Rais Magufuli, tafadhali mpeni Tundu Lissu ushirikiano, msaidieni atulie na baada ya uchaguzi ndio kesi zake ziendelee

Rais Magufuli, tafadhali mpeni Tundu Lissu ushirikiano, msaidieni atulie na baada ya uchaguzi ndio kesi zake ziendelee

SUALA LA TUNDU LISSU NI KIPIMO TOSHA CHA BUSARA ZA RAISI NA DOUBLE STANDARD ZA KIMAHAKAMA KATIKA MUKTADHA WA KUWA WOTE SAWA KWENYE USO WA SHERIA!

NB;
KAMA LISSU ANA KESI YA KUJIBU KWA MUJIBU WA SHERIA BASI SHERIA IFUATE MKONDO WAKE!
Mkuu unaongea nini mahakama haihusiani na Mambo ya siasa.
Iache mahakama ifanye kazi yake mtu akamatwe ajieleze kama aliapa bungeni alafu baadaye akavunja kiapo chake inatakiwa akamatwe.
 
Mimi sishauriwi..... na ukishauri dno umeharibu kabisaaa!
matendo yako yatashuhudiwa na yule aliye juu yako, na sisi wakazi wa muda hapa duniani tutayaona unavyo dhihaki mwenye huruma kuu unayemuomba usiku na mchana kutwa - maombi mbalimbali
 
sidhani kama unapenda vurugu mechi ndugu yangu... vyovyote viwavyo, aachwe tu hadi uchaguzi, hata kama hajaomba msamaha, sijatumwa ila kwa niaba yake, afikiriwe tu kama Yesu alivyomfikiria yule mwizi mwingine wa msalabani kwa hadi ya wote kuwa peponi siku ile...
Kwani LISSU ni raia wa aina gani tofauti na raia wengine wanaoendelea na kesi zao kwa mujibu wa sheria?
 
sidhani kama unapenda vurugu mechi ndugu yangu... vyovyote viwavyo, aachwe tu hadi uchaguzi, hata kama hajaomba msamaha, sijatumwa ila kwa niaba yake, afikiriwe tu kama Yesu alivyomfikiria yule mwizi mwingine wa msalabani kwa hadi ya wote kuwa peponi siku ile...
Magufuli sio Yesu acha kuwafananisha.Ya YESU yalikuwa yake.Ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe MUNGU
Ya kaisari yanataka Lisu akitua tu akamatwe apelekwe Segerea ya Yesu yanasema leo hii tutakuwa wote mbinguni!!
 
Kesi Lisu anazo kibao za kumtosha tu.Kwa Lisu sio busara zinahitajika sababu kesi zake ziko mahakamani.Ni sheria kufuata mkondo wake, sio busara kufuata mkondo wake!!!!
sawa, but- mahakama zinajua kwamba alikuwa huko nje kwa matibabu- na wamuache atie nia halafu baada ya uchaguzi ndio waanze kuitisha faili zake
 
Mkuu unaongea nini mahakama haihusiani na Mambo ya siasa.
Iache mahakama ifanye kazi yake mtu akamatwe ajieleze kama aliapa bungeni alafu baadaye akavunja kiapo chake inatakiwa akamatwe.
Natambua mantiki ya hoja yako lakini tambua hii nchi inaongozwa kwa mihemko na sio kwa mujibu wa sheria na katiba!

Ndio maana kwa kutambua udhaifu wa kutofuata sheria watawala wanajitungia sheria zitakazo wapa kinga pindi waondokapo madarakani!
 
Magufuli sio Yesu acha kuwafananisha.Ya YESU yalikuwa yake.Ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe MUNGU
Ya kaisari yanataka Lisu akitua tu akamatwe apelekwe Segerea ya Yesu yanasema leo hii tutakuwa wote mbinguni!!
Simfananishi JPM na Yesu... yeye mwenyewe kwa kimya chake huwa anawaombea watu misamaha , hata Kinana juzi kati alisisamehewa, iweje Lissu aliyeponea Risasi?
 
msaliti ni mamaako...TL ameeleza ukweli kwa yale yaliomtokea
Hivi wewe unaakili au unafikiri kwa kutumia makalio, hivi TL alizungumza aliyotendewa tu, hatusahau sie alivyoenda akasababisha ndege zetu zikamatwe na ujue ndege zile ni kodi yetu wananchi acha utani wako.
 
sawa, but- mahakama zinajua kwamba alikuwa huko nje kwa matibabu- na wamuache atie nia halafu baada ya uchaguzi ndio waanze kuitisha faili zake
Zinajua wapi kwa ushahidi upi? ulishawahi iona medical report ya daktari ya Tundu LISU Ikionyeshwa mahakamani? Mahakama ilijulia wapi kuwa Lisu yuko kwenye matibabu? Ushahidi pekee ni DOCTORS MEDICAL REPORT Si vinginevyo

.Weka hapa hiyo medical report ya kuonyesha miaka yote hiyo hadi tarehe anarudi alikuwa yuko tu akitibiwa!!!!
 
