Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Nyie Wasukuma akina Masanja mna wakati mgumu sana wa kumtetea mwenzenu, kila siku anakuja na jipya! Kazi yenu itakuwa ni kutetea kila uharo kuwa unanukia vizur

Tatizo waswahili tumezoea ahadi hewa za wanasiasa. Ndo maana tunadanganywa kila siku na tunakubali. Magufuli kaamua kuwa mkweli of what is on his mind. Go figure.

Hivi kweli kwa akili yako tukufu...serikali inaweza kuwajengea nyumba wahanga wote wa hili tetemeko? Get real bro!
 
Hivi kuna wanasiasa walioenda kule kupiga siasa? Maana tunasikia wengine wameenda kutoa misaada isipokuwa mwanasiasa namba moja ndio hajaonekana huko. Hivi kwani siasa ni nini? Siasa ni maisha, siasa ni kuongoza watu, siasa ni utumishi, Hivyo kama kuna wanasiasa wameenda kule na kuzungumza chochote ikiwa ni pamoja na kutoa misaada hiyo ndiyo siasa safi sio kujifungia ndani. Hata dini zinasema dini safi ni kutunza na kutazama wagonjwa na wenye shida. Kama kusaidia wenye shida ni kufanya siasa basi hiyo ndiyo siasa nzuri. Kama mwanasiasa wa upinzani atakwenda kule akakuta serikali haijawajibika ipasavyo na akakosoa hiyo ndiyo kazi yake na wala sio kosa.

Marekani imepiga mabomu na kuua askari zaidi ya 60 wa Syria ikidai ni bahati mbaya haikuwa lenga wao. Urusi imesema UN ifanye kikao cha dharura kujadili suala hilo. Marekani inasema Urusi inataka kulikuza jambo hilo. Hiyo ndiyo siasa kutumia makosa ya mwenzako kujiimarisha. Huyu analalamika kwakuwa yeye hajaenda kule toka madhara yametokea na hajajionea kwa macho yake mwenyewe kadhia ile na wenzake waliwahi kufika kule na kutoa misaada na kukosoa serikali kwa kutochukua hatua kwa haraka. Kama angefika kule mapema au kabla ya viongozi wa upinzani angejionea hali halisi na huenda haya anayoyasema asinge yasema. Hili ni wazi linamuumiza sana moyoni kwakuwa anaona kuchelewa kwake kumewafanya wenzake kujijenga kisiasa. Na hili haliepukiki katika siasa hata misibani wanazunguza siasa kwakuwa siasa ni maisha. Hapo la msingi ni kupambana na watu wote watakaotumia janga hilo kukusanya michango ya kitapeli kwaajili ya kujinufaisha.

Nafikiri kuna baadhi ya maneno rais hakuwa na haja ya kuyasema kwani yatakuwa yanawaongezea machungu waathirika. Kweli wale watu wamekuwa wakihangaika toka wamepata janga hilo kwa kujaribu kujisitiri na wengine wanaonekana wakijenga vijibanda au hizo kuta kwa shida. Tumewaona baadhi ya wananchi kupitia vyombo vya habari wakilalamika kuwa viongozi wa serikali wanafika na kuwapa pole tu lakini hawapewi misaaa ya kuwafanya wasimame upya au hata ya kujikmu kwa muda mfupi. Sasa sijui kama nao wanatumia nafasi ya maafa hayo kisiasa. Kuna baadhi wamepoteza ndugu kila kitu hivyo wanahangaika na ni vigumu kuamini kuwa wamekaa tu wakisubiri msaada wa serikali. Kuwaambia tena wafanye kazi wasisubiri serikali ni kuwaongezea maumivu kwani toka wamepata matatizo wamekuwa wakihangaika na kuishi kwa shida mpaka sasa hivyo walihitaji faraja zaidi kuliko kusutwa.

