100 kila wilaya, zahanati 357 nchi nzima, haijawahi kutokea dunia nzima inashangazwa na kumkubali sana DR JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI
 
Inside is for inner
Sio lazima kila kitu ujue
Itoshe kuambiwa imeachiwa

Ndege yao, we unataka ujulishwe kilichofanyika ikaachiwa, ili ufanyeje?

Wakati inanunuliwa ulijulishwa?

CAG anaruhusiwa kukagua ?

Tulia subiri kuipokea , MBULULA WEWE.
 
safi sana walifikiri tunaibiwa kirahisi awamu hii? wakacheze tu na watoto wao huko
 
Chakaza, Punguza kuhangaika mkuu. Unaambiwa ndege ishaachiwa bado hutaki tu unataka kuendelea kuibua vihoja dhaifu.
Haya inaonekana unapenda Sana sababu

Basi na wewe tuambie Umeandika haya kwa sababu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tungekuwa tumeshinda kesi yule LeProfesseri "mijicho" angekuja hapa speed kujitapa na kutoa povu la nyimbo za utukufu kwa awamu ya 5. Lakini kwavile serikali yetu imepigwa dafrao wamerudi wameinamisha vichwa kwa aibu, na wanaongea kinyonge sana.
 
Mmeanza kutafuta sifa, hamuoni hata aibu, lipeni Deni vinginevyo ndege itakamatwa Tena muaibike tena
 
Walifurahi sana kusikia imekamatwa. Walikesha wakiomba isitolewe ili wacheke. Wamefeli sana.

Leo hii aibu zimewajaa. Wanainamisha vichwa chini kwasababu hawana la kusema. Wameumbuka sana.

Sisi tunaangalia juu tukiwa na nyuso zenye furaha na tabasamu. Tunafurahia kurudi kwa ndege yetu. Tuna uzalendo.

Tarehe 14/12/2019 ni kesho. Nadhani watajifungia ndani jinsi aibu ilivyowajaa.

Ndege ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Niliona ACTL ikitoa gawio ili fedha hizo zikasaidie maendeleo ya jamii. Pongezi kwao.

Waendelee kutazama chini na sisi tunatazama juu. Tunawapa vidonge vyao. Wakimeza wakitema shauri yao. MAGUFULI SAFIIIIIII. Kama mzalendo wa kweli itikia...ukinyamaza mnafiki.
 
Back
Top Bottom