Rais Magufuli, samahani mimi sijakuelewa kuhusu COVID-19 tests...

Rais Magufuli, samahani mimi sijakuelewa kuhusu COVID-19 tests...

Mh Rais sisi Watanzania pamoja na unyonge wetu nakuku amini kama Rais wetu kiukweli hatukuelewi na mimi sitaki kuwa mnafiki napenda niweke kumbukumbu sio kubishana na mwalim hapana ila kumwambia mwalim sijakuelewa.

Leo umesema mlipeleka sample za mbuz?, oil,mafenesi na mapapai na vilileta majibu + nikorona.

Mh Rais what if wapimaji hawakuwa makini nakitokana na sampul nyingi wakaleta result hiyo?

Pili kama kweli unayoyasema sisi hatupo kwenye kisiwa Kwanini usiwaite who waje Tanzania washuhudie huwo udanganyifu wa mabeberu,?

Mh unatukumbusha zama zile za mwal alipozuwia tv na yeye akajifungia ndani na satelite yake akiona dunia inaendaje nakuja tusimulia. Zama zimebadilika taifa lina watu wana akili kiasi zinamwagika kutupa maneno yajumla jumla while hatujuw kesho yetu nihatari kwa ustawi wa taifa letu na usalama pia.

Ulisema watu wajifukize lakini ili kukiuwa kirus cha covid unaitaj joto linalo fikia 56-58c je kuna mwanadam anaweza kujifukiza mpaka kwenye hicho kiwango wakati joto lamwanadam tu halizid 37cent. Hivi kweli unajuwa madhara ya hotuba zako kama Rais na mwisho wake.

Wewe ndio rais wetu ila wewe sio Dr wala sio mwanasheria wala bunge. Why kuongelea watu wengine nakuwaacha ktk mkwamo bila majibu? Sasa wafanyeje?

ima maana kwa kauli yako mask na vipimo vyote fake so what is alternative2.

Mkuu wangu na mzee wangu zitafakari kauli zako. Unatuathiri sana kamaRaia kisaikolojia. Je tumsikilize nani?
Anakuambia vipimo fake. Si anunue original ?
 
Kwani ni kipi kilicho msukuma hadi kupima matunda, mbuzi na oil na kwa malengo gani au aligundua nini kabla? tuanzie hapo huenda labda mimi ndio sijaelewa,
Update:
Hoja ya Rais nimeielewa, hoja yake ilikuwa kama sampuli hizo zilizo pimwa zimekutwa (+Ve) basi huenda pia kuna wengi wanapimwa na kupewa majibu yasiyo sahihi.
 
Wakuu tusiache kuchukua tahadhari za kujikinga na Corona. Kinga ni bora kuliko tiba.
 
Kama tuna kiongozi anaamini kabisa taarifa aliyopewa kuwa "sample" zinatoka kwenye oil, fenesi, papai, mbuzi, kondoo na binadamu zote zinaleta majibu ya kimaabara yenye kufanana kuhusu gongwa hili. Basi kama nchi tuna tatizo kubwa sana la kiuongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa anataka kuaribu mashine ya kufanyia uchunguzi wa Corona alafu aseme mashine ni mbovu.
Dr watuambie; sample ya corona inayopelekwa maabara inachukuliwa nini...damu..majimaji..nyama...au kitu gani; afi hizo sample zipatikane kwenye oli..fenesi..papai...mbuzi..kondoo...binadamu adi kwenye mchanga.
Nimechoka niliposikia hadi sample ya oil ya gari!
 
Back
Top Bottom