Katika hali ya kawaida ili kuwamaliza kisiasa hao aliosema wanatumia janga hilo kisiasa, angewashukuru wote waliofika kule bila kujali itikadi zao za kisiasa na kutoa misaada kwa waathirika au hata kuwajulia hali waathirika na kwamba serikali inatambua michango yao na kusisitiza kauli mbiu yake kuwa kwenye maendeleo au shida za wananchi hakuna itikadi bali tushirikiane kama taifa bila kujali kwamba wewe ni CCM, CDM, CUF, UDP nk Hata wanasiasa waliokwenda kule hatujasikia aliyekwenda kugawa misaada kwa wanachama wa chama chake au kugawa kadi kwa wanachama wapya. Mimi nafikiri hawa wangetiwa moyo zaidi ili watoe zaidi kwa kuwashukuru. Kila mtu anajua kuwa janga lilie kama ilivyokuwa kupatwa kwa jua ni la asili hilikuletwa na serikali, CCM, CHADEMA au CUF. Kinachozungumzwa hapo na wanasiasa hao wa upinzani na wakosoaji ni kwa uharaka kiasi gani serikali imechukua hatua kuwasaidia waathirika wa janga lile.

Kwa mawazo yangu nafikiri pia katika janga kama hili ili kuonesha umoja wa kitaifa na kuleta mshikamano, ingependeza kama rais angekutana na viongozi wote wa vyama vya siasa, kwanza kuwashukuru wale waliowahi kufika kule na kisha kujadiliana nao namna nzuri ya kusaidia ndugu zetu walioathirika. Nina imani hili lingemjenga sana rais kisiasa. Viongozi hawa wangemsaidia kumpa taarifa za ziada kuhusiana na hali halisi on the ground kama walivyojioneana na nini kifanyike kusaidia waathirika. Hii ingekuwa ni taarifa ya ziada baada ya ile ya PM kwani sidhani kama PM alifika kila mahali. Baada ya hapo pia ingependeza kama wangeongozana katika ndege moja ya serikali au hata treni kwenda BK na kutembelea sehemu mbali mbali zilizo athirika huku wakitoa misaada na faraja kwa waathirika. Hakikia ingeishangaza dunia na kumuweka yeye katika chati ya juu kabisa. Maana kwenye misiba ndipo watu wanaogombana hupatana na kuwa kitu kimoja. Hata masuala ya UKUTA yangesahaulika na badala yake wote tungewaona wakishirikiana na wananchi wa Bukoba na kutoka sehemu mbali mbali kujenga KUTA za nyumba za wananchi walioathirika na tetemeko kisha baada ya ujenzi waka kaa kwennye hema kwa pamoja wakipata luch pamoja na kushushia na rubisi. Ingekuwa amazing!

Naweza kuwa nimefikiri kijinga lakini ndio mawazo yangu na sizuiliwi kuwaza labda niambiwe siruhusiwi kuongea kile ninachowaza lakini nimesoma katiba nimeona inaniruhusu kujieleza na kutoa maoni yangu.
 
kikwete alihudhuria misiba mpaka wakawa wanamsema humu ni rais wa misiba,tena kuna mmoja alisema hayo mambo ya kuhudhuria misiba ni mambo ya waswahili teh teh teh,
jk ana hekima

Yule jamaa ana mapungufu lakni sio mtu mbaya
 
Ni mtizamo tu. Serikali za nchi tofauti (baadhi zikiwemo Kenya, Uganda,China} zimechangia. Watu Binafsi wamechangia. Kampuni za mafuta zimejitolea kujenga shule 2 kati ya 4 zilizoathirika. Kati ya misaadi ni pamoja na mabati. Hadi hapo serikali ya Jamhuri ya Tanzania haijatangaza imejipanga kwa kiasi gani. Jeshi la Wananchi lipo. Hatuoni mantiki Jeshi likatumika kujenga nyuma alfu kadhaa kwa misaada iliyopatikana.
 
