Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Sioni Rais alipokosea na sio kwamba namtetea..he is very right.Ndiyo maana kaweka exceptional waende private.Kupata mimba kwa mwanafunzi wa kike ni kosa.Kwanza kujihusisha katika mapenzi kwa wanafunzi ni kosa.Tusitake kufanya watu wazidi kukiuka maadili eti wakishusha engine warudishwe darasani..haitakuwa na maana na haimfundishi chochote yule mwingine ambaye hakupata mimba aachane na uzinzi.Kwa hali hii watasoma tuu na hawatawaza uzinzi.
Hili nalo neno.Sijawi kufurahishwa sana na hiki kitendo cha binti kupata mimba na baadae arejee shule akishajifungua.Waende tu shule za private.Nahisi uzinzi hautogopwa na hawa watoto kabisa.Ni mtazamo tu.
 
Je kama mwanafunzi alibakwa? Je mwanafunzi akipewa ujauzito na mwalimu? Matineja wengi hawajapevuka kiakili kiasi cha kujua madhara wanayofanya. Si haki kuwanyima fursa adhimu kama ya elimu.
Anasema na ole wake atakae mpa mimba mwanafunzi, ole wake ole wake, kwa hio nae ataadhibiwa, mm napinga wanafunzi kuacha masomo na kuingia katika mapenzi, ikiwa mtoto anaona akifanya ujinga na serikali uka accommodate ule umalaya wake, maadili ndio yanazidi kuporomoka , na ndio sasa itakuwa ni kuzaa nje ya ndoa ni jambo LA kwaida, watoto WA kike wafanye walichofata shule, au wakae mitaani wazae wawapishe wanaotaka kusoma period.
 
Kwa ilo mh rais nimekukubali kwa asilimia 1m.

Ivi vitoto vipo tayari na mimba zao, vinajua uchungu wa kuzaa, vitamsikiliza mwalimu kwa lipi?
 
Mnaopinga kama ni wazazi naomba kuwauliza je mabinti zenu wanapochelewa kurudi nyumbani wakizitafuta mimba nje huwa mnawafungulia milango?
Ni hivi dadaangu, ni kweli wako akina dada ambao wanapata ujauzito kwa uzembe, kwa kuzitafuta, nk. Lakini wapo wengine wengi tu ambao wanapata mimba kwa kubakwa, kwa kudanganywa, kwa matatizo mbalimbali. kinachotakiwa wala siyo hotuba za kibabe kama hizi. huyu binti mjamzito anatakiwa kuwekewa utaratibu maalum. kama tunaona tatizo kumchanganya na wengine, basi wawe na utaratibu wao. cha msingi wasinyimwe haki yao ya Elimu. na kama tuna akili hata kidogo, tutakumbuka ule usemi kwamba UKIMWELIMISHA MAMA UMEELIMISHA JAMII. sasa ukimfungia mlango wa Elimu huyu mama mzazi, huyo mtoto wake je, si umemwadhibu bila kuwa na kosa? maana UKIMNYIMA ELIMU MAMA UMEINYIMA JAMII. Hebu inueni macho mtazame mbele zaidi, msiishie tu hatua chache
 
Mngekuwa walimu, wala msingemlaumu Mh Rais. Kwa kauli hiyo mm sijaona kosa lake hapo. Ni ukweli usiopingika kuwa lazima watoto wetu wazingatie maadili mema hasa wanapokuwa wanafunzi/shuleni. Mtoto akipata mimba in haki asirudi shuleni. Adha inayopatikana huko shule za serikali ni kubwa sana, kufundisha wazazi wenzio ni shida kubwa sana. Hongera mh Rais.
Kama amepata mimba baada ya kubakwa je?
 
Ni kweli maana mtu a sex yeye mimba apate yeye na kaenda shule kusoma au kufanya mapenzi so nimachaguo tuu ukitaka soma kama hutaki zaaa ni uchaguzi wa mtu
 
Pole sana Mama Janet, natambua sana "mzigo" ulionao. Kama raia/mti mbichi umeweza kutendewa hivi, vipi kuhusu wewe/mti mkavu.
 
Watanzania saa nyingine tuwe wakweli, kuna mtu anasomesha wajawazito kweli? jiulize maswali haya kisha nipe majibu
1. Mwezi wa ngapi mtoto mzazi atakatisha masomo yake? (kumbuka ujauzito ni miezi 9)
2. Miezi atakayokuwa shuleni akilea ujauzito wake mchanga, je nini mahusiano yake kati ya walimu na wanafunzi wenzake darasani?

3. Ni mwezi wa ngapi baada ya kujifungua ataruhusiwa kuendelea na masomo yake? kama ni miezi 3 baada ya kujifungua - je atapewa muda wa kuondoka mapema shuleni na kwenda kunyonyesha mtoto? kumbuka kunyonyesha si chini yamiezi 6.

4. Je baada ya likizo ya uzazi, mtoto huyu Mzazi atakuwa na uwezo wa kuyakumbuka aliyofundishwa miaka iliyopita? hasa ukizingatia suala la uzazi si la mchezo - tena mtoto mzazi huyu bado alikuwa hajapevuka - i mean impact ya uzazi itakuwa imemwathiri vipi kisaikojia?

