Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Ile taasisi ya WAMA itafumbia kinywa hili?

Kama ndiyo hiyo ya Mama Kikwete. Yeye Mama Kikwete alisema wasirudi shule yaani hata leo Mama Kikwete amekumbusha kuwa hata bungeni alikataa hiyo habari ya watoto wa kike kupata mimba, mara wajifungue kisha shule.
 
Mi ningeonelea huyu bingwa angesema hata wale waliofukuzwa shule moja wasiruhusiwe kusoma shule nyingine, na hata kama wapo watu ambao wameshawahi kufukuzwa shule na wakaenda kuendelea mahala pengine basi hawatatambulika kama walisoma shule, kwa sababu tayali walishafukuzwa mahala pengine. Ni mtizamo tu lakini.
 
Sidhani kama aliwahi hata kuwa mwalimu?
Hatujawahi kuwa na mwalimu asiejua mahitaji ya wanafunzi na makandokando yao Hasa wasichana.
Ni wa kumsamehe bure!!!
 
Huyu Jamaa ni role model wangu. Jamaa namkubali 100%. Hajawahi kuniaangusha.

Napenda hotuba zake. Khaaa
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Naamini tunakoenda kuna sababu ya yeye kufanya vile. Issue sio mimba au kuendelea kusoma. Tatizo ni promotions na kufanya jambo hilo kuwa la kawaida. Hata mabwabwa wapo wengi miaka na miaka, tatizo ni ku promote kuwa kutumia Ceptic line its okay.
Na watoto wa kike na wazazi wazembe lazima watishwe kidogo.
 
SAFI SANA MHESHIMIWA RAIS WANGU MARA YA KWANZA NILIKUWA SIONI SABABU YA KUKUOMBEA LAKINI SASA NIMEIPATA KABISAAAAAAA BRAVO SANA SANA NINAJUA WAPO AMBAO WATAKUPINGA LAKINI SIKU ZOTE MJUBE WA KWELI HAKUWAHI KUPOKEWA KWA AMANI NA UPENDO NA UKWELI HUWA HAUPENDWI NA WATU WEWE NI MJUMBE WA KWELI NA KWELI NDIYO UNAYOISEMA NA HAUTAPATA WATU WA KUKUUNGA MKONO LAKINI UHAKIKA NI KWAMBA MUNGU YUKO UPANDE WAKO
 
Hivi mtu akiwa under 18 tunamuhukumu kwa maamuzi yake?
 
Aliyekuambia wakiume ataendelea na shule ni Nani?

Alafu Rais amesema hatasoma serikalini hivyo unaweza mpeleka mtoto private Mkuu.

Jamaa yupo sahihi asilimia Mia moja.
 
Naona mashoga na wabakaji wana tetea utumbo wa ushoga..
Magufuli ni chaguo la Mungu
 
Hawakatazwi kusoma ila hawatasoma shule za umma.
 
Very very True...
Hahaha huyu atakuwa anakula gomba aisee sio ganja,hafai hata kukaa na mgonjwa mana atakufa mapema,hajua kupangilia maneno kwenye mtiririko wenye tafsida
 
Safi nimependa namuombea mungu rais wangu
 
Na wafanyakazi wenye watoto pia kila saa wanatoka kwenda konyonyesha kazi hazifanyiki. Mwambieni Mr. President kila kitu kina mipangilio huyo mwanafunzi aliyejifungua siyo kwamba atarudi muda mchache baada ya kujifungua kwani masomo yatakuwa yamempita atarudi baada ya mwaka maana ata kariri darasa kwa hiyo hapo hamna ruhusa ya konyonyesha. Na pia siyo wote watakao kuwa na uwezo wa kurudi wala asihangaike kuwachimbia mkwala wengine watashindwa maana kuna babysitter.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…