Hivi, haeleweki wapi? Maelezo yako pia yamejaa paukwa za miaka mingi huku ww ukiwa hutaki muono wa sasa.
Mwl gani unayemzungumza eti alikuwa anajifungia na satellite anaona mambo ya duniani Kisha anakuja kutuhabarisha kuwa ameona maono .
Hizi ni paukwa ambazo kiuhalisia mpaka leo zinajionesha Mwl Nyerere alikuwa Genius kwa kiasi kikubwa lile alilofikiri na kulitoa kwa wananchi baadhi walipokea, wengine walibeza na wengine kukaa na mashaka.
Mwisho wa siku yalipojiri, wengine wanasema aliona kwenye satellite kabla, wengine wanasema alioteshwa wengine wanashangaa
Rudia hotuba zake kila toleo utaona usema SATELITE ni upuuzi.
Mfano anaposhangaa vigogo duniani kuungana huku viinchi vidogo vikifikiria kutengana ni upuuzi unahitaji kuwa na satellite .
Kuwa na mitazamo mipana ya kuwa na jumuiya ya Afrika Mashariki yenye nguvu kiuchumi huku wananchi wa Afrka Mashariki wakiwa wamoja wenye kuushi kwa upendo kiasi mabeberu wakapambana na kufanikisha kuiua hiyo jumuiya bado unahitaji Mwl ajifungie kwenye satellite ?
Tusijidharau kiasi hicho, rais anayomashaka makubwa hata mm ninapoumwa na kwenda kuchukua vipimo pia huwa na mashaka.
Moyoni ningependa hata kuwekwa wazi hii ndo damu yako , tunachanganya na hiki na hiki Kisha tutapata hiki katika kugundua hili, iwe mkojo, mavi, nk.
Hongera Rais NAKUKUBALI.