Uhalifu Uhusiane AU USIHUSIANE na kutia nia; Akikanyaga au Asikanyage; ajiandae kisaikolojia au la, ni maoni yangu mimi pangu pakavu tia mchuzi... figusu afanyiwe baada ya uchaguzi... kuchafukiwa au kuchafuliwa wakati huu wa uchaguzi hatutaki kama wana familia wa nyumba yetu sote Tanzania
Baada ya uchaguzi Lissu atakuwa Rais wetu, nani atathubutu kumfanyia figisufigusu? Au hamuamini Kama mgombea wenu atashinda?
 
Hivi wewe unaakili au unafikiri kwa kutumia makalio, hivi TL alizungumza aliyotendewa tu, hatusahau sie alivyoenda akasababisha ndege zetu zikamatwe na ujue ndege zile ni kodi yetu wananchi acha utani wako.
Ngoja tu huyo TUNDU lisu Arudi ndipo ataijua vizuri Tanzania aliyoiacha miaka hii ambayo hakuweko mjinga mkubwa

Wapambe wake wamweleze LIve bila kumeza maneno kuwa yeye hakujali kuchafua nchi na sisi watanzania kama kuchafuka alishatuchafua sana we have nothing to loose or to reverse akifika zamu yetu sisi kushughulika na yeye.Kama vile ambayo yeye alikuwa hajali haogopi yeyote ndani ya nchi au nje ya nchi kufanya aliyofanya na sisi hatujali hatuogopi yeyote na chochote tutakula naye sahani moja aje tu tunamngoja kwa hamu
 
Uhalifu huwa hauhusiani na kutia nia.
Huwezi omba excuse kuwa kwa kuwa nagombea msinikamate kwa makosa niliyofanya kabla ya kutangaza nia hakuna.

Akikanyaga tu nchini ni segerea hakuna majadiliano ni yeye tu kujiandaa kisaikolojia
Ni vema muda mwingine ungekuwa unawaacha kwanza wenye akilini tomami na uelewa mkubwa wajadiliane kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafadhali sana mheshimiwa sana, Raisi wetu, Dkt. Magufuli, yahusu huyu Tundu Lissu atakaporudi nyumbani Tanzania. Kama kweli alikuwa msaliti, ni Mungu tu ajuaye na ni Mungu tu aliye hakimu wa haki.

Mheshimiwa sana, wewe ni Mkatoliki na pia mseminari, waijua vema hadithi ya mwana mpotevu na kondoo aliyepotea.

Tundu Lissu ni Mtanzania kama wewe, baba, kaka na mtoto wa familia Tanzania yetu wewe. Hotuba yako (Uchaguzi House) ya leo 22/07/2020 nimependa na iwe ya kweli kwa vitendo.

Tafadhali, chondechonde, akirudi huyo (Tundu Lissu) Jumatatu, muacheni arudi kwa style yake, afanye anayotaka kufanya bila kuvunja sheria. Hakuna haja ya kutunishiana misuri kwa sasa, muacheni aje, kama figusu, mfanyieni baada ya uchaguzi na sio sasa. Tutachafuka na kuchafuana sote, nyumba yetu sote (Tanzania) itanuka, mpeni Tundu Lissu ushirikiano, msaidieni atulie na baada ya uchaguzi ndio kesi zake ziendelee au figisu zozote.

Mheshimiwa sana Rais Magufuli, kama umesoma, umesomea au kutaarifiwa. Ni hayo tu yangu. Nyumba Tanzania ni yetu sote. Bila matusi au mkwaruzo tuwe kama nguchiro na Mchwa, nyumba moja bila mkwaruzano.

Ni hayo tu kwa leo. Ubarikiwe na Uongozwe kwa niaba aliye juu na amri ya uhai wako kwake.
Wewe mleta uzi unatumia sheria za nchi gani? Yaani unamuelekeza Rais wa Nchi aingilie uhuru wa Mahakama? Wote waliopo mahabusu kwa kesi hukuwaona bali umemuona huyo Lissu tu? Basi na hao mahabusu waachiwe hadi uchaguzi uishe ndo wakamatwe tena na kuendelea na kesi zao.
 
KWANINI VIONGOZI WANAOJINASIBU KUABUDU DEMOKRASIA WANABAKA KATIBA ZAO NA KUONDOA UKOMO WA MADARAKA!?

CCM KUMEOZA NA UPINZANI KUNATOA FUNZA!
Safi sana aisee sikua nimejua kumbe ofisi za Msajili wa vyama vya siasa zimeshindwa kudhibiti hilo?Lkn lnaweza kutishia kuvifuta vyama hivyo vinapoleta upinzani mkali sio?
 
Baada ya uchaguzi Lissu atakuwa Rais wetu, nani atathubutu kumfanyia figisufigusu? Au hamuamini Kama mgombea wenu atashinda?
Tunaamini Hashimu Rungwe atakua rais.
 
Back
Top Bottom