Rais Magufuli, tafadhali mpeni Tundu Lissu ushirikiano, msaidieni atulie na baada ya uchaguzi ndio kesi zake ziendelee

Natambua mantiki ya hoja yako lakini tambua hii nchi inaongozwa kwa mihemko na sio kwa mujibu wa sheria na katiba!

Ndio maana kwa kutambua udhaifu wa kutofuata sheria watawala wanajitungia sheria zitakazo wapa kinga pindi waondokapo madarakani!
Hahah Malawi/Sudan wote walijitungia Sheria kama hizo lkn sasa hivi hao viongozi wako wananyooshwa kwa uzuri kabisa.
 
Raisi Nyerere alipomsamehe yule Mgiriki aliyesema serikali yake iko mfukoni mwake alikuwa anatumia katiba au sheria gani? Si ni katiba hii hii aliyotuachia muanzilishi wa aina hii ya serikalini tuliyonayo au ?
 
Uhalifu huwa hauhusiani na kutia nia.
Huwezi omba excuse kuwa kwa kuwa nagombea msinikamate kwa makosa niliyofanya kabla ya kutangaza nia hakuna.

Akikanyaga tu nchini ni segerea hakuna majadiliano ni yeye tu kujiandaa kisaikolojia
Nakuona makonda unaendelea kupanga njama zako za kummaliza Lissu
 
two wrongs do not make it right YEHODAYA
 
Nakuona makonda unaendelea kupanga njama zako za kummaliza Lissu
Hivi Kumbe YEHODAYA ni makonda... chondechinde kaka, usimalizie hasira zako za kigamboni kwa Lisu, duniani tunapita tu kama ulivyopita kwenye mchujo pale Kigamboni na maiha yanaendelea kama kawa...
 
Hivi Kumbe YEHODAYA ni makonda... chondechinde kaka, usimalizie hasira zako za kigamboni kwa Lisu, duniani tunapita tu kama ulivyopita kwenye mchujo pale Kigamboni na maiha yanaendelea kama kawa...
Yehodaya ni Makonda mwenyewe. Hiyo id inahudiwa na makonda na vijana wake.

We fuatilia posts na thread za iyo id baada ya kura za maoni kigamboni utapata picha
 
Acheni tu wamkamate kwani hilo linaongeza uzito upande mmoja kwa jahazi kuelekea kupinduka. Najua wakati fulani itabidi watz tufanye kitu dhidi ya udhalimu huu. Nina uhakika mwisho hautakuwa mzuri kwake kama ilivyokuwa kwa viongozi wengi waliotumia nguvu, mifano ni mingi sana.
HAKUNA wa kumtegema mwanadamu mwenzie, sote tu mavumbi na mavumbini tutarudi- haina haja ya kutunishiana misuri iloihali sote twarudi mavumbini na JPJP hana cha kupoteza hata kama atakuwa Raisi wa awamu moja
Lissu ni level ndogo kwa raisi kuhangaika naye, msafiri mmoja kurudi nyumbani haimsumbui rais. Waambie walio level ya kiprotokali na Mwananchi/raia Lissu.
Rais ana majukumu makubwa kushugulika na Lissu.
Kweli ila akimuweka ndani ntaamini kuwa mzee magu muoga sana .
 

Tundu Lissu kama kweli anarudi Tanzania basi anakaribishwa nyumbani kwake ambako ndiko alikozaliwa.

Huko nje wote tunarukaruka tu lakini mwisho wa siku Tanzania ndo nyumbani.

Msitafute sababu kwa kumhusisha raisi kwenye hili.

Tundu Lissu mwenyewe hamtambui raisi Magufuli iweje leo aanze kelele za kumwomba hili na lile?

Kama ana kesi za kujibu ambazo bado zio "pending" basi arudi tu hakuna namna.

Chadema waandae utaratibu wa kumpokea na kumsindikiza nyumbani kwake atakapofikia.

Hilo ni jukumu la Chadema na si watu wengine.
 

Sijaelewa uko radhi JPM aingilie uhuru wa mahakama
 
Kanisa katoliki linaruhusu ndoa za mitala au mtu akiwa na title basi ya sheria za kanisani hazi apply kwake ?
 
Kipanga, for the sake of public and national interest, wamuacheーーkila mtu Ana jua muumba alivyo muokoa toka tundu la mauti
 
Kanisa katoliki linaruhusu ndoa za mitala au mtu akiwa na title basi ya sheria za kanisani hazi apply kwake ?
Muhimiri ulio jichimbia sana sehemu zote wewe unauzungumziaje ndugu yangu?
 
Lissu ni level ndogo kwa raisi kuhangaika naye, msafiri mmoja kurudi nyumbani haimsumbui rais. Waambie walio level ya kiprotokali na Mwananchi/raia Lissu.
Rais ana majukumu makubwa kushugulika na Lissu.
Wambie waache kumwinda maana inaonekana wanakusikiliza kama ni level ndogo mwacheni awe huru kufanya siasa
 


Yaani kitendo cha kuwaomba hivi serikali ni kuonyesha hatuna uhuru. Jiulize hizo kesho zinamisingi gani ya maana. Yaani ukisema Raisi mjinga ni kesi moja, ukisema Raisi ni dikteta uchwara ni kesi ya pili, ..... Kama yote aliyokuwa anasema sio ya kweli kwanini alipigwa risasi! na mpaka namba ya gari lililokuwa linamfuata aliwaambia Polisi
 
Kama ana kesi ya kujibu akamatwe tu hakuna double standard.
Kuna ndugu zetu nao wana kesi kipindi hiki cha kuchagua viongozi wawapendao la sivyo kesi zao zisimame au waachiwe huru kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…