Uchaguzi 2020 Rais Magufuli ndiyo anaibuka kuwa atawaongezea mishahara wafanyakazi. Tunamwambia kuwa hatudanganyiki ng'oo

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli ndiyo anaibuka kuwa atawaongezea mishahara wafanyakazi. Tunamwambia kuwa hatudanganyiki ng'oo

Huyu acha dharau zake zimtokee puani. Uongozi wa nchi unahitaji uwe na heshima kwa unaowaongoza maana ndo waliokuweka hapo. Sasa acha akapumzike na mifeni yake.
 
Watumishi wote na familia zao kura kwa lissu,mmeteseka kwa kukandamizwa stahiki zenu kwa muda mrefu sanaa.Miaka 5 mmekuwa kituko mtaani maisha yenu.
 
Hawezi kuongeza mishahara! epuka kuipa nafsi yako majuto na masononeko ya miaka 5 kwa matumaini hewa, ipe faraja nafsi yako kwa kumnyima kura asubuhi na mapema.
 
Watumishi wote na familia zao kura kwa lissu,mmeteseka kwa kukandamizwa stahiki zenu kwa muda mrefu sanaa.Miaka 5 mmekuwa kituko mtaani maisha yenu.
 
Ndugu yangu kumbuka sheria ni msumeno inakata mbele na nyuma. Ukiwa mfanyakazi unalindwa na sheria sawa lakini ni lazima pia mfanyakazi ati sheria za kazi. Mfano uwajibikaji, kutokupokea rushwa, vyeti feki, wizi hizi zote zinamuondolea kinga. Nchi kabla Magufuri hajaingia madarakani wenyenchi yao ambao ni wapiga kura walikuwa na malalamiko Kila kona yanayohusu rushwa, kuzalauliwa na hao watumishi wa uma. Kucheleweshewa kwa makusudi kwajili ya urasim. Kwakifupi walikuwa watumishi wengi wezembe walirudisha nyuma uchumi wa nchi wakati huohuo wao wanaendelea kudai maslai haki. Au umejisaulisha ndugu yangu, nasema uongo ndugu yangu. Ilikuwa imefika wakati ukitaka kumuandikisha mtoto darasa la kwanza mwalimu anakuomba pesa la sivyo atakwambia nafasi zimejaa. Sasa jemedali wetu mtetezi wawanyonge JPM ameingia kaweka mambo sawa tunampa mitano mingine ili kazi iendelee.
Hayo ndiyo yanajustify watumishi wa umma kutokupewa nyongeza ambayo ipo kisheria na ina madhara chanya kwenye mafao yao? Kwanini wana Lumumba mna akili nzito kiasi hiki, je unaelewa madhara ya kutokuwapa nyongeza kila mwaka kama sheria inavyotaka? Jibu swali kama huwezi muite KM Bashiru akusaidie.
 
Kuondoa FAO la kujitoa Ni ugomvi mkubwa na Wafanyakazi private sekta.

Mwaka 2018 Magufuli na CCM walifuta FAO la kujitoa bila kujali maoni ya TUCTA.

Wafanyakazi sekta binafsi walilalamika, CCM NA MAGUFULI hawakujali.

NSSF wanalipa 33% ya mshahara wa Mwezi na watu hawajui Ni Lini watapata Pesa zao.

Watu wote wanastahili fao la kujitoa.

Wale MATAGA wanaitetea CCM hawaonekani kwenye Uzi huu.
Mataga walio wengi hata kazi hawana, wanabangaiza vibarua Lumumba, wanalipwa posho hata mshahara hawaujui. Hawajui increment wala fao la kujitoa. Kwa ujumla hawajui chochote zaidi yakusema CCM oyee, na hata elimu zao tia maji tia maji, msomi gani utamuajiri umlipe posho tu bila mshahara? Hawa wananjaa sana wasidhani hatuwajui.

Wenye vielimu kidogo ndio hao wamegombea uenyeviti katika ngazi mbali mbali za chama, hawana mshahara zaidi ya posho, ufisadi na hisani, kupigizana kelele na mataga kuhusu Fao la kujitoa ni kupoteza muda maana hawaelewi chochote!
 
Unaandika pumba, bilashaka wewe ni mchumia tumbo au unakaa kwa dada yako!!

Acha tunaojielewa tumshughulike huyu katili, jizi, Mbaguzi Jiwe
Hao ni vijana wa lumumba pale hawajui lolote zaidi ya kutetea Zile buku 2 kwa siku
 
Wewe acha unafiki unafikiri hutoba ya jana alisoma akiwa chumbani kwako tu. JPM amejipambanua kwakusema ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Aidha jana ametoa sababu za wazi kabisa kwamba alikuwa amaimarisha uchumi akimanisha ukusanyaji wa kodi, kuziba mianya ya rushwa, wafanyakazi hewa, kuzibiti mafisadi, kuongeza nidhamu na uwajibikaji kazini. Sasa ameona mambo yapo kwenye right truck, uchumi umekua nidhani kazini na uwajibikaji umekua sasa mishahara itapanda kwa speed ya kimbunga.

Sisi wananchi wajasiliamali tumemuelewa sana. Tunajua miaka mitano tulikotoka hapa tulipo na tunako elekea. Usiishi kwa mazoea utafilisika ndugu amka. #JPM mi5 tena kazi iendelee
Je sheria inasema hivyo kuhusu kupandishwa mishahara ya watumishi wa umma, je pia Kuna exceptional yoyote katika sheria inayotaka mtumishi wa umma aongezewe mshahara kila mwaka? My friend kwa sasa watu elimu iko kwa kichwa sana
 
Kama amesema serikali yake inapanga kuongeza mishahara ya wafanyakazi ni kwasababu tayari ameshaujenga uchumi kwa kiwango cha kuruhusu kuwepo kwa nyongeza hiyo.hata hivyo kwa sasa inawezekana kutokana na namna alivyoujenga uchumi katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.


Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
Uchumi umeimarishwa na bado unatumia TECNO F3 ya laki 2.huo uchumi haujakufikia? 😀

(msikie atakavyojishebedua)
 
Tatizo la serikali hii ya awamu ya 5 ni kutoa kipaumbele katika mambo ambayo hayana msingi..............

Angalia sasa jinsi walicyokuwa wakihangaika na kuwanunua wabunge wa Chadema, wakiamini kuwa ndiyo wanakiua chama hicho.............

Sasa angalia jinsi walivyoingia hasara, badala ya kukiua chama hicho jinsi walivyokuwa wakiwaza, ndiyo kwanza kimekuwa more stronger and stronger
Acha uongo, ustronger upi?
 
Back
Top Bottom