Ndio baadhi yetu tulikuwa tunasema kukaa kwake kimya ilikuwa ni heri. Akifungua kinywa tu, basi kuna watu ikiwa ni pamoja na wahanga wa janga hili watakwazika. Kazi ya serikali ni nini? Kwa nini basi serikali inakusanya kodi? Ndio, watu wachangie na waliishaanza kuchangia lakini ilikuwa ni WAJIBU wa anayekusanya kodi kuwa wa kwanza ama kutangulia kutoa huduma ya kwanza na kutoa uelekeo wa kitaifa katika kipindi cha masaa 24. Itamchukua muda mtukufu kujua majukumu ya serikali.
Mimi mijadala inayomuhusu nimeamua kuufyata maana naamini kuna watu wakubwa tu hawasikilizi, itakuwa maneno ya huku Jf!? Nasubiria tu nione msema kweli pekee ambaye ni muda nione atakuja na jibu gani
 
Tatizo waswahili tumezoea ahadi hewa za wanasiasa. Ndo maana tunadanganywa kila siku na tunakubali. Magufuli kaamua kuwa mkweli of what is on his mind. Go figure.

Hivi kweli kwa akili yako tukufu...serikali inaweza kuwajengea nyumba wahanga wote wa hili tetemeko? Get real bro!
Tufanye nyumba haiwezekani, mahema ya kuwastil kwa muda nayo!? Chakula je!? Kuhakikisha hawapatwi na magonjwa ya mlipuko je!? Mtu kafiwa, kabomokewa na nyumba, kapoteza vitu kwa asilimia kubwa, watoto, wazee, wajawazito wanalala nje kwa wiki nzima sasa halafu Baba Mkubwa atakuja na kauli "tetemeko halijaletwa na serikali wala ccm, hivyo wafanye kazi kwa bidii"
 
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Nacho kipenda zama hii rais wetu ni msema kweli.
 
Kuna wakati unajikuta ungetamani kuzuia maneno yaliyokwisha tamkwa na mtu mtukufu sana ambayo kwayo utukutu wake unaonekana!
 
Mzee wa Msoga angekua kashefika kitambo sana yaani yule mzee ni binadamu kwelikweli ana maneno ya Busara ana Hekma ana Taaluma ni mwanadiplomasia TUTAKUKUMBUKA DAIMA MILELE MZEE WA MSOGA 😕😕😕.......hivi punde tutakuja kwako tukuombe urudi kwenye kiti chako ukae mpaka 2020 ndio uitishe tena uchauzi.
 
Kuna Kipindi nilisema kuwa huu msemo wa HAPA KAZI TU kuna siku utakuwa kinyaa, naona yametimia haiwezekani mtu kupoteza ndugu na hana pa kulala unamwambia akafanye kazi

Sasa ulitaka awaambie wafanye nini, hovyoo
 
Magufuli is very RIGHT. Maisha yanaendelea. Tusitegemee serikali kutumia rasilimali zake kuwajengea nyumba wahanga. In fact to me, Magufuli angetumia hiyo hela ya michango kukarabati mashule, hospitali na barabara zilizo athirika. Na ndo inapashwa kuwa hivo.

Hili janga ni funzo kwetu sote. Jamani katieni bima nyumba zenu na other valuable properties (by the way bima ya nyumba iko chini mno). Tatizo waswahili kila kitu tunakifanyia mzaha tukitumia visingizio lukuki. Lakini kwa mwenye akili dunia ya leo huwezi kujenga nyumba yako kwa hizi hela za kuokoteleza...ukashindwa kuikatia bima.

Najua wengi tutapiga kelele tukisingizia umasikini (this is a popular excuse so far in our country).......lakini ukweli unabaki. Dunia ya leo...haina msaada tena! Ni jukumu lako kufanya uwezalo kujikinga na haya majanga yasiyotabilika (umeme, mafuriko, tetemeko nk). Ndo maana utakuta wazungu hata akizeeka hawi mzigo kwa ndugu au serikali. Au hata akifa...ana bima yake ya kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele. They always work hard and save for the rainy day!

