Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Je mwanafunzi akimpa mimba Mwalimu wake? 'Tatizo hapa ni maadili katika jamii zetu' inatakiwa tutatue tatizo na siyo kulikimbia
kilicho katazwa ni mwanafunzi kupewa mimba afu azae afu arudi shule,, hilo la Mwanafunzi kumpa mimba mwalimu wake hilo lako
 
Sasa km hawezi kusomesha watoto walio pata uja uzito kwa kubakwa na mtu huyo huyo anawaonea huruma wauaji na kuwatoa jela... ! Hii inaleta picha gani, km kiongozi ni msomi anashindwaje kujua tatizo la ujauzito ni suala mtambuka... kuwasomesha waathirika siyo sababu ya kulikuza ... uelewa huu unazungumzika kisomi tu nje ya hapo haiwezekani, ukitaka maoni ya watu halina mashiko kabisaaa tena huku kwa walalahoi wasomi wa shule za kata watakushangaa ... ajabu mtawala msomi (km kweli) anaamini hivyo
 
Sheria ni msumeno wote wanatakiwa kufukuzwa shule.

Ndo maana lazima uwe na utulivu, uelewa na busara ya "shule" kulijadili hili siyo kila mtu anapumzi ya kulizungumzia..... kaa huyu amekariri sheria ni msumeno hajui hata kwanini inakua msumeno kwa "watoto"
 
Sikulaumu, kumuunga mkono Rais kwa hili jambo lazima wewe huna elimu.
Ujue wewe ndiyo unamatatizo,yanayo takiwa kupingwa ni sheria na siyo utekelezaji wa sheria,sioni wewe ulioenda shule ukiijadili,sheria ni msumeno kila mahali duniani,kama ina madhara inatakiwa uizungumzie hiyo sheria,rais namuunga mkono akifuata sheria na akiwa na mdomo miwili kama sasa nampinga mfano(kuwaachia kina babu seya),hii nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria,kuna sheria mbovu nyingi sana na zinahitaji kubadishwa.
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.



" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.
Naam ulisema kweli
 
Back
Top Bottom