Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Mkuu, wakiruhusiwa kusoma hao wakiwa na mimba watafanyana sana. Tena wakikamatwa watasema rais aliruhusu.

Watu wengine translation inawasumbua kidogo.
Mkuu,
Ndiyo hivyo yaani hata mambo haya mbona katika familia yapo mzee au walezi wanakataza live kabisa na hakuna hizi porojo!

Rais akisema watu midomo juu Kama filimbi.

Yaani, Tanzania imebadilika sana na wengi wanapotea.
 
Hapa Rais Magufuli umenishangaza, sio Mimi tu dunia nzima. Tanzania haitaendelea hata Aivute na Kamba. Watoto wetu anaowakatalia kuendelea na shule, watavuka mpaka
Kwa shida zao, wakaajiliwe house girl nchi jirani na watoto kama wao ambao serikali yao imewaruhusu kuendelea na elimu. Wabunge na wawakilishi wote wa Watanzania simamieni haki za watoto, hii ni haki mojawapo ya binaadamu, elimu, Magufuli ni Rais wetu lakini hatujamuuzia nchi, Wabunge waamue tupeleke watoto wetu shule. Tuache ukimya, ukimya wetu lazima tutetee haki za Watanzania wote haswa watoto wetu. Kauli ya Rais ni aibu, sio kwetu tu ulimwenguni kote. Serikali ikifanya vizuri tuipongeze, ikifanya vibaya lazima tusimame Pamoja tutetee haki za wanyonge. Mtu akiteuliwa Rais, ni kuwaongoza Watanzania, hatumuzii haki zetu na kodi zetu, Hawalipii hawa watoto ni serikali ya Watanzania. Wabunge mpira uko, kwenu, Rais ama watoto masikini.

http://hakielimu.org/files/publications/Watoto Wetu Waendelee na Shule Baada ya Kujifungua.pdf
 
Lakini sasa katiba inasemaje kuhusu marufuku hii??

mana haya maneno ni matam sana kuyatamka watu wakakupigia makofi.

Angetupa na kumbukumbu ya katiba kwanza kuhusu haki ya elimu kwa kila mtz kama katiba haikuweka wazi alete katiba mpya ili sasa hii iwe ni sheria kwa mujibu wa katiba otherwise hizi porojo tukienda kwa Mahakamani zitakuwa hazina mashiko.

Hujui tafsiri ya sheria ndiyo maana unasema kuhusu Katiba.
Sheria au Katiba ina pande mbili ambazo ni haki (upate elimu ) Wajibu (vigezo vya kutimiza ili upate hiyo elimu).
Na bado kuna bylaws za nchi na taasisi za elimu (shule ).

Kwa hiyo, ukiwa unadai haki yako mahala popote pale kwanza jiulize Kama umetimiza wajibu wako na kuzingatia bylaws zote.

Vinginevyo, unakuwa kilaza na mkurupukaji.
 
tujifunze na sisi kuwa na mambo yetu, na viwango vyetu vya maadili ambavyo tunavisimamia.
NGO na wafadhili wake ambao wengi ni wazungu wasilazimishe kuleta mambo ambayo sisi hatujaona maana yake.

Wazungu hawajafundisha watoto kupata mimba shuleni, wala hawatulelei watoto wetu, mzazi anamwacha mtoto na house girl, baba mlevi, familia hazina maadili, hali ngumu ya uchumi hairuhusu wazazi kuwapatia watoto mahitaji muhimu, wazazi wenyewe hawana elimu ya kutosha kwa hiyo kwa hiyo hawawezi kuwapa elimu ya uzazi watoto wao, jamii nzima imevurugika kwa umaskini...leo hii tuna mzuia mtoto wa kike kurudi shule, hapo aliyemtia uja uzito ama yupo shule pia ama hana kipato cha kueleweka ama kakataa ujauzito ule. Mtoto ambaye hana kosa lolote anazaliwa kwenye umaskini , hapo tutakuwa tume tatua matatizo au kuyaongeza?

Sio kila kitu tusingizie wazungu, hili tatizo ni ishara ya mapungufu mengi serikalini na kwenye jamii
 
Sometimes mwanamke kabakwa wengine ni mazingira magum ndo yanawapelekea kuingia kwenye vishawish
Malezi mabaya , wazazi na watu wazima kwenye jamii wanalikoroga halafu wanampa binti alinywe peke yake, hata kijana aliyemtia mimba haguswi....binti kupata mimba ni matokeo ya makosa ya watu wazima wengi tu walio kwenye maisha yake na maisha ya mtu aliyemtia mimba.
 
Lakini huo mtazamo wa Magu ni mtazamo wa watu wengi pia.

Wewe subiri tu uone maoni ya watu humu....utashangaa!!

You are right, yaani comments nyingine nasoma hadi napata kizungu zungu....huyo binti anayenyimwa kuendelea na shule anategemewa kumlea mwanaye hadi akue.....! akianza kuchuna mabuzi anabatizwa jina jipya "Malaya"
 
Wanaowapa watasomeshwa gerezani miaka 30?