Leo hii baadhi ya waTanzania wenzetu walioko mambelezz (au hata hapa nyumbani) wanatangulia mbele ya haki...tunaanza kupitisha bakuli! (kusafirisha mwili). This is bad and we should correct this culture. Kateni bima za maisha kwa uhai wenu, nyumba zenu na mali nyinginezo. Tuache hii tabia ya kuishi kwa kutaka kuonewa huruma na binadamu wenzetu. Undugu au urafiki haina maana kwamba tuwe mizigo kwa wenzetu.

Maisha yako. Jukumu lako.

Masanja

Unafiki Mbaya sana,,,eti unawambia wakatie bima nyumba zao,,,kweli alieshiba hamjui mwenye njaa,,,,
 
Miaka mitano tutaona Kama decade kwa mipasho utafikiri mswahili dah aseee.

Sasa hapo "Mswahili" katoka wapi.Mbona nyie mnadharau Waswahili.Mwezi mwite mwezi msimung'unye maneno.
 
Kufanya kazi siku hizi imekuwa fasheni.ni kazi gani ambazo wana kagera walikuwa hawazifanyi mnataka wazifanye ? Kauli zenye ukakasi namna hii kwa watu waliopata majanga hazivumiliki hata kidogo.watu wale wanahitaji kauli za faraja hakuna anayependa kulala nje wakati ana uwezo wa kuezeka kwa nyasi banda lake akajihifadhi na familia yake kwani hizo nyumba zilizopata madhara hapo mwanzo serikali ndiyo iliwajengea hao watu. Wana kagera na watanzania kwa ujumla tuna jambo la kujifunza hapa.

Utadhani labda miaka yote watu Walikuwa hawafanyi kazi wanaitegemea serikali,,,,,,,aisee ni Mtihani kweli
 
Hii makitu ningependa sana itokee maeneo ya idodomya maanake pale kuna magamba wengi sana. Wananchi tujipange haswa sasa sijui ikitokea njaa njaa nchi nzima inakuweje hapo? Naisi tutaanza kuwindana tulane njaaa kwa maneno ya kiongozi wetu. Hivi anawashahuri huyu maanake maneno yake yanatia hasira sana.hotuba zake ziandaliwe na apewe asome ili kuinusuru nchi yetu
 
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.

Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.

Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.

Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
Kwa maneno haya kwa waliopatwa na zahma hii ni sawa na ikitokea tukivamiwa na kupigwa mabomu aje kiongozi atuambie wananchi mtajiju kwani serikali na chama hakihusiki..hii sio sawa.
 
Tatizo waswahili tumezoea ahadi hewa za wanasiasa. Ndo maana tunadanganywa kila siku na tunakubali. Magufuli kaamua kuwa mkweli of what is on his mind. Go figure.

Hivi kweli kwa akili yako tukufu...serikali inaweza kuwajengea nyumba wahanga wote wa hili tetemeko? Get real bro!
Hivi wewe aliyekwambia anataka kujengewa nyumba ni nani? Tangu nchi hii iumbwe ni serikali ipi iliwahi kuwajengea wananchi nyumba waliopatwa na majanga kama haya? Watu wanacho complain ni kauli zisizo na faraja zilizotolewa na mkuu wa nchi.hata kama wakiamuwa wasitoe chochote huwezi kuwambia wananchi msitegemee serikali fanyeni kazi kana kwamba wao hawafanyagi kazi au wamekaa tu kusubiri serikali. Haina shida ndugu zao wapo na watakaoguswa watawasaidia nakuwafariji. Sikutegemea kama rais angeweza kuongea kauli zile achilia mbali kwenda kuwatembelea wahanga wa tetemeko. Wana kagera hawana hiyana wataendelea kumuombea huku wakitambuwa sura siyo roho.
 
Mm majanga ni matukio ya asili yanapotokea huja bila taarifa .tujenge uzalendo wa kusaidiana pale inapobidi kule japan niliona rule mji wa Kumamoto ulipatwa Na tetemeko .serikali imeshajenga Nyumba Na tayar wale wahanga wamehamia .bila kuathiri masharti maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom