Rais Magufuli tafakari hili haraka sana, Wapambe wanakudanganya

mangikule

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2012
Posts
6,468
Reaction score
6,022
Nimeiona hii kwenye mitandao ya kijamii yakanifikirisha sana!

Nimekuwa nikitafakari sana utendaji wa rais wangu na wanaomzunguka! Ukweli kwa mtizamo wa haraka haraka utapenda namna unavyojinasibu kuwaweka wakoloni wa zamani katika kikaango! Nimetafakari nia nzuri za kina Gadaffi na Sadam Hussein na jinsi raia walivyodanganywa, hadi kuwatoa kafara!

Nimetafakari hayo yote nikajiaminisha kuwa wewe rais wangu unaweza kuwa na nia njema sana lakini hao wanaokuzunguka wakakuharibia. Na hii haijaanza leo! Kipindi cha Nyerere wakati yeye anatekeleza siasa ya ujamaa na kujitegemea kwa vitendo wapo waliojificha kwenye kivuli hicho huku wakiwa na agenda ya uroho wao na tunawafahamu wapo hadi sasa.

Rais wangu jitenge haraka sana na watu wasiokutakia mema! ili kuondoa fursa ya wakoloni wa zamani kutumia watanzania kukuumiza! Hili ni kosa la akina Guadhafi na Saadam walilofanya! Kutengeneza kakikundi aminifu kilichokuwa kinafaidi.

Jitenge na Makonda haraka sana! Jitenge na Ndugai haraka sana! Jitenge na AG haraka sana! Jitenge na wapiga debe hawa ambao nawaona ni kama mbwa koko waharibifu tu. Fanya haraka uepuka haya ya Malawi yanayokuja! Akina Sirro watakutosa trust me! Mabeyo ni mwoga na hana support ya TPDF trust.

MALAWI: RAIS LAZARUS CHAKWERA AMUONDOLEA KINGA YA KUTOSHTAKIWA RAIS WA ZAMANI PETER MUTHARIKA, AMFUTA KAZI MKUU WA POLISI

> Saa 24 tangu ashike madaraka, Chakwera amemuondolea kinga ya kutoshtakiwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Peter Mutharika
> Pia, amemfuta kazi Mkuu wa Polisi ambaye atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya utesaji na mauaji yanayomkabili. Wakati wa maandamano ya kupinga ushindi batili wa Rais Mutharika Mkuu huyu wa Polisi ndiye aliyekuwa "Maliyamungu" wa Rais Mutharika akiamuru polisi wawakamate waandamanaji, wawatese na hata kuwaua kwa mateso na risasi. Rais Chakwera pia amewataka Mawaziri kurudisha mali za Serikali walizoiba ndani ya saa 72 kisha washtakiwe na waliohujumu uchumi wafilisiwe.

NOTE: 1. Huu ni ujumbe mahsusi kwa Viongozi wanaopambana kujiwekea kinga za kutoshitakiwa. Mfahamu tu kuwa kinga hizo sio za milele siku mkiondolewa madarakani hakuna guarantee kuwa hizo kinga zitaendelea kuwepo pengine muombe Mungu mufe upesi kabla ya kufurushwa madarakani. Chama kingine kitaposhika hatamu huenda hizo kinga zikafutiliwa mbali na mkawa wenyeji wa mahakamani na hatimaye gerezani au kunyongwa hadi kufa sambamba na kufilisiwa.

2. Hapa kuna ujumbe unatumwa kwa wakuu wa Polisi pamoja na Polisi kwa ujumla. Wakati Mkuu wa majeshi wa Malawi akiamuru Jeshi liwalinde waandamanaji na kuwakabili Polisi wanaowapiga na kuwaua waandamanaji, Mkuu wa Polisi wa Malawi yeye alikuwa bize kuamrisha Polisi wawapigie waandamanaji kipigo cha MBWA KOKO hadi wachakae. Mkuu huyu wa Polisi alifanya haya ili kumfurahisha Rais Mutharika ili alinde MATUMBO yake ilihali akijua ni kukiuka Katiba na kinyume cha maadili ya kipolisi.

Wale polisi mnaotumiwa vibaya na watawala barani Afrika endeleeni tu kuwafurahisha wateule wenu ila mjue hawatokuwa madarakani milele.

Wahenga walisema mwenzako akinyolewa wewe zako tia maji.

Hili ni somo jengine kutoka Malawi sijui kama nchi ya KUSADIKIKA imejifunza chochote hapa. Wacha nimalizie riwaya pendwa ya "Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe" kabla ya kuanza kusoma "Mfalme Juha".

Nini maoni yako?

Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
 
Umeandika vizuri tu ni ushauri wako kwa Rais Sio Mbaya Ila makonda hana shida kubwa kiivo ukiondoa chuki mliyopandikizwa juu yake ni mchapa kazi kwa vitendo ila mbolongaji kwenye matamshi yake tu ilo haifanyi mimi nimuone hafai ila ushauri mzuri .....

#Mimi CcM
 
Zambi ya usaliti ni sawa nakula nyama ya mtu (Mwl. Nyerere alisema)

Huyo rais wa malawi nayeye atafanyiwa hivyo hivyo like South Africa kwa zuma alichomfanyia Tabo mbeki, muone nayeye kilichomkuta.

Kwahiyo kushabikia ya malawi ni uendawazimu! Nachama cha upinzani tanzania kinachoweza kuchukua nchi
Nakuleta haya uliyo yaandika Hakipo. Naikitokea CCM wakasaritiana basi ujue ndo nwisho wa utawala wao.

CCM wako makini sana nahilo swala.
Mpaka atokee mwenda wazimu ndani ya CCM kufanya hivyo lakini anaweza asimalize mda wa utawala wake.
 
Mbowe atakumbukwa kwa kuua upinzani, hoja za kijinga kama hizi za mleta mada. Vitisho kuhusu "Guadafhi" (sijui ni nani huyo) Saadam, Milosevic nk haiwezi kufufua upinzani njaa huu wa Tanzania! Nendeni hapo jirani Burundi muone vyama vya upinzani wanavyofanya kazi zao!
 
Kaa uandike ueleweke sio unaandika km mtu asiyejua kusoma
Wakuu atakae elewa anieleweshe
Mwenye masikio na asikie !!ila huu ni ukweli mchungu naamini baada ya Chakwela kufanya maamuzi Yale..wengi viongoz wa kiafrica wenye siasa mgando wamejawa na hofu ya kesho yao!!
Mimi pia aliyesoma alichoandika mleta mada anieleweshe
Bwana Mangikule asante kwa barua hii. Umemwandikia mtu ambaye hapendi ushauri wa mtu, anapenda kufanya mambo kienyeji na mshamba sana wa mambo mengi. Mwisho wa huyu jamaa atauleta mwenyewe kwa ujinga wake ndivyo historia inavyotuonesha.
 
mangikule,

Nadhani upo nje kabisa ya ukweli. Huwezi linganisha hali ya Malawi na Tanzania. Sisi pamoja na mapungufu ya wapinzani lakini CCM imekuwa namfumo wa utawala ambao hautoi nafasi ya wizi wa kupindukia zaidi ya watu wachache ambao hawaathiri mfumo wa utendaji kazi wa serikali.

Pia mfumo wetu wa taasisi za ulinzi na usalama hazina vinasaba vya kufanya yale ya Malawi. Pia watanzania tunaishi kama ndugu na haijawahi tokea tukashindwa kuelewana isipokuwa ni watu toka nje hutuletea umbea ili tuvurugane wachukue gas, madini na mafuta.
 
Kaa uandike ueleweke sio unaandika km mtu asiyejua kusoma
We jamaa utakufa macho, unaoperate ID zaidi ya kumi na kila thread umo, duh huu mkakati wenu Lumumba inabidi malipo yaongezeke, buku7 wanawaonea, hivi kwenye hiyo buku7 mnalipa Kodi?
 
Tumejipanga, Mwaka Huu Wataisoma Number 😀
 
Hivi Makonda amefanya kazi ipi Dar.

Zaidi ya kukurupuka na kushindwa kumalizia au kufanikisha kila analolianzisha.
Usisahau pia katabia kake kakunyima watu haki ya kuishi kalikopelekea Marekani kumpiga persona non grata.
 
Mwenye masikio na asikie !!ila huu ni ukweli mchungu naamini baada ya Chakwela kufanya maamuzi Yale..wengi viongoz wa kiafrica wenye siasa mgando wamejawa na hofu ya kesho yao!!
Usichokijua Chikwela kachukua yale maamuzi kimhemuko! Yani ule mzuka wa kiupinzani ndio aliofanya achukue hiyo hatua ambayo pia ni kaburi kwake mwenyewe.

Kuthibitisha hilo subiri mzuka na akili zikitulia atagundua kachimba kaburi atakalo tumbukia hata yeye mwenyewe na atabadilisha hicho kipengele huko mbele ya safari,!
 
Madaraka hulevya! Kwa sasa hawawezi kuelewa ulichoandika mpaka watakapoana kinatokea!
 
Kwa nchi za Kiafrica mtu kufuata Sheria ni Hadi alazimishwe na akikazimishwa atasema ananyimwa Uhuru?

Najua Mimi sitaweza kuja kuwa Raisi maana itakuwa mara nne ya Raisi aliyepo sasa,

Ni makosa makubwa Sana kiongozi yeyote wa nchi kufuga mchwa kwenye Taifa, Ni makosa makubwa Sana kila dhambi nchini kuilea na ikaendelea kutamalaki, wizi, Ufisadi, Rushwa, zilizokuwa zimelelewa na kufugwa na CCM siku na miaka mingi, na ndio ikawa life style ndani ya Chama na serikalini na ndio ikawa maisha ya kawaida kabisa Kwa kila ofsi utakayoingia,

Ndiyo matokeo ya ubaya unaomwandama huyu Raisi aliyepo sasa, Yeye amekuja kuondoa life style iliyokuwa imezoeleka, ni lazima kuwepo kelele Tu,

Na kama anataka iwepo shwari kama zamani, ayaache hayo mambo, nakuhakikishia hata hao wapiga kelele hatawaona tena, atakuwa Rafiki wa kila mtu,

Na Upinzani uliopo ni wa Aina hiyo, na Vyama pinzani vinapendwa sana Kwa sasa na dizaini ya watu hao na style hiyo ya maisha ya zamani, Upinzani siku zote hauwezi kukataa wapiga Kura hata Kura za majambazi kwao ni Sawa Kwa sababu wao wanataka Dola

Lakini uzuri ni kwamba, bado wenye haki nchi hii wako wengi kuliko hao mchwa,

Na hicho wanachokitamani wapinzani kitokee nchini ni Kwa sababu ya kelele za wasiohaki, na wasio haki siku zote matumbo Yao hushibishwa na visivyo vyao, na Mungu hawezi kukaa Kwa mashetani hawa"

Lakini mwisho wa siku, mtu ukiwa ni mwenye haki, ni vyema pia Sheria zikakutawala, sio Sheria kukutawala, hizi Sheria zetu za Kiafrica kuwalinda watawala si za haki pia na huo ndio ukweli, Unataka kuwa Raisi wetu, kuwa sehemu yetu
 
Mangikule;

Ulivyoanza niliiona point yako nikahisi labda mwenzangu kuna jipya umeligundua dhidi ya cream ya Rais, kumbe umeegemea kwenye Mfano wa Malawi.

Ni hivi kilongola utofauti wa kura chache ndio unaweza kupelekea mahakama kuanza ku doubt na hata Jumuia za Kimataifa kuweka shinikizo la kuangaliwa upya uchaguzi.

Utofauti wa kura 38% dhidi ya 35% huu unawazika na ukiingia ndani unaweza kukutana na rafu za hapa na pale YES ila si utofauti wa asilimia 58% kwa 32% hakuna Jumuia yoyote inaweza kuutizama uchaguzi huu kwa jicho la figisu.

Kinga ya kutokushitakiwa ni kweli si ya kudumu ila mchakato wa kuiondoa pia sio wa kitoto pia kutegemea na Rais na Baraza la Usalama la nchi hiyo litakua na maoni gani? Mfano kilichotokea Kenya baada ya uchaguzi nk.

MAONI YANGU
Kuna usemi wa kimombo usemao "the end justify the means" JPM ni kweli yapo maeneo anaifumbia macho sheria, lakini angalia pros na cons za kama angeamua kufuata Sheria.

Mfano ununuzi wa Ndege;
Japo nijambo ambalo liko katika ilani lakini PPRA ACT haikuzingatiwa kwani kwa kufuata Sheria hiyo ingemchukua si chini ya miaka 3 kufanikisha mchakato ambao ameweza kuufanya ndani ya mwaka mmoja.

NCHI NI YA KWETU NA SHERIA NI ZA KWETU PIA.

Pili ujengwaji wa Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme Mto Rufiji, lilipingwa ndani na nje ya nchi kwa kisingizio cha kujaribu makazi ya wanyama na mazingiza.

Isivyokua bahati hakuna aliyekua tayari kuja na alternative zaidi ya kutaja madhara. Sasa tujiulize je wanyama ni bora kuliko Mama zetu na wake zetu wanavyokufa mahospitalini kwa kukosa huduma ambazo vifaa vyake vinatumia umeme?

Je viwanda vyetu ambavyo vingekua chachu ya kutengeneza ajira kwa vijana wetu kuliko Swala na Simba na Tembo?

HAITATOKEA UKAMPENDA MTOTO WA JIRANI KULIKO WA KWAKO, HIVYO MZUNGU HAWEZI KUKUONA WEWE UNAENDELEA KEEP ASI CHA KUTISHIA SOKO LAKE.

Wasalaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…