Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

HII KAULI ITAWAAHUSU WATOTO WA MASIKINI AMBAO MKUBWA KILA KUKICHA ANASEMA YEYE YUKO KWA AJILI YA KUWASAIDIA. MTOTO WA MWENYE NAZO AKISHAJIFUNGUA ATAMPELEKA PRIVATE SCHOOL. Napenda kumjulisha Rais wangu kwamba sio wote waliopata mimba wanapenda, ELIMU NI HAKI KWA KILA MTOTO, haijalishi hali yake.
 
Mnyongwa anyongwe,ila haki yake izingatiwe,au ndo zile kunya anye kuku,bata kajinyeaa!!!
 
Atakayefanya kama alivyosema RAIS atakuwa MZAZI mpumbavu.Kuna shule za private,kama anauwezo ampeleke mtoto wake private.

Huu ujinga ati mtoto sababu amepata Mimba asisome aupeleke Lumumba na Chato
Samahani sana kama mwanao tayari anamimba mpeleke evening class wao hawabagui hata ukiwa na mapacha wanakuchukua tu
 
tujifunze na sisi kuwa na mambo yetu, na viwango vyetu vya maadili ambavyo tunavisimamia.
NGO na wafadhili wake ambao wengi ni wazungu wasilazimishe kuleta mambo ambayo sisi hatujaona maana yake.
Sema wewe hujaona maana yake siyo sisi! Wewe unaona ni haki mtoto akipata ujauzito asirudi shule? Kwanini anyimwe haki yake ya kikatiba ya kupata elimu, kwanini apewe adhabu mara mbili. Halafu hujui tu hii ni kwa ajili ya watoto wa masikini wanaotegemea shule za serikali
 
Kauli zake zinapingana na maono yake....maono ni kujenga tanzania ya viwanda...kauli na matendo ni kuendeleza ujinga...unapowanyima watoto wa kike another chance...an oppurrunity to correct their mistakes...wao wenyewe watakuwa hawana elimu na watoto wao pia watawambukiza huo ujinga..miaka kumi yake atatuachia taifa la wajinga..
 
Na aina ya watu wanaozaa sanasana ni vijijini huko familia duni ambao ndo wapiga kura wake majority.Bottom line namsupport kwa hili ule mchezo sio wa kuuendekeza
 
Samahani sana kama mwanao tayari anamimba mpeleke evening class wao hawabagui hata ukiwa na mapacha wanakuchukua tu

Mimi siyo Mpumbavu,nina jua nini Maana ya HAKI ya BINTI.Unapomkataza binti kupata ELIMU unalififisha TAIFA.Pili msijiongelee nyinyi,umimi tuuache ,kuna watoto wa maskini wanaopata mimba si kwa kupendabali ufukara walio nao.

Mtoto wa waziri wakimpa mimba mtoto wa mkulima/mfugaji asubuhi atatoroshwa na ndege kwenda ughaibuni,umemfikiria mtoto wa mfugaji/mkulima akimpa mtoto wa waziri mimba anaishia wapi??

AKilini mwetu tufikiria zaidi ya umimi,kuna wenzetu wanahitaji kusemewa!
 
sipati picha mwalimu amejaziwa wamama darasani eti anawafundisha huku yeye mwenyewe hajawahi kupata mtoto, badala ya kuwa ticha yeye ndio inabidi aombe shule kwao, labda ianzishwe shule maalum kwa wote wababa na wamama ambapo watakuwa free muda wowote akitaka kungonoka inakuwa ruksa akipata mimba anazaa akimaliza anarudi shule hata akiamua kubeba mimba ya 1, 2,3,4 na kuendelea ila walimu wake muwe ninyi mnaounga mkono wazazi kusoma na nyie muone kazi maana mnadhani ualimu ni kama kupiga porojo kama hizi mnazopiga humu jf
 
Anaweza kuwa na nia njema lakini kwa jinsi anavyolikabili hili tatizo kakosea
1. Uwelewa wa hawa watoto wanaotiwa ujauzito ni mdogo sana, naweza kusema wengi wao hurubuniwa tu.
2. Watoto wenye wazazi wenye uwezo, watajifungua na kurudi shule (Private) watoto wa walala hoi ndio watakuwa wameshaharibiwa maisha.
3. Wasababishi wa haya matatizo (wanaume) bado hawabanwi.
4. Sasa sijui anaanda Taifa la aina gani la baadae.
5. Hivi hana mtu wa kumuandikia speech, yani huwa anaongeaga maneno mepesi mepesi kwenye mambo mazito eg: "....Mwisho utakuta darasa la kwanza wote wanawahi kunyonyesha maana huo mchezo ni mtamu, kila mtu anaupenda..."
6. Kosa moja, adhabu ya maisha.
7. Na ilani yake ya ccm alisema watoto watakaopata ujauzito mashuleni, wataendelea na masomo baada ya kujifungua.

NB:Maendeleo ya nchi kwa Rais kama huyu, tutasubiri sana, Labda Yesu ashuke.
 
Namuunga mkobo na mguu, Serikali isisomeshe wazazi, wazazi watumie mifumo mingine iliyopo kujiendeleza ki - elimu. Ipo Ngumbaru, Qt's, Private schools waende huko. Walipe malipo ndio adhabu ya kosa la kuchezea nafasi waliyopewa.
 
Wakati tunampongeza Rais, lazima tuangalie yale mambo ambayo tunampongeza. Isiwe tu kumpongeza kwa sababu yeye ni Rais, lazima asahihishwe jamani. Anachokisema Rais ni kinyume kabisa na mikataba/maazimio ya umoja wa mataifa ambayo sisi tumeisaini.

Article 26.

(1) Everyone has the right to education. Education shall be free, at least in the elementary and fundamental stages. Elementary education shall be compulsory. Technical and professional education shall be made generally available and higher education shall be equally accessible to all on the basis of merit.
(2) Education shall be directed to the full development of the human personality and to the strengthening of respect for human rights and fundamental freedoms. It shall promote understanding, tolerance and friendship among all nations, racial or religious groups, and shall further the activities of the United Nations for the maintenance of peace.
(3) Parents have a prior right to choose the kind of education that shall be given to their children.
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.

Taifa lazima Liwe na sheria tena zile ambazo kama Taifa litajuvunia. Mimba za utotoni sio maadili yetu .huku wazungu sio wanapata mimba hizo utotoni unadhani ni Serikali. Familia. Long lived traditions. Nk wee kazana kutetea ujinga
 
Back
Top Bottom