Rais Magufuli shujaa wa Kiswahili hakuna ubishi

Rais Magufuli shujaa wa Kiswahili hakuna ubishi

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Sitaki kuongea mengi ila toka ameingia 2015 mpaka kufikia hotuba yake ya jana ni dhahiri huyu mzee amekuza Kiswahili sana.

Nimependa sana anavyojiamini, hata akiwa na mgeni badala ya kuwa mtumwa wa lugha amekuwa shujaa wetu.

Tumpongeze kwa hilo tafadhali. Zamani, Watanzania wengi walifichwa mambo mengi kwenye lugha ya Kiingereza. Mf. Ukienda ofisi ya uma kueleza shida yako unaweza jibiwa kwa neno ambalo hulielewi na hapo hutakiwa na cha kuuliza tena.

Vivyo hivyo unakuta mtumishi wa serikali anazungumzia jambo basi kingereza 60% na Kiswahili 40%

Hata mahakamani sasa itakuwa Kiswahili hili jambo jema.
 
Kwan ni nani hapa anayejua kiswahili vizuri anayeweza sema n zaidi ya Magu? Magu anapambania anachokiamini. Love this guy
 
Magufuli hajui kiswahili fasaha wala kingereza cha grammer. Anajua kizinza tu
Hata kama ila anataka kitumike serikalini ili kila mtu aelewe, atakuja mwingine ataendeleza zaidi.
 
Halijui Kimalkia limebaki kuwaonea wivu wenzake!
 
Kuna jirani yangu anajifanya yeye ni shujaa kwenye kiswahili ila akiwa pale Kolumbiyo university panapohitajika kutumia lugha ya malkia uwa ananywea kabisa kama kamwagiwa maji ya baridi.
 
Anakipambania kivipi? Hebu tuwekee ushahidi husika wa kuonyesha juhudi zake za kukipambania Kiswahili? Na unakipambaniaje kitu wakati wewe mwenyewe hutafuti muda wa kujifunza ili ukijue vizuri? 😳😳😳
Hata kama hajui lakin anakipambania.
 
Back
Top Bottom