Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Watanzania Ujue Mungu anatuona nafikiri kwa uhakika kuna wengine wanacommenti bila ya kusikiliza kilichosemwa kwenye hiyo hotuba.
 
Kwani hivyo vibanda/nyumba zao zilizodondoshwa na tetemeko walijengewa na serikali? Walibweteka wakasubiri kujengewa na serikali? Hivi kulikuwa na tatizo gani serikali ikapeleka misaada kadri inavyoweza na ikatoa pole kwa waathirika badala ya longolongo zisizostahili? Mbona serikali yenyewe imeshindwa kutumia jeshi na kitengo chake cha maafa, nayo tukiiambia imebweteka kwa kuwategemea matajiri ambao ilikuwa inawasimanga kabla itafurahi?
 
mseven katisha.. alikua akichangia udsm pale inaelekea anamapenzi na hii nchi
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Nikama wale walio sema wanaiomba serikali next time iandae kupatwa kwa jua mkoani kwao kwani imekuwa ni kivutio kikubwa sana wakidhani kupatwa kwa jua kumeandaliwa na serikali
 
Nyie Wasukuma akina Masanja mna wakati mgumu sana wa kumtetea mwenzenu, kila siku anakuja na jipya! Kazi yenu itakuwa ni kutetea kila uharo kuwa unanukia vizur
 
Leo Sumbawanga nako wamepata majanga ya mvua kubwa ya upepo na barafu. Kuna nyumba zimebomoka na kuezuliwa paa, mifugo imekufa. OMBI langu kwao wakae tuu kimya maaana wasiombee kutana na tetemeko la maneno.

Mungu akitaka taifa lake limrejee hutumia matukio kama haya. Tutafakari pamoja
 
Sawa mkuu tunasubiri ujenzi wa viwanda nadhani hii ni kauli inayotekelezeka.
 
Kuna kitu kinakosekana.watu wana changa fedha ziende kwa waathirika wa tetemeko la ardhi ili wapate chakula. Malazi na matibabu.Watu wanajua uwezo wa watanzania! Mtu anapo patwa na dharura kama hii siyo rahisi kukabiliana na matatizo yote kwa wakati mmoja.Hivyo kuwaambia wajitegemee kujenga wenyewe ni kama kuwachoma kisu kwenye kidonda.

Binafsi nadhani wangesaidiwa kwanza warudi kwenye maisha yao ya kawaida ndio maneno ya kwamba watu wajifunze kujitegemea kukabiliana na dharura yatolewe.

Ndio maana tunatoa mabati, segment, misumari, magodoro, na vyakula tunataka waathirika warejee kwenye hali ya kawaida haraka iwezekanavyo! Kukaa na misaada ya watu muda mrefu haileti picha nzuri.
 
Wewe ulitaka asemeje?

Hebu rudia tena kusikiliza hako kahotuba hapo huu.


Ulitaka aseme Serikali yangu itahakikisha ndani ya mwezi mmoja wahanga wote Wa tetemeko watakuwa wamesha jengewa nyumba nzuri,na wanapatiwa Chakula mwaka mzima bure,na makaburi ya walio tangulia mbele za haki yana jengwa buree.?

Amesha sema muache mihemuko ya kisiasa kwenye suala la majanga kama hili,tujitokeze kusaidia wahanga, nawewe muhanga usibweteke jishughulishe,Serikali YAKE itatoa mile ilicho nacho,,

Usije sema nimepewa bati 20 nyumba yangu ni ya bati 70.

Hili janga halija letwa wala kuratibiwa na Serikali sema itathaminisha Mali iliyo haribiwa na kukipwa hiyo sahau,utasaidiwa kile Serikali kuu imekipata toka ndani na nje kwa wadau.
 
Tujifunze kukabiliana na changamoto ya mabadiliko,ni bora kuambiwa ukweli kuliko ahadi za kisiasa,mfano ni kipindi cha Mzee wa msonga alivyosemaga serikali haina uwezo wa kuleta mvua na wananchi walimwelewa.
Ukweli upi huo tulioambiwa? Ni nani hajuwi kwamba tetemeko halijaletwa na CCM wala serikali? Ni kazi gani ambazo wananchi wa kagera walikuwa hawafanyi wamelala mpaka sasa unawambia fanyeni kazi? Watu wamepata majanga badala ya kuwa nao bega kwa bega ndio kwanza unatoa kauli za kuwabeza,unaleta siasa na ubabe haisadii.najuwa hata ccm wanajuta kumweka huyu mtu hana utu. Kweli sura siyo roho.
 
Nachompendea Mh prezidaaa ajui mungunya maneno anakupa moja Kwa moja haitaji porojo porojo Sijui hivi Mala vile yupo straight

Kagera wameambiwa ukweli so wasibweteke
 
Serikali lazima itafakari hill kwa kina sana. Je wale ambao nyumba zao husombwa na mafuriko hujengewa sana nyumba mpya na serikali? Wakilianzisha tu mahali fulani, itakuwa ni kawaida na kawaida hugeuka kuwa ni sheria machoni mwa wanajamii. Wale walisaidiwa, kwa nini sisi tunabaniwa?
Wale was mafuriko hadi Leo hii wanaishi kwenye mahema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…