5. Uhusiano wa huyu mtoto mzazi na walimu wake utakuwaje baada ya ku-resume masomo yake; atakubali adhabu zote kama watoto wengine? kuna adhabu zingine hasitakubalika kutokana na uzazi - Wizara itatoa dokezo kwa watoto wa namna hii? Kwa mfano huwezi kumwambia mtu aliyetoka kujifungua miezi 6 ati aruke kichura, akimbie kuzunguka darasa sababu kachelewa nk


6. Je mapokeo kwa wanafunzi wenzake yatakuwaje? kumbukeni age kama hii kuna utani mkubwa - na nakumbuka kuna watoto huwa wanaacha shule sababu ya utani utani kwa mfano: we mama jitahidi darasani kama huwezi kalee mwanao nk

7. Je atakuwa na uwezo wa kuhimili mikiki ya masomo yake huku ana mtoto anahitaji attention yake akifika nyumbani? kuna H/W na kazi ambazo mtoto anahitaji muda kuzifanya akiwa nyumbani - Sitaki kusikia ati Bibi wa mtoto atamsaidia - si kazi yake.


Yapo mengi tu ambayo ukifikiri sana unaona kuruhusu kitu kama hiki hutakuwa umemsaidia huyu mtoto mzazi. Hao wanaharakati watafute njia nyingine ya kuwasaidia hawa watoto lakini si kwa kuwadanganya kwamba wakirudi shule wanaweza kuzikabili changamoto hizo hapo juu.

Kuruhusu jambo hili hamuoni litakuwa kama fungulia mbwa? watoto hawa hawa wanajua zipo kondom madukani tena zingine zinagawiwa bureee, lakini hawapendi kutumia - sasa kuruhusu kitu kama hiki ni kujaza wajawazito mashuleni.

Narudia tena, zile NGO zinazotaka watoto hawa wasome, zinaweza kuanzsiha program maalum nje ya ile ya kawaida ya kuwasaidia - wakija na write-up nzuri basi hata Serikali na sekata binafsi inaweza kusaidia pia.

JPM upo sahihi.
 
Siyo shabiki wake wala wa chama Chake Ila Kwa Hili namuunga mkono kwa 100% Mwanafunzi abaki mwanafunzi na mzazi abaki mzazi warudi shule waliobakwa pekee na kuthibitishwa na Dr na kesi zao kutolewa hukumu Mahakamani kwamba kweli walibakwa, kuwachanganya watoto wetu wadogo na wazazi ni kuwakomaza wanetu Wakiwa wadogo
 
kama alibakwa jee? i think magufuli kwa hili kakosa hekima na nahsi alkua under influence ya mama salma kikwete na hili linaweza pelekea abortion nyingi sana kutokea
 
our no 1,leo amegusia topic muhimu mno ambaye yeye kama kawaida kaiweka kimihemko,please wana JF tujaribu kuidadisi hapa,ni kweli kila mzazi anapenda mtoto wake aelimike shuleni,

mtoto wa kike inapotokea anapata mimba why anaathibiwa yeye tu,maana anafukuzwa shule hadi yule wa kiume aliyempa mimba anaachiwa aendelee na masomo,kwangu huu ni utaratibu dume na unaendeleza ukandamizaji wa watoto wa kike,halafu baadaye tunakuja kupiga kelele ohooo mbona hatuna wasomi wengi wa kike,

kumbe wengi wao wameathiriwa na mfumo dume,solutions watoto wa kike waruhusiwe kuendelea na shule baada ya kuzaa,iandaliwe kampeni nchi nzima ili watoto wa kike wanaopenda wapigwa sindano za kuzuia mimba,na hizi zinatofautiana kutoka mwezi mmoja hadi miezi sita,ila ni lazima kila mmoja kupimwa maana zina side effects kutegemeana na mhusika,condoms zigawiwe bure mashuleni na iandamane na elimu nzuri how to use it safely,

its time noe tabia hii ya kuwafukuza shule only girls ife maana ni ya kibaguzi.
Hiyo mimba kainunua dukani?
1: Kavua pichu kalalia mgongo akaruhusu aingiliwe kupata uroda.
2: Binti kubakwa kuna mazingira aliyatengeneza( kukaa ghetto za wavulana peke yako)
3: Kushinda kwenye masoko, magulio hadi usiku
4: Kudanganywa na vitu vidogo ( simu, chips mitumba(Nguo)
5: Kutokuwasikiliza vizuri wazazi walezi waalimu.
UBAKAJI HAUJI HIVI HIVI TU.
 
Lakini huo mtazamo wa Magu ni mtazamo wa watu wengi pia.

Wewe subiri tu uone maoni ya watu humu....utashangaa!!
Hata mie sipendi binti apate mimba akiwa shule ( sekondari) .Form two ni miaka 16 tamaa ya nini? Unatoa under wear halafu?!
 
Je kama mwanafunzi alibakwa? Je mwanafunzi akipewa ujauzito na mwalimu? Matineja wengi hawajapevuka kiakili kiasi cha kujua madhara wanayofanya. Si haki kuwanyima fursa adhimu kama ya elimu.
Ubakaji isiwe kigezo.
 
tujifunze na sisi kuwa na mambo yetu, na viwango vyetu vya maadili ambavyo tunavisimamia.
NGO na wafadhili wake ambao wengi ni wazungu wasilazimishe kuleta mambo ambayo sisi hatujaona maana yake.
Unazungumzia maadili kwa mtoto wa kike anayetembea zaid ya kilometa 7 kufata shule ? ametoka shule ajala chakula saa nane mchana jua linampiga,anakutana na mtu wa boda boda siku ya kwanza anampakia bure na kumnunulia chips na kumacha,kesho yake hivyo hiyvo kwa watoto wake mtu waaina hyo wanajenga kumpenda automatic.unakuta jamaa hatumii hata nguvu kumpata.atleast serikali ingejenga bweni kila shule ya sekondari arafu ndio waje na hizo kelele zao za kijinga
 
Back
Top Bottom