Watalima mazao huko na wakija kutoka...

Na mafisadi kasema wapewe kazi ya kulima... ili na wao wazalishe kwa jasho lao

Magu anaongea baba huyo eeeeeh

Ya ng'ombe na kondoo ha ha ha haaa
 
Ni kweli maana mtu a sex yeye mimba apate yeye na kaenda shule kusoma au kufanya mapenzi so nimachaguo tuu ukitaka soma kama hutaki zaaa ni uchaguzi wa mtu
Aya ikitokea umebakwa ukapata mimba inakuwaje apo kwa upande wako
 
Swala La Kubaka Hlo Linajulikana, Na Taratibu Zitafwatwa. Mf. Akifanywa Kwa Nguvu Au Na Mwalimu Au Mlezi, Hyo Ni Police Kesi Na Dawati La Jinsia Lipo. Lkn Hii Michezo Wanayofanya Wanafunz Cku Hz Ya Kujiuza Kwa Madereva Af Et Magu Awarudishe Shule! Swala Et Mzazi Hausiki Hlo Co Kweli, Walio Wengi Hawana Time, Watoto Wamechagua Mapenz Kuliko Elimu Af Wabembelezwe Kusoma? Mtoto Anatakiwa Aanze Kupenda Shule Akiwa Std6 Had Form Two, Lkn Ndo Wanakuwa Wehu, Ss Unataka Wasome Lini? Tukisingizia Umackini Tutakua Tunakosea Maana Familia Nyingi Mackin Zmesomesha Watoto Wa Kike. Na Hz Shule Za Kata Watoto Wamezagaa Huku Na Huko Wana Tamaa Za Chips, Smartphones, Shule Zpo Kla Kata Lkn Wanataka Kupanda Boda Boda, Je Wangesoma Miaka Ya Nyerere? Tulee Watoto We2 Tuwakunje Wangali Wabich, Tucwaachie Waalimu Pekee. Magufuli Ameshaliona Hli, Watoto Wanacheza2 Mashuleni Wanasubr Kengele Waende Kubanduana. Mbona Wapo Ambao Wanabidii Ya Kusoma? Kwan Wao Hawataman Mapenzi? Maranyingi Wanawaona Wenzao Mafala Na Wao Wajanja.
 
Hujui tafsiri ya sheria ndiyo maana unasema kuhusu Katiba.
Sheria au Katiba ina pande mbili ambazo ni haki (upate elimu ) Wajibu (vigezo vya kutimiza ili upate hiyo elimu).
Na bado kuna bylaws za nchi na taasisi za elimu (shule ).

Kwa hiyo, ukiwa unadai haki yako mahala popote pale kwanza jiulize Kama umetimiza wajibu wako na kuzingatia bylaws zote.

Vinginevyo, unakuwa kilaza na mkurupukaji.

yawezekana wewe ndio kilaza zaidi., baylaws ni sheria za kujitungia tu unlala asubuhi unaleta wazo liwe sheria ikitokea umeenda mahakamani katiba Inazungumzia jambo lile mahakamani hutaweza kuleta baylaws na ikaweza kusimama kama sheria.

Ndio mana saiv mumeleta baylaws kupiga marufuku mikutano ya siasa wakati katiba ya nchi inaruhusu. Mukishatamburikiwa kila siku mnaleta sheria mpya tu hamjali kama munavunja katiba.
 
yawezekana wewe ndio kilaza zaidi., baylaws ni sheria za kujitungia tu unlala asubuhi unaleta wazo liwe sheria ikitokea umeenda mahakamani katiba Inazungumzia jambo lile mahakamani hutaweza kuleta baylaws na ikaweza kusimama kama sheria.

Ndio mana saiv mumeleta baylaws kupiga marufuku mikutano ya siasa wakati katiba ya nchi inaruhusu. Mukishatamburikiwa kila siku mnaleta sheria mpya tu hamjali kama munavunja katiba.

Usiwe kihiyo na gulagula nimesema pana Katiba inaonesha haki kisha na wajibu.

Supplement nikakutolea bylaws Kama mifano midogo.
Sasa kwa sababu, akili huna unachukua supplement kutaka kufanya replacement ya Katiba

I rest the case. Keep believing your failure thoughts...
Truly, arguing with a Zygote will lead to Harvest nothing!!
 
Kwa mtazamo wangu naona kaongea kitu kizuri sana mbele ya jamii ambayo kabla ya kuruhusiwa mwanafunzi kusoma baada ya kujifungua wanazibeba kweli kweli izo mimba je wakiruhusiwa unazdhani itakuwaje? Ndio watazibeba kweli kweli
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

"Kama kweli"?
 
Huu mfano wa kuonesha kuwa ushoga ni kinyume na uasilia wa viumbe hai hauna tatizo na hamna njia ya kiungwana ya kuelezea tabia chafu kama hii.
 
Back
Top Bottom