Rais Magufuli, tafadhali mtumbue Harrison Mwakyembe, wizara upande wa michezo imemshinda

Rais Magufuli, tafadhali mtumbue Harrison Mwakyembe, wizara upande wa michezo imemshinda

Naunga mkono hoja ajiuzuru kabisa, wenzake wanashindana kuleta wawekezaji kwenye wizara zao yeye anashindana kufukuza wawekezaji, JPM fukuza huyu waziri bana
 
Kwa kweli maoni ya Wazir hayakubaliki, yaani timu zimejikongoja miaka yote hata viwanja vya mazoezi hazina Leo wanabadilisha uendeshaji wanakwamishwa, kwani serikali inazisaidia nn hizi team zetu?
 
Wameua hata umiseta tu kazi kukomalia maendeleo ya wenzake tu. Hili jamaa halafu linaongea kwa base kama linaongea cha maana kumbe hakuna kitu
 
Simba na Yanga wamiliki ni Chama pendwa ikitokea mtu kawa na nguvu kwenye hizi timu anakua anatishia uhai wa uwepo wa chama pendwa ndio maana yanga ikiwa sawa jua simba kuna shida pia simba ikiwa poa upande wa pili kuna jambo hakuna mwaka zote zitakua sawa keep in your mind ndugu
 
Hata upande wa habari kashindwa kabisa, magazeti yanachapisha waraka wa kumvuruga raisi yeye waziri yupo yupo tu. Huyu waziri ni kimeo kabisa. Wizara zote kashindwa. Anafaa akalime viazi kwao
 
Wizara zenye upekee kama hizi zinatakiwa ataeuliwe waziri mwenye uelewa mzr wa mpira wa miguu na michezo yote kwa ujumla wake, siasa inatakiwa ziwe kidogo sana anapodeal na mambo kama haya.

Katika kauli zote tatu au nne alizotoa katika nyakati tofauti tofauti, sijaelewa hata moja kwakweli, na sina hakika kama hata yeye mwenyewe anaelewa anachokiongea.
 
Ila huyu mzee walimuonea kumueka kuwa waziri wa michezo, sijaona umuhimu wake kwakweli, yaani hana mawazo kabsa
 
Huyu mzee katumwa na shetani kweli,hivi kama timu imetulia na hamna vurugu ye tatizo lake ni nini,shame on him
 
Serikali imejifunza kwa Moisse Katumbi, haitoweza kufanya huo ujinga,.. Pambaneni na hali zenu...
 
Serikali inaogopa mtu mmoja kuwa popular kuliko wengine, kisiasa huo ni mtaji mkubwa sana! Kwenye taifa masikini linalopatikana pembezoni mwa bahari ya Hindi, ni vigumu sana kwa wenye uchu wa madaraka kumwachia mtu mmoja kuwa popular kiasi kikubwa kama ilivyoshuhudiwa miezi kadhaa iliyopita huko kwenye uwanja uliojengwa kwenye utawala wa mzee aliyetoka kijijini lupaso...
Kumlaumu mtu mmoja kwenye suala kama hilo ni sawa na kumpapasa mtu aliyekupiga konde zito.
Mwisho wa siku " politics " ogopa sana kitu inaitwa politics, siasa, siasa, siasa+ uchu wa madaraka + ugali ugali + tamaa tamaa tamaa.
 
Kwa kitendo ulichofanya cha kutaka kuihujumu timu yetu ya simba tunasema hatuna imani na wewe tena kwenye mpira wa miguu. Hii timu ya simba sio timu ya serikali bali ina wanachama wake ambao wanafanya maamuzi juu ya klabu. Na sisi ndio wanachama ambao tumeamua kumpa timu Mo Dewji na ametusaidia kufika robo fainali africa mpaka kusaidia Tanzania kuingiza timu nne mashindano ya africa lakini hilo hulioni. Tunakuomba ujiuzulu mapema kabla hatujafanya maandamano ya kukupinga hadharani.
Nawasilisha.

Kama hisa 49 ziwe na watu wa tatu hivi anadhan hao wawekezaji wako rahisi hivyo kupatikana? Ingekuwa easy hivyo si korosho zote zingekuwa zimenunuliwa,? So simba na Yanga ziwe na wawekezaji sita? Watatoka wapi?
 
Back
Top Bottom