Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Ha ha ha ha.. Kila siku wanapewa mimba.. wanabakwa na kupewa mimba.. Mie nawajua ni watoto sifanyi nao zinaa.. Miguberi ipo kibao huko iliyokubuhu, na mafundi pia..
Ndo wawataje sasa hao wabakaji.

[HASHTAG]#namuungamkonorais[/HASHTAG]
 
Hahah magufuli utadhani hizoo hela anazotoa nizake anatoa mfukoni anavoongea sasa.....
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

Ndio hapo sasa wazazi kulea vyema, kama wanataka wasomeshwe bure au wawapeleke private schools huko hakumuhusu.

Ila kasema kuhusu wanafunzi wanaweza fanya ile ya kuzaaa then anarudi, anaenda tena kuzaaa anarudi na pia kuanza kuwapa habari za uzazi na hayo waliyotenda na kuvutia wengine... iki tunajua lipo na linafanyika duniani katika mengi kama binti hajajiweka sawa na kujua hatakiwi kujaribu. So itawavutia wajaribu halafu wapate raha na kujua shuleni watarudi tu bila wasiwasi huku wazazi wakijua hawahitaji kulipa.

Kasema waende veta etc kqma ndio wameamua kuzaa wa bahati mbaya kuna njia za kupitia hata sheria ipo kwa waliowagikisha walipo.. kama mvua 39 etc. So nafikiri kesi zingine zitaangaliwa zilivyo na kuchunguzwa haswa na kuwapa nafasi. Waongo watajiweka pabaya.
 
Kwa hilo la mwanafunzi mzazi hata mimi napinga kwani atashauri na wengine
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.

Lkn walikuwa wanshangilia
 
Inakuwaje pale Binti mwanafunzi akapata mimba baada ya kubakwa!!
unatoa taarifa polisi within 24 hrs, unapatiwa tiba yavali na unakuwa na documentation, daktari atathibisha kuwa kweli umebakwa

lingine
 
Ameyasema hayo leo akiwa Bagamoyo kwenye uzinduzi wa barabara.

"Kwenye utawala wangu siko tayari kuruhusu ujinga kama huu, kama wanaona inafaa basi wafungue shule za wazazi ili huku wakiendelea na masomo waendelee kunyonyesha watoto wao."

Ameongeza kuwa hizo NGOs ndio zimeleta mambo ya ajabu ajabu hadi wanaume kwa wanaume kuingiliana, wanawake kwa wanawake kuingiliana.

"Hata wanyama hawafanyi hivyo mbuzi Ng'ombe huwezi kuwaona wakikosea ile sehemu...Wachungaji si mpo hapa mmewahi kuwaona mbuzi wakikosea au ng'ombe wakikosea"....aliongeza Magufuli.
huyu mzee hana hekima hata kidogo. kama baba mwenye familia huwezi ropoka maneno kama haya mbele ya familia yako. trust, mzee huyu hana hata chembe ya aibu
 
7102031d419eeffc02efa339699b5634.jpg


Rais Dkt.John Pombe Magufuli amesema kuwa katika kipindi cha utawala wake hakuna mwanafunzi atakaye rudi shuleni akipata ujauzito na hata baada ya kujifungua kwani wakiruhusiwa kurudi shule wataharibu wanafunzi wengine.

"Kuna watu nimewasikia wanatetea wanafunzi kurudi shule baada ya kujifungua, yaani sisi unataka tusomeshe wazazi? Ndani ya utawala wangu kama Rais hakuna mwenye mimba atarudi shuleni kama akipata ujauzito, hawa watu tukiwaacha watazaaa mno, sababu huo mchezo ni mzuri. Katika kipindi changu kama Rais ukipata mimba kwaheri na hao NGO wanaotetea kama wanataka wajenge wao shule za wazazi lakini si shule za serikali"Amesema [HASHTAG]#RaisMagufuli[/HASHTAG].
 
Ukitazama kwa jicho la tatu utagundua NGO'S nyingi sana hapa bongo zinapata support kutoka nje ambazo zina masharti magumu kiasi kwamba endapo watashindwa na misaada inasitishwa, so wao wanaangalia matumbo yao na kufumbia macho athari katika jamii!
Very very True...
 
Huyu jamaa huyu,ana maneno makavu sana

Huyu Mkulu nasikia kabla hajaenda kuongea kwenye hazra huwa anapitia mtaa fulani huko Tanga unaitwa Majani Mapana a.k.a Wide Leaf! Akishalikoka basi atatiririka kama vile yuko mteremko wa Kitonga!!!!!
 
Sasa picha ndio linaanza.
Mkuu keshasema na alishatamka kwamba hapangiwi na mtu.

But my take mheshimiwa sana rais wetu nadhani inatakiwa awe na akiba japo kidogo ya maneno because alwayz what goes around comes around too that thats the law of karma.

Kuna mazingira mengine ya upatikanaji mimba ambayo unaweza kumhukumu bure kabisa mtoto wa kike i.e ubakaji
Ndo wawataje wabakaji. Mara nyingi wabakaji wamekuwa wakiachwa tuu wawabebeshe mimba wanafunzi wwngine.

Kwa hili nipo upande wa Rais.
Ukibakwa nenda mahakamani. Mbakaji afungwe wewe uzae na usomeshwe.

Usipopeleka mbakaji jela zaa na hamna kusoma.

Maana kuna wengine wanajitakia kabisa. Ni kiherehere chao.

NB: ukifanya mapenzi na binti umri chini ya 18 Umebaka. Subirini maembe yaive. Kuna Team Wasaka Bikra ndo wanaharibh watoto.

Kwa wanafunzi wasikaribie mazingira hatarishi, watahatarisha Elimu zao.
 
L
hii ni sheria ambayo nikipewa urais wa siku moja pale magogoni nitaifuta kabla ya lunch time,all girls rukusa kuendela na masomo baada ya kuzaa,kwanza imejidhihirisha kuwa kuwa fukuza shule kumepunguza mimba mashuleni,ndio kwanza zinaongezeka
Rais kasema waondoke katika mfumo wa shule za serikali...

Hajakataza wasendelee na masomo... Mbona mnajivika ukilaza kiasi hiki..

Nna wasiwasi hiyo video hamjaisikiliza..mnakurupukia comments tu.
 
Mie naona ameongea kujifurahisha ili aonekane mkali unajua hata baba kwa mtoto wake lazima ampe mikwara kwamba ukipata mimba nakufukuza hapa nyumbani kwangu anafanya hivyo ili mtoto awe makini na masomo hivyo magufuri yupo sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom