HOJA ZA KUONGEZA MUDA WA URAIS ZIKEMEWE NA ZIPIGWE MARUFUKU KABISA!
Katiba ya nchi ni kama msahafu kwa nchi husika, ni nadra sana kufanya mizaha na misahafu mitakatifu.
Hivi karibuni wamezuka watu ambao kwa maono ni walevi wa mchana ambao kila kukicha wanazidi kuongezeka.
Leo huko korogwe bila aibu amezuka Mbunge na kudai kuwa Rais aliyeko madarakani aongezewe muda atawale miaka 20!
Siku za karibuni aliwahi pia kuibuka mmojawapo wa Rais mstaafu naye akatoa hoja kuwa Rais aongezewe muda .
Labda tukumbushane, hoja hizi dhaifu hazikuanza leo wala si ngeni, kule zanzibar zilizuka wakati wa Dr.Salmin au wao wanamwita komandoo, walevi wa mchana wakapaza sauti aongezewe muda.
Ni mwaka 1990 wakati Rais Mwinyi anazindua kipindi chake cha mwisho cha utawala aliibuka mshairi mmoja pale jangwani, akaghani shairi lililorushwa mubashara na RTD mchi nzima, huku akitoa rai kuwa hakuna haja ya msururu wa wastaafu kuwa Mwinyi apewe muda wa nyongeza.
Ni Julius Nyerere aliyekata mzizi wa fitina kwa kukemea kwa uwazi kuwa hakuna haja ya kubadilisha katiba kutengeneza masultani na wafalme.
Ikumbukwe kuwa kama Mwinyi angebadilisha katiba na kusalia madarakani basi tusingekuwa na waluomfuata yaani Mkapa, kikwete na sasa JPM
Ni wazi kuwa wanaovimbiwa kwa sasa na kutaka katiba ibadilishwe wasingekuwepo.
Kuna habari kuwa JPM amekemkea Mbunge aliyetaka katiba ili atawale miaka kumi, iwe ni fundisho kwa wale wote wanaojikomba ili kuidhaliisha katiba yetu, tuwajatae mchana kweupe!
Sent using
Jamii Forums mobile app